Usalama wa Nchi ni jambo tukufu na kipekee sana. Tusibweteke na kumpongeza CDF pekee....

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ametamka wazi akiweka angalizo la uwepo wa wakimbizi ( niseme WAHAMIAJI) kwenye teuzi tena level za maamuzi ndani ya nchi yetu.

Nimeona wachambuzi mbalimbali wakimpongeza kwa kuweka wazi angalizo hilo. Nimemsoma mtani wangu kisiasa Yericko Nyerere akichambua kwa undani maeneo ambayo ujasusi umetamalaki na namna ufundi mkubwa uliofanyika kufifisha kila juhudi ya Taifa kujikwamua

Pamoja na kumpongeza CDF Nkunda, lakini tujitathmini kama Taifa kwamba tumefikaje hapa.. Mamlaka ya uteuzi imeainishwa kwenye Katiba yetu. Tumezoea utamaduni wa viongozi wakuu kuvunja Katiba kama vile kufanya teuzi bila kuzingatia vettings. Unaweza kukuta vetting imefanyika lakini inatupiliwa mbali.

Chama Cha Mapinduzi kimejitwalia mamlaka makubwa zaidi na hatima ya Taifa wameifumbata mikononi mwao. Sasa linapokuja suala la teuzi ama kushinda chaguzi mbalimbali, Chama huamua nani ashinde ama ateuliwe. Hivyo angalizo la CDF limeivua ngup CCM na Mwenyekiti wake kwa kuonesha namna gani wanavyojali maslahi yao zaidi ya maslahi ya Taifa.

Imefika mahala, inapotamkwa ama kuelezewa hoja ya USALAMA WA TAIFA inamaanisha usalama wa CCM hususan nafasi za juu za utawala.

Ushahidi wa haya ni namna ambavyo Katiba na hususan sheria ya uchaguzi inavyovunjwa wazi wazi kwa kufanya kampeni kwa mgombea wa CCM wakati kipenga cha uchaguzi hakijapulizwa bado.

Wakimbizi kuteuliwa na kuwekwa kwenye nafasi za maamuzi ya nchi ni jambo hatari sana kwa usalama na ustawi wa nchi yetu.

Tujitathmini, tuchukue hatua kusahihisha hili kosa kubwa.

Ninapata hisia kuwa yule aliyeamrisha jeshi kufanya usafi tarehe 24 anaweza akawa kaguswa na tamko hili.


Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki JamiiForums
 
Matatizo yakianza jeshi litakuwa la kwanza kulaumiwa, kitendo cha Kagame kutuma watu wake nchini na kuteka watu na kuondoka nao kwa rais makini ni Kutangaza vita Ila kwa sababu Kagame ana watu wake Hana hofu.

Rais anatakiwa ajue majukumu yake na sio kuchambana Kama tuko kwenye taarabu, amewapa wageni kuendesha bandari bila kuangalia usalama wa nchi, anagawa mbuga zetu bila kuangalia maslahi ya nchi, Kama ana akili ajue huo ni ujumbe wa wazi toka jeshini, badala ya kuweka watu mahiri usalama wa Taifa anaweka wale watakaolinda maslahi yake ya uongozi hayo ndio matokeo yake.
 
Sio muda wa kunyosheana vidole?
Tanzania sio kisiwa.

Kuna mtu anaongelea ujasusi kwa kutafsiri vitau vya Wazungu.

Watu wapo busy na kucheza na loop hole ya sheria zetu
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ametamka wazi akiweka angalizo la uwepo wa wakimbizi ( niseme WAHAMIAJI) kwenye teuzi tena level za maamuzi ndani ya nchi yetu...
Very right

Acha tupige usafi…. tutaelewana tu
 
Back
Top Bottom