Nchi iko salama na Haijayumba, mpuuzeni Mbowe - CCM

Watu wasidanganyike.
Nchi haiko salama tena.
Je usalama utatoka wapi katika hali hii tunayoiona sasa na ambayo hata Chiligati amekili kuwa ipo ila inatafutiwa ufumbuzi?
 
Mzee Mkandara.. umenichekesha sana hiyo ya "the utamu".. maana inaweza kusababisha TISS wachanganyikiwe tena.
Haya mambo si mambo siku hizi bongo kila mmoja ruksa kurusha matusi hata akina Chiligati.Naona mmomojoko wa waadili umeingia hata kwa wazee.
 
Gloria Tesha
Daily News; Saturday,October 25, 2008 @00:02

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema nchi haijachafuka wala kuyumba kama wanavyosema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na kuwataka Watanzania wapuuze kauli hizo zenye kila dalili ya uchochezi.

Aidha, CCM imemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuacha mara moja tabia ya kumsema vibaya Rais Jakaya Kikwete kwa kile kilichodai kuwa ni udhalilishaji wa kiongozi huyo wa nchi na kamwe CCM haitavumilia jambo hilo.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati, alipokuwa akitoa tamko la CCM kuhusu hali ya kisiasa na kiusalama nchini kwa waandishi wa habari Dar es Salaam.

Chiligati alisema taarifa hizo za baadhi ya wanasiasa zinasambaza hofu, woga na wasiwasi mkubwa si kwa wananchi tu, bali hata kwa wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza na ambao tayari wapo nchini.

“CCM inasema nchi ipo salama na haijayumba kama wasemavyo hao wapinzani na mali za wananchi na wawekezaji zipo salama hivyo kauli hizo ni za watu walioishiwa sera,” alisema Chiligati.

My Take:

Hivi demokrasia lazima iwe na heshima na uungwana?

Maneno haya ya Chiligati bado yana mantiki aliyokusudia? Je, ni kweli nchi ipo salama na haijayumba kama wasemavyo wapinzani? Watanzania mnaonaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom