NCCR yamtaka Mh Ezekiel Wenje kuomba radhi

Kwanza ni miongoni mwa watu walioshiriki vurugu za kuua NCCR enzi ya Mrema.Pili alimuelekeza mgombea urais wa NCCR Hashim Rungwe asiiseme vibaya CCM.Tatu alikuwa akiishambulia CDM muda wote wakati wa uchaguzi mwaka juzi.Nne aliitukana CDM kwamba ni chama cha kumwaga damu kutokana na maandamano yake.Unataka ushahidi gani tena zaidi ya huu?

Kaka sisi waswahili tuna msemo 'ASIYETAKA KUJUA MAANA USIMWAMBIE MAANA MAANA HATA AKISHAJUA MAANA AITAKUWA NA MAANA.
 
Hawa NCCR hawajui kuwa zama za kumezeana zimeisha? Dada yake Mbatia, mama na Baba mmoja Nderakindo kessy amepewa kiti cha CHADEMA EALA na CCM, halafu wamezee tu! Waliangalia nini mbali na uccm? Haiku ajabu kwa CUF kwanza walistahili kiti lakini pia ni washirika wa CCM kwa kinachoitwa mwafaka Zanzibar, NCCR wana nini na CCM? Kwanini wanakereka kuambiwa ukweli? Uteuzi wa Mbatia una nini zaidi ya UCCM, Kikwete aliangalia nini Kama siyo kuhadaa ulimwengu kuwa na wapinzani nao wamo. Wafunike kombe mwanaharamu apite haya mambo yana mwisho.
 
mkubwa!....Mimi napingana na wewe Mbatia ni CCM "C" na sio CCM "B" na ndio maana wanamshambulia Wenje,kwani Wenje kakosea kasema "B" badala ya "C" kwani "B" inawenyewe

Ok nimekupata mkuu kumbe ndio maana wamekuja juu?kama angesema ccm c" wasingelalamika.
 
i support wenjes statment.

Hivi unatarajia mbatia atamsemea ubaya jk hata kama kaliboronga??

The answer is no

kwa hiyo mbatia = ccm b
 
Safi sana wagawanye uwatawale , Jk uliganya kazi kubwa sana kumpa ubunge Mbatia

Mfumo wa "Divide and Rule" ni kielelezo tosha kuwa upaende mmoja ni lazima uwe mtumwa na mwingine mtwana....
Binafsi naamini kikatiba Mbatia hana hatia kwani mamlaka iliyompa hiyo nafasi ni mamlaka ya Urais na wala si Mwenyekiti wa CCM au Amri Jeshi Mkuu...
Imefika mahali kina Wenje na CDM wajifunze kuwa watu makini si lazima kila jambo kulipinga hata kama halina mantiki, hiyo si dhana halisi ya upinzani wa kisiasa...
 
Let's do a simple arithmetic here.

If A=B and B=C then, A=C.

We can conculde that A=B=C! Maana yake ni hii. Kama CCM=CUF na CUF=NCCR Mageuzi ndiyo kusema CCM=CUF=NCCR.

Huu ndiyo uhusiano uliopo baina ya vyama hivi vitatu vya CCM,CUF na NCCR. Kama kuna mtu anapinga hili alete hoja zake za kutetea kwamba huo uhusiano haupo. Kwenye hesabu lazima kuwa na proof ya kuthibitisha kuwa ile kanuni au formula ni sahihi.

Sasa ili ku-prove ukweli wa kanuni ya A=B=C ni kwamba: Rais Kiwete ana mamlaka kikatiba ya KUTEUA WABUNGE MPAKA 20 KWENYE BUNGE LA JAMHURI. Mpaka sasa ameshateua Wabunge zaidi ya KUMI toka CCM. Hivi majuzi KAMTEUA MBATIA-M/kiti wa NCCR kama Mbunge. Lakini pia alishawahi kumteua Mbunge toka chama cha CUF miaka ya 2005-2010! LALKINI KIWETE HAJAWAHI TEUA MBUNGE TOKA CHADEMA.

Q.E.D(Quite Easily Done)!
 
Machalia na Mkosamali lazima watambue kuwa wako kwenye chama ambacho ni so unpopular among Tanzanian,ndio sababu wengine walidiriki kukiita MASIHALA MAGEUZI,Mbatia sio mpinzani wa dhati ilo hata kipofu analiona,yeye ni opportunist ni type ya watu kama Shibuda na hawana future yoyote kwenye siasa ya nchi hii kwani historia itawahukumu.Masalia na Mkosamali bado ni vijana sana na endapo mtaweza kusoma alama za nyakati na kucheza karata zenu vizuri bado mna future kubwa kwenye siasa lakini msitegemee NCCR itawafikisha popote,kwani so far ni chama cha Kibondo na Kasulu kwingineko ni historia tu,nina uhakika M4C ikiingia Kibondo na Kasulu 2015 hamtapata kitu.Mkosamali kumbuka ulipata kura za Maruhani tu,si kwamba unapendwa sana.
 
Sina uhakika sana kama Chadema kimeshafikia hatua ya kupambana na vyama vyote siasa ikiwemo CCM,Juzi nasikia Dr Slaa naye kamshambulia Seif Sharif,sasa wakianza kushambulia kila chama cha siasa bila kutumia diplomasia inaweza fika sehemu ikawa ngumu kwao kupata ushirikiano wa kisiasa hapo mbeleni!
Chadema wakukmbuke bado ni chama kinacho jiimarisha kisiasa hata kama CCM itakufa wao wanahisi hakuna vyama vingine vitakuwepo?Umesha jenga uadui na kila chama cha siasa unategemea nini ?CCM pamoja na kuwa chama tawala kinajitahidi kisijenge uadui na vyama vya siasa unategemea CCM wajinga?
Chadema wajaribu kupunguza jazba za kisiasa au kujidanganya kwamba wao pekee yao wanaweza kufanya shughuli za kisiasa bila ushirikiano na vyama vingine vya siasa!
Wanasema hivyo vyama ni CCM B Au C Je ninyi mnashindwaje kuwarubuni vikawa Chadema B au C kuongeza nguvu yao ya kisiasa au hata kuongea lugha ya kidiplomasia kuweza kujenga umoja zaidi?
Mfano mzuri,Zitto alipokuwa anakusanya saini sabini za wabunge huko bungeni kama sio CUF na NCCR na baadhi ya wabunge wa CCM kutoa ushirikiano angefanikiwa?
Kesho kuwe na kadhia kama hii huko Bungeni Chadema watake ushirikiano kutoka CUF au NCCR kweli watapata ushirikiano tena?
 
Sir Leem

Hoja yako hainamashiko. Sikuelewi unazungumzia uhusiano gani kati ya CHADEMA na vyama vingine. Kumbuka tu kwamba uhusiano wa CCM na CUF na NCCR ni wa kinafiki na wa kutaka KUVIDHOOFISHA vyama vya upinzani. That is the plan. Usitegemee ati CCM aanzishe ushirikiano na chama pinzani ili aje kukiachia KUSHIKA DOLA. Forget!

Kama unajidanganya kuwa kuna ushirikiano kama huo,then you must be day dreaming!!!
 
nimemuona anatoka povu kabisa kumtetea boss wake. Kila mtu anajua kuwa mbatia ni kibaraka na hata hashim rungwe alitutanabaisha, pia kila mtu anajua kuwa mbatia ni bwabwa. Siasa za kujipendekeza namna hiyo za huyu machali zinatia shaka kubwa na kukatisha tamaa vijana wenye ambition ya siasa maana amekuwa kama ni house boy wa mwenyekiti kwa kukubali kutumwa na kutumiwa. Heri angekanusha mbatia mwenyewe.

kaka hizi shutuma zako ni nzito sana hivi ukiambiwa uzithibitishe utaweza? Au unachangia hoja kwa kufuata mkumbo, hebu jaribu kukosoa maandiko yako kabla hujayapost..be prudent
 
huyu jamaa anataka waombwe msamaha na mh Wenje niaibu kwa NCCR kikubwa kama wanataka kuheshimika wasiongozane na ccm
 
NCCR- Mageuzi wamewajia juu wapinzani wenzao, Chadema. Wanawashutumu Chadema kwa kuwaita NCCR- Mageuzi ' CCM 'B'!
Tumemsikia Mbunge Machali akionyesha machachali yake ya kisiasa. Naye amewaita Chadema ' mahayawani' Neno ' hayawani' lina maana ya ' mnyama'- mtu kuitwa hayawani ina maana ya mtu ' mshenzi'- usiyestaaribika kama alivyo mnyama. Nalo ni tusi, si ajabu nao Chadema wakaja na kauli ya kuwataka NCCR- Mageuzi wawaombe radhi kwa kuwatukana hadharani!
 
Unajua tofauti ya mke na kijana mkubwa wa kiume kwa baba yake??? Mke huwa hakui kwa mme wake, kijana wa kiume hukua na baba kumwachia majukumu ya kuendesha mji au masuala ya familia. In summary CDM ni kijana mkubwa wa kiume na NCCR ni kama mke kwa CCM, tena mke mwenza na CUF, haishi kulalamika.

Wakati mwingine baba huwa hataki kumwachia madaraka kijana wake lakni familia inamshinikiza kuwa masuala makubwa maakubwa amwachie kaka CDM, apumzike kulinda afya yake. Hakuna sehemu utasikia masuala makubwa makubwa mwachie mama au mke wako, hakuna narudi.

CDM mwendo mudundo, vijana taifa la leo enzi za la kesho hiyo ni kwa CCM.
 
NCCR- Mageuzi wamewajia juu wapinzani wenzao, Chadema. Wanawashutumu Chadema kwa kuwaita NCCR- Mageuzi ' CCM 'B'!
Tumemsikia Mbunge Machali akionyesha machachali yake ya kisiasa. Naye amewaita Chadema ' mahayawani' Neno ' hayawani' lina maana ya ' mnyama'- mtu kuitwa hayawani ina maana ya mtu ' mshenzi'- usiyestaaribika kama alivyo mnyama. Nalo ni tusi, si ajabu nao Chadema wakaja na kauli ya kuwataka NCCR- Mageuzi wawaombe radhi kwa kuwatukana hadharani!

Hii umeikopy kwenye blog ya Mjengwa au...?
 
Back
Top Bottom