Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Pasco, thank you. I understand that it is only human to question the motive and intention of ones act. It is even more so when that person is unknown or the act itself is not popular.

I have been in out-of-the-picture politics since 2004. The reason was simple, I should concentrate on my profession and set a base. I did that until last year when i contested and won the Mabogini Ward Councillorship.

Now I am serving my people, my country. The drive is a feeling of obligation and duty. And, as a person the satisfaction that by doing good I will have played my part.

I will admit one thing which many wouldnt publicly or openly admit. I want to be and feel a hero. I want to be appreciated and praised for towering down the stronghold of injustice.

We human beings are created in the likeness of our God. Our God is a God of praise that is why he wants us to praise him and serve him. We sing his praises. He is requires us to do so and by doing so he blesses us.

I am ready to go for this. I have all my nerves ready for the outcome. But I am trustful it will all be safe and the objective will be reached.
 
Malengo ya CHADEMA ni kupindisha sheria, kukiuka sheria na kuvunja sheria? Nani anatakiwa kutilia mashaka uanachama wa mwenzake? Ningetegemea kama mwanachadema uwe mstari wa mbele kupigania haki na ukweli. Kilichotokea Arusha hakivumiliki na lazima kipingwe kwa nguvu zote.

zaidi, soma maelezo yangu na utoe tafsiri yako. Au toa msimamo wako. Msimamo wangu uko wazi. Wabunge hao sio wajumbe wa halmashauri hizo. Nitausimamia msimamo wangu na uanachama wanguu utabaki.

Mwisho, unaandamana nchi nzima ili iweje kama hutaki haki itendeke? wewe ni mwanachama wa kipekee kabisa. Ukishaandamana halafu? Kwa hiyo kwa sababu tumepanga kuandamana basi tusitafute haki mahakamani? Sitakushangaa. Ukisoma nilichosema utaelimika na kuelewa nini cha kufanya.

Just a quick one hivi rekodi yako katika sheria umehusika katika kesi ngapi na za namna gani? Nijuavyo mimi weledi wa sheria waliopo Chadema ni wengi kama Dkt mwenyewe pamoja na Tundu Lissu hawa hawajaliona hilo? Kama wameona na wamekaa kimya wewe ungeanza na uamuzio wa kujitoa chamani na kisha uwashitaki uwezi kushona knguo ukiwa umeivaaa Alberto mzee wa kugoma chuoni.
 
Just google 'blacmail definition' halafu uandike tena.

Kama umeelewa nilichomaanisha hiyo tu yatosha.

Wewe ni mnafki.
Unasema wewe ni diwani wa chadema vilevile ni mwanasheria. Sasa hizo tofauti zote ulizoorodhesha hapa hukuziona tangu mwanzo? Ulitoa ushauri gani. Au ulisubiri watu wafe ndio utafute umaarufu. Wewe una umahiri gani katika sheria kumshinda Marando au Tundu lisu.
Kama unataka kuwashtaki nenda kawashtaki, kuna haja gani ya kutupigia makelele hapa?
Umetumwa au unajituma kuleta chokochoko, na lengo lako na huyo aliyekutuma halitatimia.

We are watching you with close eyes as we did to Zitto (Najua Zitto alikuwa rafiki yako pale Daruso, hivyo baada ya mpango wake wa kuvuruga chadema kama alivyotumwa na Rostam kushindikana, ameamua kukutumia wewe. Huna ushawishi huo)
 
Msando nakuheshimu sana,ila nakukumbusha kuwa fani ya sheria ni mfu tuliyeazimia kumlea milele. Nasema ivi kwa sababu fani hii imekariwa, samahani kwa kusema kuwa na 'learned illiterates'. Haiwezekani tukaendelea na upuuzi wa sheria zetu. Ingewezekana tungefuta fani hii Tanzania,sheria ndo imetuletea Mikataba feki,ujinga wa Dowans na uchwara mwingi. Sheria ni fani isiyokuwa updated inasubiri wabunge wa std7,8 na form4 wa ccm na maprofesa wa sociology,education na physics wakae bungeni kurekebisha sheria. Hapa fani imekufa. Igeni kwa wahasibu jamani kila mwaka wanafuta na kuingiza mabadiliko ktk sheria kuendana na walati. Sheria wamelala wamesubiri profesa maji marefu,mbunge ccm hawaelekeze kufuta sheria mbovu na kandamizi. Ni ajabu kuacha legalism ichukue hatamu. Mkuu kwanza jitaidi kuikwamua sheria kutoka mateka,undeni bodi ya sheria si kusubiri darasa la saba wabunge ndo watengeneze sheria. Futa sheria za kale,mfano,eti kubeba elfu nyingi mfukoni ni kosa kisheria na unapaswa kuomba ulinzi ku escort ela,hapo apo serikali ina noti kubwa zaidi kama sh.elfu 2,5 na kumi. Mkiacha sheria ndani ya wanasiasa,naona kama tunapoteza wakati vile! Mwisho, mh.Alberto,all the best. Ktk suala lako hii hakuna wa kukushangaa,ata washtakiwa wenyewe watakufuraia ukiondoa na mkanganyiko huo. Ila ungemuondoa mwanasheria mkuu,maana kwa udkteta wa taifa letu,hoja yako nzuri inaweza kukwamishwa na watu kama hawa. Siku njema.
 
DieHard,

Wanaweza wakawa wameliona au hawajaliona hilo. Sijazungumza nao.

Lazima utofautishe uamuzi binafsi wa mtu kutokana na uelewa wake na uamuzi wa chama.

Ninachokiona hapa ni mawazo na imani kwamba ni makosa makubwa kufanya jambo lolote ambalo linagusa chama chetu hata kama jambo hilo liko wazi. Hata kama jambo hilo ni kinyume na sheria.

Hayo si mawazo ya viongozi wa Chadema. Ni mawazo ya wale ambao ni mashabiki.

Ninachokisema na nitakachokifanya Chadema wameshafanya kama Chama kwa njia ya maandamano. Chadema ilipinga na bado inapinga uhalali wa Mary Chitanda.

Kujitoa kwenye chama? Sio leo wala kesho. Siwezi kukimbia chama changu kwa kile ninachokiamini. Ni jukumu langu kusimamia imani yangu ndani ya chama. Ni siasa nyepesi na woga kujitoa uanachama kwa jambo kama hili.

Siasa zetu bado zimejengeka kwenye misingi ya 'taboo'. Lazima misingi hiyo ivunjwe na ikome. Eti mtu anafukuzwa uanachama bila kufuata utaratibu anahamia chama kingine. Kwa nini? Una haki ya kukishtaki au kumshtaki aliyekufukuza bila kufuata utaratibu au kwa uonevu. Chama sio cha mtu binafsi, ni taasisi.
 
Ndio maana tunadai katiba mpya! Usitumie nguvu nyigi mahakamani, itakula kwako. Kwa kuwa kuna fursa ya katiba mpya, tumia nguvu nyingi kuweka sawa kipengele hicho ktk katiba mpya. Nakuunga mkono katika hoja, ila si katika njia!
 
Just to let MsandoAlberto know that I acknowledge this thread and I have no comment, am learning
 
Pasco, thank you. I understand that it is only human to question the motive and intention of ones act. It is even more so when that person is unknown or the act itself is not popular.

I have been in out-of-the-picture politics since 2004. The reason was simple, I should concentrate on my profession and set a base. I did that until last year when i contested and won the Mabogini Ward Councillorship.

Now I am serving my people, my country. The drive is a feeling of obligation and duty. And, as a person the satisfaction that by doing good I will have played my part.

I will admit one thing which many wouldnt publicly or openly admit. I want to be and feel a hero. I want to be appreciated and praised for towering down the stronghold of injustice.

We human beings are created in the likeness of our God. Our God is a God of praise that is why he wants us to praise him and serve him. We sing his praises. He is requires us to do so and by doing so he blesses us.

I am ready to go for this. I have all my nerves ready for the outcome. But I am trustful it will all be safe and the objective will be reached.
 
Jabulani,

Katiba sawa. Lakini sheria tajwa iko wazi. Kabla ya kwenda kwenye katiba hiyo sheria lazima ifuatwe kuhusu Viti Maalumu.

Kama Wakili bado sijapoteza imani na mahakama. Ni Katiba ndio imeunda chombo hicho. Nitaitumia nafasi hiyo.
 
Ndugu zangu WanaJF,

Hatimaye nafsi yangu imekuwa huru. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu huku nikiumia moyoni nafsi yangu sasa imekuwa huru na niko tayari kufanya lile ambalo naamini halitawapendeza wengi lakini ni sahihi kwa maslahi ya Taifa letu.

Mimi kama Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea na Diwani kwa tiketi ya CHADEMA nimekuwa na wakati mgumu kufanya au kufikia uamuzi huu.

Kwanza, kabisa ni mategemeo ya wengi kwamba kama Diwani wa Chadema ni lazima nifuate utaratibu ndani ya Chama. Nategemewa kusema au kufikiria vile chama au wanachama wengine wanavyofikiria. Hapana.

Pili, nategemewa kwamba nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakisaidia chama kukua na kupendwa zaidi (njia zile ambazo wengine wanaona ndizo sahihi ikiwa ni pamoja na kutosema ukweli au kukemea uovu ili mradi chama kitanufaika).

Tatu, nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakidhoofisha chama cha mapinduzi (CCM). Hata kama ni kwa uonevu au kwa kupindisha ukweli (mara nyingi kinachosemwa dhidi ya CCM ni ukweli na ni mara chache sana watasingiziwa au kuonewa).

Nne, kama Mwanasheria na Wakili nimtetee na kumlinda mteja wangu. Hilo nitafanya daima.

Lakini katika hili, nitafanya vile ambavyo nafsi yangu inanituma kufanya na kwa faida ya nchi yangu. Pia vile vile kulinda heshima na fani ya sheria mbele ya jamii.

Nimeamua kuwashitaki Waheshimiwa Wabunge wafuatao;

1. Mh. Grace Kiwhelu - Viti Maalum (Moshi Vijijini) - CHADEMA.

2. Mh. Lucy Owenya - Viti Maalum (Moshi Mjini) - CHADEMA.

3. Mh. Mary Chitanda - Viti Maalum (Tanga) - CCM.

Pia katika kesi hizo nimemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Waheshimiwa Wabunge hawa ni wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Halmashauri ya Manispaa Arusha.

Ni ukweli usiopingika kwamba Waheshimiwa hawa ni wateule wa vyombo (organs) vya vyama vya siasa i.e. CHADEMA na CCM. Vyombo hivyo UWT na BAWACHA vilivyowateua haviko ndani ya Halmashauri husika. i.e Hai na Arusha. Vyombo hivyo viko nje ya Halmashauri hizo hivyo hawastahili kuwa wajumbe.

Sheria husika kuhusu Wabunge wa Viti Maalumu kwa Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa Sheria Namba 7 ya 1987 inasema hivi (kifungu cha 35(e):

35. Constitution of district councils

(1) Every district council shall consist of–

(a) members elected one from each ward in the area of the district council;

(b) three members appointed by the Minister;

(c) the Member or Members of Parliament representing constituencies within the area of the district council in the Assembly; and

(d) such number of women members who are qualified to be elected to the council, being not less than one third of all the members referred to in paragraphs (a), (b) and (c) to be proposed by the political parties represented in the Council in such numbers as shall be proportional to the number of the members of those parties elected to the Council, who the electoral authority shall declare to have been elected into the Council;

(e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Kwa kiswahili naweza kusema Kifungu hicho cha sheria kinasema hivi;

Mbunge mwingine yoyote ambaye uteuzi wake umeanzia kwenye vyombo vya vyama vya siasa ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya.

kwa upande wa mamlaka za Majiji sheria husika ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 13 ya Mwaka 2006 kifungu cha 17 ambacho kinaongeza kifungu kidogo (d) kwenye kifungu cha 19 cha Sheria Namba 7/1982 kwamba;

(d) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno; nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili.

Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda Arusha. Alitumia siasa kutoa tafsiri hiyo huku akijua wazi kwamba anakosea.

Mwanasheria Mkuu alikosea zaidi pale alipoamua kuchukua jukumu la kutoa tafsiri ya sheria badala ya kuiachia mahakama itoe tafsiri hiyo. Sheria zote mbili za Serikali za Mitaa (Namba 7 na 8 za Mwaka 1982) zimetoa utaratibu wa kufuatwa endapo kutakuwa na maswali kuhusu uhalali wa mtu kuwa mjumbe kwenye Halmashauri. Sheria inasema hivi:

43. Decision of questions as to membership of council

(1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

(a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

(b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

(c) a person claiming to have been a candidate at the election;

(d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

(e) the Attorney-General.

Mwanasheria Mkuu anatajwa kama mmoja wapo wa watu wanoweza kupeleka maombi mbele ya Hakimu Mkazi ili atoe uamuzi kuhusu uhalali wa ujumbe wa mtu. Hakufanya hivyo badala yake watu wamekufa, mali zimeharibika na wengi wameumizwa. Pia serikali inaingia gharama kuendesha kesi dhidi ya walioandamana.

Ni sababu zipi zilimfanya Mwanasheria Mkuu asilione hili? Kwa nini alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu Mary Chitanda? tangu uchaguzi ulipomalizika, mvutano ulipojitokeza tarehe 17/12/2010 mpaka tarehe 5/01/2011 Mwanasheria Mkuu hakuwa amepata jibu la nini kifanyike kutatua Mgogoro wa kama Mary Chitanda ni mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha au la?

Kwa kusoma vifungu hivyo vya sheria hata mtoto wa mwaka wa kwanza wa stashahada ya sheria (Certificate of Law) angeweza kutoa tafsiri sahihi ya Mbunge wa Viti Maalumu anatakiwa aingie kwenye Halmashauri ipi. Ni Halmashauri ile ambayo chombo kilichomchagua kipo. Kama alichaguliwa na UWT Tanga basi anaingia halmashauri ile ambayo UWT Tanga ipo. Kama alichaguliwa na BAWACHA (Baraza la Wanawake Chadema) anaingia pale ambapo baraza hilo lipo. Na sio Halmashauri yoyote nchini!

Natambua Mods wanaweza kuamua hii mada iende kwenye Jukwaa la Sheria. Napinga mada hii kupelekwa huko kwa sababu siasa ndio ilitumika kufikia tafsiri hiyo na athari zilizojitokeza ni za kisiasa zaidi. Sheria iko wazi.

CHADEMA waliamua kutumia njia ya Maandamano kupinga kile kilichoonekana ni dhuluma ya wazi na uvunjaji wa sheria mchana kweupe. Walitaka kuonyesha umma ni jinsi gani baadhi ya watu wako tayari kukanyaga sheria za nchi ilimradi tu matakwa yao yatimie. Kilichofuata ni kupigwa nakutawanya kwa nguvu kubwa bila sababu. Labda sababu ilikuwa ni kuficha ukweli.

Naamini kwamba Mungu ana njia nyingi za kutufanya tuone ukweli na sasa muda umefika. Ni muda wa mahakama kuiangalia Sheria inasemaje na kutoa tafsiri sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa.

Hili nitalisimamia na kulipigania. Hata kama Chama changu kitaguswa kwa msimamo wangu niko tayari kutetea ukweli na sheria za nchi. Hicho ndicho kiapo changu mbele ya Jaji Mkuu mwaka 2007. Siwezi kukivunja nitakuwa kama wao.

HITIMISHO.

1. Waheshimiwa Grace Kiwhelu, Lucy Owenya na Mary Chitanda SI wajumbe halali wa Halmashauri za Hai na Arusha.

2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (pamoja na Katibu wa Bunge na Tume ya Uchaguzi) walitoa tafsiri ambayo si sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda, Grace Kiwhelu na Lucy Owenya kama wajumbe wa Halmashauri hizo.

Siasa imetuponza. Maamuzi ambayo yalitolewa kisiasa ili kufanikisha nia na malengo ya kisiasa yamesababisha watu watatu (3) wamepoteza maisha, mali zimeharibiwa na wengi wamebaki vilema.

Hakukuwa na sababu ya polisi kuzuia maandamano ya amani yaliyopangwa na CHADEMA. Hiyo ilikuwa ni njia ya kuficha uovu ambao sasa utajulikana. Uzembe na ubinafsi vinaimaliza hii nchi.

Wote tusimame imara na kutetea ukweli. Tuungane kwa pamoja kuwasaidia wananchi wetu masikini ambao sisi wasomi tunachokisema wanakiamini hata kama tunawadanganya.

MwanaJF yeyote anakaribishwa kuungana nami kama mlalamikaji katika kesi hizo mbili za kuweka kumbukumbu sawa. Kesi dhidi ya Wah. Grace Kihwelu na Lucy Owenya zinafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kesi dhidi ya Mh. Mary Chitanda inafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Nawasilisha taarifa.

Mheshimiwa msomi, ninakushukuru kwa homework uliyoifanya. Nina swali dogo tu kuhusu wabunge wa Chadema viti maalum. Ninayo taarifa kuwa hawa walichaguliwa na BAWACHA kitaifa na sio kutoka kwenye majimbo. Hili nalo likoje kisheria?
 
Msando naomba ufafanuzi wa thread #75 kwa mtazamo wa kesi unayokusudia kuifungua.

RM
 
i am following, its so interesting. kama roho na moyo wako u radhi na unajua unachofanya, go on, dont listen to negativity.
 
Msando,
Huku ndiko ninakoita kuitii dhamira yako. Hutakiwi kuendelea kusutwa na dhamira yako mwenyewe kwa maslahi ya mtu, kikundi cha watu au taasisi/asasi fulani. Au kwa kuogopa kupoteza umaarufu, cheo, madaraka,... VITI MAALUM vitaendelea kututesa sana sio tu katika kupindisha sheria kama hizi bali hata gharama za kuviendesha.
Naamini baada ya kesi hizi hata kama utashindwa kuna mabadiliko chanya yatafanyika. Ingekuwa ninajua nami nifanyeje ningeng'ang'ana VITI MAALUM vifutwe kabisa. Wenzetu Kenya hawana upuuzi huu na Bunge lao ni moto wa kuotea mbali.
 
Pasco, thank you. I understand that it is only human to question the motive and intention of ones act. It is even more so when that person is unknown or the act itself is not popular.

I have been in out-of-the-picture politics since 2004. The reason was simple, I should concentrate on my profession and set a base. I did that until last year when i contested and won the Mabogini Ward Councillorship.

Now I am serving my people, my country. The drive is a feeling of obligation and duty. And, as a person the satisfaction that by doing good I will have played my part.

I will admit one thing which many wouldnt publicly or openly admit. I want to be and feel a hero. I want to be appreciated and praised for towering down the stronghold of injustice.

We human beings are created in the likeness of our God. Our God is a God of praise that is why he wants us to praise him and serve him. We sing his praises. He is requires us to do so and by doing so he blesses us.

I am ready to go for this. I have all my nerves ready for the outcome. But I am trustful it will all be safe and the objective will be reached.
Nakushukuru kwa kuwa muwazi, kwa mtazamo wangu, mimi nilikudhania unatarget the big picture ya 2015 bearing in mind age ya Ndesa, ndio maana unaanza kuzichanga karata zako mapema, haswa baada ya kugundua hulka ya watu wa Moshi, wao wanachagua mtu sio chama, nawe umeamua kujitanabaisha kama mtu wao.

Kwa vile wewe ni mwanasheria, na Chadema mnao wanasheria wengi tuu, tena makini na waliobobea, kwa nini hizo hoja zako za kisheria hukuamua kwanza kuzipitishia kwenye chama kupata baraka za chama ndipo uendelee mbele?.

Kwa jinsi ninavyokusdoma, unaonekana uko very confident na unachokifanya, unaonekana wewe ni mtu wa self determination na pia you are a fighter, hauni kuzionyesha hulka hizi mapema asubuhi namna hii, kutapelekea kutuma wrong signal, kwamba you are up to something bigger, na wenyewe wakishakuhisi wewe unaweza kuwa ni tishio kwa himaya yao, unakijua kitakacho kukuta?.

You have been warned, usije kusema hukujua!. Mark my words and when that time comes, I will remind you!.
 
Umechemka !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ushachakachuliwa wewe!........mafisadi ..........washa.....? Sina uhakika ngoja niacha

mimi nazani kama ni kushitaki ungemshtaki mary chitanda na mwana sheria mkuu
kwa nini?...................

Lucy owenya na grace kiwelu wote ni wa bugu wa viti maalumu mkoa wa kilimanjaro kwa hiyo wanaweza pangiwa sehemu yeyote .....
Mary chitanda yeye ni viti maalumu tanga iweje ...achague arusha......walakini hapo!
na huwezi niambia kuwa alipiga kura arusha kwa kuwa alihamishiwa arusha toka tanga lah! Yeye alichaguliwa tanga kuwakilisha tanga na si arusha ....................full stop!

Mwanasheria yeye kashindwa kusimamia sheria.....ashitakiwe.....mshtaki huyo! Full stop
 
...kama sheria iko wazi nakushauri bwana Alberto uendelee kuitendea haki nafsi yako... naamini umefikiria vya kutosha mpaka ulipoamua kuja na huu uamuzi..lakini pia kumbuka una wajibu wa kusaidia chama chako kilichokupa tiketi ya kuwa diwani....
 
Nakushukuru kwa kuwa muwazi, kwa mtazamo wangu, mimi nilikudhania unatarget the big picture ya 2015 bearing in mind age ya Ndesa, ndio maana unaanza kuzichanga karata zako mapema, haswa baada ya kugundua hulka ya watu wa Moshi, wao wanachagua mtu sio chama, nawe umeamua kujitanabaisha kama mtu wao.

Kwa vile wewe ni mwanasheria, na Chadema mnao wanasheria wengi tuu, tena makini na waliobobea, kwa nini hizo hoja zako za kisheria hukuamua kwanza kuzipitishia kwenye chama kupata baraka za chama ndipo uendelee mbele?.

Kwa jinsi ninavyokusdoma, unaonekana uko very confident na unachokifanya, unaonekana wewe ni mtu wa self determination na pia you are a fighter, hauni kuzionyesha hulka hizi mapema asubuhi namna hii, kutapelekea kutuma wrong signal, kwamba you are up to something bigger, na wenyewe wakishakuhisi wewe unaweza kuwa ni tishio kwa himaya yao, unakijua kitakacho kukuta?.

You have been warned, usije kusema hukujua!. Mark my words and when that time comes, I will remind you!.
Msando ana ajira yake tayari ambayo inalipa sana kwa sasa kama waganga wa kienyeji. Hana sababu ya kutishika na CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa sio MAMA YAKE na hasa kama analolisimamia ni HAKI. Endelea Msando.
 
Kwa Mkeshaji, natakiwa kufanya nini?

Kukubali kwamba Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri sahihi?

Nikubali kwamba wabunge wa viti maalumu wanaweza kuingia kwenye Halmashauri yoyote nchini?

Kwamba sheria niliyokuwekea hapo juu si sheria na hakuna haja ya kuiheshimu?

Kama nisipokubali hayo nitakuwa maarufu so let me be. Kama kwa kupinga dhuluma nitapoteza umaarufu acha upotee.

I will stand and say what i believe to be the truth.

Karibu tena.

Albert ndugu yangu,

Uko sahihi!! Unachotakiwa hapa fungulia mashitaka mwanasheria mkuu kwa kupindisha sheria. Then, tutaungana nawe... hawa wabunge na ujumbe wao hawakujiepeleka wenyewe huko, bali mwanasheria. wewe kufa na mwanasheria Mkuu. Kesi itakuwa nzuri sana.
 
Umechemka !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ushachakachuliwa wewe!........mafisadi ..........washa.....? Sina uhakika ngoja niacha

mimi nazani kama ni kushitaki ungemshtaki mary chitanda na mwana sheria mkuu
kwa nini?...................

Lucy owenya na grace kiwelu wote ni wa bugu wa viti maalumu mkoa wa kilimanjaro kwa hiyo wanaweza pangiwa sehemu yeyote .....
Mary chitanda yeye ni viti maalumu tanga iweje ...achague arusha......walakini hapo!
na huwezi niambia kuwa alipiga kura arusha kwa kuwa alihamishiwa arusha toka tanga lah! Yeye alichaguliwa tanga kuwakilisha tanga na si arusha ....................full stop!

Mwanasheria yeye kashindwa kusimamia sheria.....ashitakiwe.....mshtaki huyo! Full stop

hayo mengine yote nayaacha kwako, je kwenye sheria nilizotaja hapo juu, hili linaingia wapi?

Lucy owenya na grace kiwelu wote ni wa bugu (sic) wa viti maalumu mkoa wa kilimanjaro kwa hiyo wanaweza pangiwa sehemu yeyote .....

Nani ana mamlaka ya kusema huyu ni mjumbe au la? Kwa nini hutaki mahakama iseme hicho unachosema wewe? Kama tafsiri ya Mwanasheria Mkuu ina walakini kwanini ya kwako iwe sahihi?

Na hoja ya msingi, kusiwe na muingiliano wa mamlaka. Mahakama ndio chombo chenye mamlaka ya kutafsiri sheria sio wewe, sio mimi, sio wanasheria waliobobea wa Chadema, sio mwanasheria wa serikali.
 
Back
Top Bottom