Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Si suala la umaarufu wala nini, kama wana CDM wanalalamikia Mary Chatanda kushiriki katika baraza la madiwani Arusha kama Mbunge wa kuteuliwa basi waunge mkono kesi hii, ili haki itendeke na si kupinga eti kwa sababu watapoteza Halmashauri ya HAI endapo MSANDO atashinda katika kesi husika. Kama unachukia uonevu chukia pia kuonea, kama unachukia kubaguliwa chukia pia kubagua. Tusiwe tunakasirika na kulalama pale CDM inapoonewa lakini inapoonea tukae kimya. Tusimamie haki na si kusimamia chama.

TAADHALI KWA WAKILI MSANDOALBERTO (wewe ni mwanasiasa wengine sisi ni wanaharakati hatuna chama bali tunasupport chama tunacho amini kitaleta mabadiliko yanayotakiwa hapa nchini) Kumbuka CCM wanampango wa kuvunja Baraza la Madiwani Katika JIJI la ARUSHA na kuunda TUME, hivyo kesi yako hutomkomoa MARY CHATANDA WALA CCM, lakini kwa Upande wa HAI mjini ukishinda kesi utakikomoa chama chako na wanachama wenzako LUCY OWENYA na LUCY KIWELU. Je utaweza kupambana kama ZITTO ndani ya chama? yaani wewe uwe upande mwingine na CDM upande mwingine katika mapambano hayo? Jifunze kwa yanayomkuta ZITTO lakini ukiwa tayari kwa lolote GO ON.

My brother, kama ni mabadiliko hayawezi kuja kwa maneno peke yake. Lazima maamuzi magumu yafanyike na atakayepinga anipinge kwa hoja. Sitarudi nyuma hata kidogo. Mawazo yangu yatabaki kuwa huru na sitaruhusu nitumbukie kwenye dimbwi la mkumbo au ufuasi. Chadema itajengwa kwa mawazo huru na siasa ambazo zi za kufuata mkumbo.

Niseme neno, kwa Mahakama kutoa uamuzi kwamba Wabunge hao sio wajumbe haimaanishi kwamba CDM au CCM vitapoteza halmashauri walizoshinda. Sheria iko wazi kwamba kitakachotokea ni wale kutokuendelea na ujumbe wao lakini maamuzi yaliyopitishwa wakiwemo hayatakuwa batili unless kwa sababu nyingine kama vile kutokuwepo kwa quorum etc.

Kuna watu ambao wanachukulia kwamba Halmashauri ya Hai itapotea. Si kweli. Mwenyekiti wa Halmashauri akishachaguliwa anaendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka mitano. Huo ndio uwoga unaowaingia watu kiasi kwamba wako tayari kuvunja sheria ili mradi Halmashauri ibaki kwetu. Hata kama ingekuwa tunapoteza Halmashauri isingekuwa sahihi kuvunja sheria kisa halmashauri. Tutakuwa na tofauti gani na CCM ambao wako tayari kuua ili mradi ukweli usijulikane? Wako tayari kuua ili mradi Meya awe wa kwao?

Chadema hatuko hivyo na hatutakuwa hivyo. Wanaokurupuka humu ndani aidha si wanachadema au ni wanachadema ambao hawana uelewa wa kutosha na wanafuata mkumbo. Tutawanyoosha tu.
 
Mkiamua kusoma vizuri bandiko la Msando mtamuelewa vizuri na nadhani ni move nzuri na yenue afya njema kwa cdm
 
Mkiamua kusoma vizuri bandiko la Msando mtamuelewa vizuri na nadhani ni move nzuri na yenue afya njema kwa cdm

It will take time for some of them to figure out the content, aim and objective of the move. But with time they will understand. it is unfortunate that some have reacted without giving it a second reading.

At least Albedo you have seen that.

This time around CDM is gooing for the kill.
 
It will take time for some of them to figure out the content, aim and objective of the move. But with time they will understand. it is unfortunate that have reacted without giving it a second reading.

At least Albedo you have seen that.

This time around CDM is gooing for the kill.
Mkuu keep it up naamini watakuelewa tu with tym.

The move has my full support na nitaifuatilia
 

Mwanasheria unaweza kunukuu wapi nimesema umewaonea.

Nilichokuuliza mimi ni priority zako kama katika mambo ya msingi kabisa hilo ni la priorty kwako kwa chama au kwa wananchi.

Pili nikasema isije ikawa ni jambo la haki lakini lina msukumo wa ubinafsi zaidi ndani yake. ndio maana umelipa kipaumbele.

Ulitaka tukuulize nini mkuu ili uhisi kuwa umeeleweka. Mimi nimekupata umeandika kila kitu.

Quote me right nimeandika hivi

Zing, sijasema umeandika popote. Nimesema 'unafikiri'. Fikra si lazima ziandikwe.

Kuhusu priority, mimi kama Mwanasheria na Wakili hili ni priority ya kwanza kabisa. kwangu binafsi, kwa fani yangu ya sheria na wale wote ambao wanaamini katika utawala wa sheria.

Najua kwamba inakera na kuchanganya lakini mwisho wa siku swali linabaki, je hii nchi ina sheria? Kama zipo kwa nini tusizifuate?

CCM hawakufuata sheria ndio maana wakalazimisha Mary Chitanda aingie kama mjumbe kwenye Halmashauri. Hapo ndipo mgogoro wote wa Arusha ulipoanzia. Hayo mengine ni matokeo. Kwa nini tusifike mahali tukatatua tatizo na umma ukaelewa dhuluma iliyofanywa Arusha hata kama kwa njia moja au nyingine itatugusa?

Ni picha gani tunaijenga kwa wananchi kwamba tunalalamika kuhusu Arusha lakini hatusemi lolote kuhusu Hai? Wananchi wanatakiwa waujue ukweli. Mahakama lazima itoe tafsiri kuhusu nani ni mjumbe wa halmashauri ya wilaya au halmashauri ya manispaa.

A price has to be paid and trust me I will pay that price. Come what may. It is enough, enough of all this hypocrisy and pretence.
 
WAKILI MSANDO tupo pamoja katika hiyo kesi yako, nimeweka angalizo kuwa je huko tayari kwa mapambano na chama chako? Maana CDM humu mko wengi, ZITTO kutofautiana kimawazo/kimsimamo na wengi CDM kunamfanya aitwe mnafiki, kibaraka ma mdini ndio maana nikasema hupo tayari?

Kumbuka wanasias wengi wao chama kwanza halafu maslahi ya Taifa baadae kwa uamuzi wako ambao kwangu ni nauona ni sahihi na nauunga mkono lakini naamini utapata upinzani makli toka ndani ya chama chako. Yaani wao hata kama hawana hoja kwao chama kwanza, hivyo usitegemee mtelemko au utaeleweka katika suala hili.

Ndio maana nikakwambia kama ROHO hi RADHI GO ON. tunaokuelewa tutakuunga mkono
 
MHE. MSANDO naomba ufafanuzi wa kisheria kidogo, unasema LUCY OWENYA na GRACE KIWELU wakivuliwa hadhi ya kuwa member wa Baraza la madiwani HAI, CDM hawato poteza nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri na wataendelea kuongoza Halmashauri ya HAI.

Je kuondolewa kisheria kwa Mhe. Lucy na Mhe. Grace kuwa wajumbe wa baraza la Madiwani HAI kwakuwa sheria haikutafsiriwa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakumaanishi kuwa hata uchaguzi wa mwenyekiti ulikuwa batili kwa kuwa kuna wajumbe wawili walikuwa si wajumbe halali ya kikao cha Baraza? Na kupelekea uchaguzi kurudiwa?

Hilo ni swali la msingi, baada ya jibu nikiwa na swali la niongeza litafuata.
 
WAKILI MSANDO tupo pamoja katika hiyo kesi yako, nimeweka angalizo kuwa je huko tayari kwa mapambano na chama chako? Maana CDM humu mko wengi, ZITTO kutofautiana kimawazo/kimsimamo na wengi CDM kunamfanya aitwe mnafiki, kibaraka ma mdini ndio maana nikasema hupo tayari?

Kumbuka wanasias wengi wao chama kwanza halafu maslahi ya Taifa baadae kwa uamuzi wako ambao kwangu ni nauona ni sahihi na nauunga mkono lakini naamini utapata upinzani makli toka ndani ya chama chako. Yaani wao hata kama hawana hoja kwao chama kwanza, hivyo usitegemee mtelemko au utaeleweka katika suala hili.

Ndio maana nikakwambia kama ROHO hi RADHI GO ON. tunaokuelewa tutakuunga mkono

Naloli nakushukuru sana kwa hilo. Hatuwezi kutegemea kwamba chama kitakuwa kwa kufanya yale wengi wanataka kuona tunafanya. Tunapenda kufanya cheap politics tukiamini kwamba tunajenga chama. Hili nimeliona kwa vyama vyote. Ndio tutapata mashabiki lakini kwa nini tusitafute wafuasi na wanachama? Popular politics sio za milele, huwa zinapotea baada ya muda kwani zinatokana na matukio zaidi na nafasi.

Naamini kabisa kwamba CDM itaeleweka na kuonekana chama ambacho hakiweki maslahi yake mbele kwa kuonyesha kwa vitendo kile inachokipinga. Huwezi ukamtaka Mwanasheria Mkuu ajiuzulu kwa sababu ya Dowans halafu unashindwa kumtaka ajiuzulu kwa kutafsiri sheria vibaya matokeo yake watu wamekufa na kujeruhiwa vibaya. Hiyo ni double standard kwani mtu yeyote makini atataka kujua kwa nini unasemea jambo moja lingine unalifumbia macho? That is damaging to the party in the long run.

But again, we are together in this and will keep going. Pamoja daima.
 
MHE. MSANDO naomba ufafanuzi wa kisheria kidogo, unasema LUCY OWENYA na GRACE KIWELU wakivuliwa hadhi ya kuwa member wa Baraza la madiwani HAI ,CDM hawato poteza nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri na wataendelea kuongoza Halmashauri ya HAI. Je kuondolewa kisheria kwa Mhe. Lucy na Mhe. Grace kuwa wajumbe wa baraza la Madiwani HAI kwakuwa sheria haikutafsiriwa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakumaanishi kuwa hata uchaguzi wa mwenyekiti ulikuwa batili kwa kuwa kuna wajumbe wawili walikuwa si wajumbe halali ya kikao cha Baraza? na kupelekea uchaguzi kurudiwa? Hilo ni swali la msingi, baada ya jibu nikiwa na swali la niongeza litafuata.

Hapana, disqualification of one of the member will not automatically nullify the proceedings of the Council. So the decisions made will stand. and that will be the same case for Arusha.
 
Mbona unatusumbua wenzio macho, miwani CCBRT yanatolewa kwa mgao kama Tanesco,,,, si uende mahakamani acha kutushusha stimu...
 
Msando shida kuna wana JF humu ndani hawasomagi thread yote na kuilewa. Mimi nimeisoma thread yako and I have gathered alot. Ila nafikiri hapa mwenye kutakiwa kushitakiwa ni attoney general ambaye alipindisha sheria deliberately.
 
Kisheria ni kweli hawastahili kuwa wajumbe wa halmashauri ya hai au arusha mjini..

Lakini je ni kweli kuwa kesi hiyo itamalizika na ushindi upatikane???
 
Msando shida kuna wana JF humu ndani hawasomagi thread yote na kuilewa. Mimi nimeisoma thread yako and I have gathered alot. Ila nafikiri hapa mwenye kutakiwa kushitakiwa ni attoney general ambaye alipindisha sheria deliberately.

BB, he will be a party. What the law requires is that anyone whose right may be affected by the decision should be a party to a suit or application. The right to be heard.

At the end of the day the AG created the whole mess. He is the one to carry the blame and not the MPs. It is unfortunate great thinking herein (except for few of those who truly are great thinkers) has a different meaning.
 
Kisheria ni kweli hawastahili kuwa wajumbe wa halmashauri ya hai au arusha mjini..

Lakini je ni kweli kuwa kesi hiyo itamalizika na ushindi upatikane???

Let us test the way our judicial system works. We should not fail for not trying. The application has been filed under the cerificate of urgency. I am curious to see what the AG is going to reply. He may try a shot on technicality but the substance remains. He has to wear his burning shoes.
 
MSANDO tupo pamoja, nchi hii inavurugwa kwa watu kuheshimu na kuabudu siasa za vyama na kuyatupa maslahi ya Taifa. Ni vyema tukakubali kuwa kwenye ukweli uongo ujitenga, huwezi sema nyama ya nguruwe ni haramu siwezi kuila lakini mchuzi wake unakunywa. GO MSANDO GO...

Ipatikane tafsiri sahihi ili kesho na kesho kutwa, ieleweke wazi kuwa si lazima usimamie Jambo ambalo si sahihi kwa imani yako na kwa maslahi ya wengi eti tu, kwa kuwa chama kimeona jambo hilo ni sahihi.

Na CDM acheni sheria ichukue mkondo wake na si kuingilia kati suala hili, ONYESHENI KWA VITENDO KUWA CDM NI CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
 
Mbona unatusumbua wenzio macho, miwani CCBRT yanatolewa kwa mgao kama Tanesco,,,, si uende mahakamani acha kutushusha stimu...

Hahahahahaha,man nilikua nime zama sana kufuatilia mawazo ya "great thinkers" ila umenifurahisha sana hapa,thanks for making me lough!

Msando,....you are great man!
One thing that i always learn here in JF is that there are very "great thinkers" in Tanzania who can do great things if they have an opportunity to do that,.....(You are among the few i can see in JF)

On the other hand,...there are very "empty minded","main stream thinkers=literal thinkers" in JF,...if you read this thread from the beginning,you will count so many of them!.....(And its so sad,this category has a lot of JF members)

Go on bro,....but am sure you know the consequences and you are ready for them
 
Msando, unataka Kupigania Ukweli na Haki kwenye Uwanja wa Siasa, it's a Futile attempt! Na huko Mahakamani kwenye Fani yako wewe Unajua fika kuwa kuna Sheria tu, hakuna Haki. Hapa Jamvini ndo Kabsaa, umeona mwenyewe Akili Mseto zilizopo hapa. Could you plz ease my Curiosity a little bit, Why in the First place, mara baada Uchaguzi wa Mayor Arusha Chadema haikwenda Mahakamani badala ya Kuingia Barabarani? Kwani kule sidhani Kama kuna Haki, bali 'Sheria' za Barabarani ndo Kama tulivyoziona!
 
Mkuu Engineer, Nakuheshimu sana ila hapa Hujajenga Bali unabomoa, Msando na Grace ni Diwani na Mbunge wa CDM sasa kutumia Maneno kama haya kwa Grace katika Thread iliyoletwa kwa Nia Nzuri na Msando sidhani kama Umetumia Busara yako Vyema

Nimekupata mkuu asante kwa ushauri na ninaomba radhi kwa hilo
 
Back
Top Bottom