Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Nakushukuru kwa kuwa muwazi, kwa mtazamo wangu, mimi nilikudhania unatarget the big picture ya 2015 bearing in mind age ya Ndesa, ndio maana unaanza kuzichanga karata zako mapema, haswa baada ya kugundua hulka ya watu wa Moshi, wao wanachagua mtu sio chama, nawe umeamua kujitanabaisha kama mtu wao.

Kwa vile wewe ni mwanasheria, na Chadema mnao wanasheria wengi tuu, tena makini na waliobobea, kwa nini hizo hoja zako za kisheria hukuamua kwanza kuzipitishia kwenye chama kupata baraka za chama ndipo uendelee mbele?.

Kwa jinsi ninavyokusdoma, unaonekana uko very confident na unachokifanya, unaonekana wewe ni mtu wa self determination na pia you are a fighter, hauni kuzionyesha hulka hizi mapema asubuhi namna hii, kutapelekea kutuma wrong signal, kwamba you are up to something bigger, na wenyewe wakishakuhisi wewe unaweza kuwa ni tishio kwa himaya yao, unakijua kitakacho kukuta?.

You have been warned, usije kusema hukujua!. Mark my words and when that time comes, I will remind you!.

Ni kweli, kwamba Chadema ina wanasheria wengi. Lakini kumbuka nchi ina wanasheria wengi na hapa ndipo tulipo leo na Dowans.

Ubunge sio kitu ambacho kitanifanya niache au nifanye mambo ambayo siyaamini. I am happy to do my wrk as a lawyer and serve the approximately 15,000 Tanzanians residents of Mabogini Ward. Kuwa Mbunge siyo jambo ambalo ni la lazima.

Tufike mahali tuache kufanya mambo kwa misukumo na mawazo ya kisiasa.

Kama kweli tunaamini CCM haifai na sisi tusikubali kuyumba tusije tukaishia kama wao. Tunachikisimamia ni haki na haki lazima itendeke kwa wananchi kujua ukweli wa yaliyotokea na sheria zinasemaje.
 
Na hao ndio wanaotegemewa na watanzania. Na hao ndio wanaojidai wanataka mageuzi. Kueguka kwenda wapi na kutoka wapi?

Safari ni ndefu ila tutafika tu. Kwa njia zote tutafika.

Mmmh diwani wananchi na wapiga kura wako bado hatujajua ni hiki tulicho kutuma ukatuwakilishe? Leo sukari tunanunua sh.2200 kwa kg
 
dar mkuu utauwa inamaana unamjua?

u mean anatudanganya kwa aliyosema! au na wewe unataka U-super star.
 
Brother Msando heshima kwako!

Nimesoma vifungu ulivyovitambua kwamba haviwapi sifa waheshimiwa tajwa ya kuwa madiwani wa halimashauri husika.
Wakati utaratibu wa CCM unajulikana namna wanavyopata wapendekezwa wa viti maalum, upande wa CDM nadhani inabidi ulidadavue zaidi.

Kama nakumbuka uzuri CDM walitengeneza vigezo vyao vya namna ya kupata wapendekezwa wa viti maalum. Labda ungerejea utaratibu mliotumia CDM maana utakuwa na kazi kwanza ya kuonyesha kiushahidi kuwa their nomination did not originate from organs of CDM within the area of jurisdiction of the district council.

Ingawa mimi si mwanasheria naomba kujua yafuatayo:
1. Nomination: kwa nini unataka tuamini kwamba hili neno lina maanisha "Propose a candidate for election" pekee na si "Appoint/Name someone to an office"? CCM utaratibu wao ni wa kura na ushahidi upo kwamba nani alipigiwa kura wapi. CDM hawakuwa na utaratibu wa kura.

2. Originate: Baada ya kupata tafasiri ya hapo juu wasiwasi wangu ni kwamba hao wajumbe wa CDM watakuja na barua CDM wilaya zikiwapendekeza kwa CDM Taifa ili wawe appointed kuwa wabunge wa kuteuliwa. Sasa hapa utakuwa na kazi ya kubishania appointment yao ilivyofanyika.

Unaweza ukapata ushahidi dhahiri kwamba uteuzi wa Chitanda ulitokea Tanga kwa kupigiwa kura, kwa CDM limekaa kimtego zaidi. Na kama nomination ikimaanisha lazima kupigiwa kura basi wabunge wenu (CDM) wote wa kuteuliwa watakuwa feki maana hawakupigiwa kura kwenye halimashauri zao.

Hebu shade some light hapa nahisi watakutoa Knock-out kwenye round ya kwanza.

Realman,

Samahani sana kwa kuchelewa kujibu maswali yako. I was not behind my compute for a while.

Kuhusu maana ya nomination;

"nomination" means nomination as a candidate for election to a local authority;

Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 2 (1) ya Sheria za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 2010, Cap 292.

Kuhusu Chadema na utaratibu uliotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni kweli kwamba utaratibu wa CDM ni tofauti na ulitumika na CCM. CCM Mbunge wao alikuwa nominated by UWT Tanga. UWT ni party organ na ni tawi la Tanga. Kwa hiyo my argument is (which you seem to agree) Mary Chitanda is disqualified from being a member in Arusha.

CDM wabunge wao wameteuliwa na Kamati Kuu ya Taifa. KKT ni party organ ambayo mamlaka yake ni nchi nzima. Kuna pengo katika sheria hapo. Hivyo CDM walichokuwa wansema ni kwamba kutokana na KKT kuwa ni chombo chake chenye mamlaka kitaifa basi wana haki ya kuwapangia wabunge wao popote nchini. Naamini kwamba mwanasheria wa CDM atakayechukuwa jukumu la kutetea ujumbe wa Grace na Lucy ataliona hilo. Lakini, ni suala la mahakama kutoa mkanganyiko huo na Bunge kwenda kupitisha sheria inayoeleweka bila taabu.

Bila kuchukua hatua ninayochukua hilo halitafanyika. I wish all of us could see that way but it remains a wish so I will open the ground on my own. There is only me to loose and i dont feel pity for myself if I loose. At least I have tried to effect change.

I trust I have explained myself to you. If there are still grey areas please shout.
 
Mmmh diwani wananchi na wapiga kura wako bado hatujajua ni hiki tulicho kutuma ukatuwakilishe? Leo sukari tunanunua sh.2200 kwa kg

Dah, Fidel kwani kulikuwa na terms of reference? Na je kwani nashtaki kwa niaba ya wananchi wa Mabogini? Naomba urudie utangulizi wangu.

Kwa ufupi, taaluma yangu ya sheria inanilazimisha kusaidia ukuaji wa sheria pale inapokuwa imedumaa au inapopindishwa. Here is one of the situations.

Na pili, mwenye jukumu la mfumuko wa bei ni Diwani? Hata wewe unaliona hilo na unaweza 'kulisemea' bila hata kuwa na diwani. Afterall, mabango ya Chadema jana mwanzo yalibeba ujumbe huo. Au sukari inauzwa sh. 2200 Mabogini peke yake? Naamini kwamba itakuwa umetoa mfano tu peke yake.

Uvunjaji wa sheria na kudharau sheria tulizojiwekea wenyewe ni tatizo la nchi nzima. Na wanaMabogini ni wananchi so hili pia ni lakwao.

Usijali, kazi inafanyika na hii ni kazi pia.
 
Kama umeelewa nilichomaanisha hiyo tu yatosha.

Wewe ni mnafki.
Unasema wewe ni diwani wa chadema vilevile ni mwanasheria. Sasa hizo tofauti zote ulizoorodhesha hapa hukuziona tangu mwanzo? Ulitoa ushauri gani. Au ulisubiri watu wafe ndio utafute umaarufu. Wewe una umahiri gani katika sheria kumshinda Marando au Tundu lisu.
Kama unataka kuwashtaki nenda kawashtaki, kuna haja gani ya kutupigia makelele hapa?
Umetumwa au unajituma kuleta chokochoko, na lengo lako na huyo aliyekutuma halitatimia.

We are watching you with close eyes as we did to Zitto (Najua Zitto alikuwa rafiki yako pale Daruso, hivyo baada ya mpango wake wa kuvuruga chadema kama alivyotumwa na Rostam kushindikana, ameamua kukutumia wewe. Huna ushawishi huo)

Sasa hizi hasira zote za nini? Chadema inavurugika vipi kwa sheria kutafsiriwa?

Kuhusu Zitto ni kweli alikuwa ni rafiki yangu. Kama unakumbuka vizuri pamoja na urafiki wetu Zitto alidiriki kusimamia kuenguliwa kwangu kama Spika (an attempt which failed) kwa kutumia kanuni za Daruso. Kukumbusha ilikuwa kwamba mtu kuchaguliwa kuwa Spika ni lazima uwe mwakilishi wa darasa au kiongozi wa faculty (Mwenyekiti na Katibu). Nilikuwa Katibu wakati nachaguliwa. uchaguzi wa Spika na Katibu wa faculty of law ulikuwa unafanyika vipindi tofauti. Nilipoacha kugombea faculty of law kama Katibu ina maana nilikosa sifa ya kuwa Spika.

Zitto picked that up and the rest is history. But we still remained friends and we are friends. Kila mtu ana principle zake na hata siku moja siwei kuwa Zitto and Zitto will never be Albert.

Sihitaji kuwa maarufu. Imani kwamba Chadema itavurugwa wewe ndie unayoijenga kwa kutokukubali mawazo tofauti au kusikia ukweli kwa sababu tu unahofia Chadema itaguswa. Hayo ni mawazo yasiyokisaidia chama.

Narudia, Chama kitajengwa kwa nguvu na jasho la kila mmoja wetu. Hatuwezi wote kuwa na uwez sawa wa kufikiria wala hatuwezi kufafanana katika fikra. Hayo unawezakuyapata CCM na zidumu fikra za Mwenyekiti. Kwangu mimi zidumu fikra za Mwenyekiti/Katibu/Wanachama/Mashabiki kama tu nakubaliana nazo na ziko sahihi.

Karibu tena.
 
Msando ana ajira yake tayari ambayo inalipa sana kwa sasa kama waganga wa kienyeji. Hana sababu ya kutishika na CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa sio MAMA YAKE na hasa kama analolisimamia ni HAKI. Endelea Msando.

Aondoke chadema kwanza ili ayafanye hayo akiwa nje ya chadema.
Anachofanya sasa ni unafki mkubwa na kujitafutia umaaruf kwa njia za kijinga.

Niliuliza swali au maswali nadhani yamekuwa magumu kiasi kwamba sijajibiwa hadi sasa:
Maandamano ya Arusha hayakuja ghafla. Kulifanyika maandalizi, na hii ni baada ya mtafaruku wa uchaguzi wa meya Arusha. Yeye Albert akiwa Diwani na mmoja wa viongozi wa chadema na mwanasheria, alitoa ushauri gani? Au alikuwa anasubiri watu wafe ili aje kutafuta umaaruf kwa njia hii anayoitumia sasa.

Nionavyo mimi (msipokubaliana sasa najua mtakuja kukubaliana baada ya matokeo) ni kuwa Albert ana urafiki mkubwa sana na Zito tangu wakiwa UDSM pale daruso, na Zito ndiye aliyekuwa Mentor wa kisiasa wa Albert na alimshawishi aingie chadema na kugombea udiwani. Baada ya mpango wa Zito wa kuibomoa chadema kama alivyoongozwa na Rostam kushindikana sasa ameamua kumu-involve Albert katika hilo, na hiki anachotaka kukifanya Albert ndiyo assignment yake ya kwanza ya "kuibomoa chadema".
Narudia kusema kuwa chadema inawaangalia kwa karibu sana "vijana" hawa wanaoleta chokochoko za makusudi hata kama hazihitajiki.
Mpango wenu haramu hautafanikiwa.

Zito na Albert waliwahi kushawishi mgomo mkubwa sana pale UDSM mwaka 2002/3 kupinga Third Phase Cost Sharing. Walipoona mambo magumu waliingia mitini na kuwaacha wanachuo solemba. Hawa jamaa ni wasaliti na wana uchu wa madaraka na uroho wa utajiri wa haraka haraka. Msiomfahamu huyu jamaa msishabikie tu.
 
"Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno;
nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili."

While am in support of your move you are yet to clear my reservation on the first two (Nominate and Origin).

Nikisoma Dictionary/Wikipedia inasema haya:-

Nominate : Propose (a candidate) for election or Appoint to an office.

Nomination is part of the process of selecting a candidate for either election to an office, or the bestowing of an honor or award.
In the context of elections for public office, a candidate who has been selected by a political party is normally said to be the nominee of that party. The party's selection (that is, the nomination) is typically accomplished either based on one or more primary elections or by means of a political party convention or carcus, according to the rules of the party and any applicable election laws.

Swali: Wabunge wa viti maalumu wanachaguliwa au kuteuliwa??
Swali: Kwa nini unataka tuamini neno nomination stands for "Propose a candidate for election" pekee na sio " Appoint someone to an office"??

Origin.
Its obvious that the law refers to an area of jurisdiction within which a political part exists e.g Moshi, Arusha, Kinondoni etc

Swali: What would happen to a Presidential appointed MP???
Swali: What would happen to a Member of Parliament (special seat) whose party doesn't have organs at District level.

Mpaka usawa huu THANKS naibania. Pamoja!!!!

RM

Umenikera kwa muda mrefu. Inachokusaidia ni ID yako tu.

ALBERTMSANDO LEGAL CONSULTANTS
ADVOCATES & NOTARY PUBLIC
COMMISSIONERS FOR OATHS
Plot No. 39 LDA, Ingira Road, P. O. Box 10620 Arusha.
Mob: +255767 533 433 or +255 785 533 433: E-mail: albert@albertmsandolegal.com

KUMB. NA. AMLC/CHADEMA/ARUSHA/02/2011. 31st January 2011

Mkurugenzi wa Manispaa Arusha,
S. L. P 3013,
Arusha – Tanzania.

Mheshimiwa,

YAH: NOTISI YA SIKU THELATHINI (30) KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA SHERIA CHA 106 CHA SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA MIJI), 1982 KAMA ILIVYOREKEBISHWA KILA MARA.

TAARIFA ZA WAJUMBE WALIOHUDHURIA MKUTANO WA KWANZA WA KAWAIDA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ARUSHA ULIOFANYIKA TAREHE 17.08.2010
Tafadhali rejea yaliyotajwa hapo juu.
Sisi ni washauri wa kisheria wa Madiwani ambao majina na anuani zao yameorodheshwa hapa chini na kwa mantiki hiyo tumeagizwa kukuandikia kama ifuatavyo;
a) Taarifa za Wajumbe waliohudhuria mkutano wa kawaida wa tarehe 17.12.2010.
Mheshimiwa Mkurugenzi, baada ya mkanganyiko uliojitokeza wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri tarehe 17.12.2010 kuhusu uhalali wa Mjumbe Mary Chitanda – Mbunge na vurugu zilizojitokeza kwenye Mkutano huo tumepokea taarifa kwamba mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010. nakala ya barua ya wito na barua ya kuahirisha mkutano huo zimeambatanishwa kama KIELELEZO ARUSHA 1 na 2.
Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa mujibu wa barua yako ya tarehe 15.12.2010 agenda za Mkutano huo zilikuwa;
1. Kufungua Mkutano
2. Uchaguzi wa Mstahiki Meya pamoja na Naibu Meya
3. Uundaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na Bodi
4. Kufunga Mkutano.

Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa mujibu wa barua yako ya tarehe 17.12.2010 Mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010 saa nne asubuhi. Tunapenda kunukuu maneno kutoka kwenye barua hiyo kama ifuatavyo;
"Mkutano utaendelea ili kumalizia agenda zilizosalia katika mkutano wa tarehe 17.12.2010" (msisitizo umeongezwa).
Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa tafsiri rahisi ya maneno hayo ni kwamba Mkutano huo wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Arusha ulianza na kuna agenda ambazo zilijadiliwa tarehe 17.12.2010 na nyingine zikasalia.
Mheshimiwa Mkurugenzi, kutokana na taarifa tulizopewa na wateja wetu Mkutano huo haukuanza wala haukufunguliwa kama ilivyo kawaida ya mikutano. Ili kujiridhisha na hoja hizo za wateja wetu tunaomba ufafanuzi na uthibitisho wako katika haya yafuatayo;
i) Muda halisi ambao Mkutano huo ulifunguliwa/ulianza. Tafadhali tambua na kuzingatia kwamba Mkutano huo unawezekana kuanza baada ya Madiwani kuwa wameapishwa na kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Kanuni. Tafsiri hii inafikiwa kwa kusoma maneno ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Arusha ambayo ni;

Kila Diwani kabla ya kushika wadhifa wake kama Diwani na kabla ya Mkutano wa Kwanza wa Halmashauri;

Hivyo basi ni dhahiri kwamba kiapo cha Madiwani ni LAZIMA kifanyike kabla ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Halmashauri na si wakati wa Mkutano. Mkutano huo hauwezi kufunguliwa au kufanyika kabla ya kiapo cha Madiwani.

ii) Majina na sahihi za Wajumbe wote waliokuwepo wakati Mkutano huo unaanza au baada ya Mkutano huo kuanza ili kuthibitisha akidi halisi ya waliohudhuria Mkutano huo na ushiriki wao. Mheshimiwa Mkurugenzi ni matumaini yetu kwamba taarifa na uthibitisho huu unapatikana kwa kuangalia daftari la mahudhurio ambalo kila Diwani lazima asaini kabla ya kuanza Mkutano.

iii) Agenda ambazo zilijadiliwa siku ya tarehe 17.12.2010 na zile ambazo zilisalia na kujadiliwa siku ya tarehe 18.12.2010 kama ulivyoeleza kwenye barua yako ya taarifa ya Mkutano huo ulioahirishwa.

iv) Majina na sahihi ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano siku ya tarehe 18.12.2010.

Mheshimiwa Mkurugenzi, hoja ya msingi ya wateja wetu ni kwamba maelezo yaliyotolewa kwamba walihudhuria ‘Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha' tarehe 17.12.2010 na kwamba Mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010 ni uongo na yana nia ya kupotosha ukweli kwa makusudi. Naambatanisha nakala ya karatasi ya daftari la mahudhurio inayoonyesha majina ya waliohudhuria ‘mkutano' tarehe 17.012.2010 na tarehe 18.12.2010 na pamoja na sahihi zao. Kama unapingana na nakala hiyo tafadhali tupatie nakala yako halisi ya mahudhurio.
Mheshimiwa Mkurugenzi, ili kutibitisha kwamba Mkutano huo ulifunguliwa na uchaguzi ukafanyika baada ya akidi (quorum) ya 2/3 inayotakiwa kwa mujibu wa Kanunu za Kudumu ni vizuri ukatoa uthibitisho wa majina na sahihi za wajumbe wote waliohudhuria.
b) Mawasiliano na Madiwani
Mheshimiwa Mkurugenzi, tunapenda kukutaarifu kwamba kuanzia tarehe ya barua hii Anuani za Madiwani wote waliohorodheshwa kwenye barua hii ni kama inavyoonekana na si vingenevyo mpaka pale utakapopewa taarifa za mabadiliko ya anuani. Imejitokeza kwamba barua zinapelekwa au zinakabidhiwa watu tofauti na baadaye kusemekana kwamba Diwani amepewa taarifa.

c) Notisi ya siku 30
Mheshimiwa Mkurugenzi, endapo utashindwa kutupatia uthibitisho wa hayo yote yalitajwa kwenye barua hii wateja wetu hawatakuwa na njia tofauti zaidi ya kufungua mashtaka dhidi yako kama Mkurugenzi wa Halmashauri na pia dhidi ya Halmashauri baada ya siku thelathini (30) ili Mahakama kuomba yafuatayo yafanyike;
aa) Manispaa ya Arusha itoe nakala halisi ya mahudhurio ya Wajumbe siku ya tarehe 17.12.2010 na 18.12.2010.
bb) Mahakama iweze kutoa tafsiri na muongozo kuhusu yafuatayo;

i) Ni wakati gani Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha ulifunguliwa/ulianza.

ii) Ni wakati gani idadi ya wajumbe waliofikisha akidi (quorum) ilifikiwa ili Mkutano hu uanze kwa mujibu wa sheria.

iii) Uhalali wa kuendelea na Mkutano bila kuwa akidi inayotakiwa kisheria.

Natanguliza shukrani,

…………………………………….
For: AlbertMsando Legal Consultants

Nakala:
i) Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Dar es Salaam – Tanzania.
ii) Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI,
Dar es Salaam – Tanzania.
iii) Mkuu wa Mkoa,
Arusha - Tanzania.
iv) Mkuu wa Wilaya ya Arusha,
Arusha - Tanzania.
v) Katibu Mkuu – CHADEMA.

RB,

The last one kuhusu Presidential MPs, here is the law;

Section 19 (2) (e)

Any Member of Parliament appointed by the President shall be a member to a Council in which that Member of Parliament ordinarily reside;

Provided that, where Members of Parliament appointed by the President are more than three, the Minister shall by order published in the Gazette direct that the rest of the Members of Parliament in excess of three become members of the neighbouring Council as if they were ordinarily resident in those Cuncils; and.....

Najaribu kutafuta Sheria ya tume ya Uchaguzi to find the definition (if any) kabla sijakujibu.

Ila kuhusu definition ya 'nomination' tafsiri inayotumika ni ya kwenye sheria zetu na sio kwenye dictionary. So tafsiri niliyokupa ni ya kwenye sheria ya Uchaguz i Serikali za Mitaa ya 2010.

i will be getting back you whenever i get an update.

But, I must say I am very please with you contributions which in a way are helping shape the case properly. This is what we need as a country and (as a party).

Thank you very much
 
Umenikera kwa muda mrefu. Inachokusaidia ni ID yako tu.

ALBERTMSANDO LEGAL CONSULTANTS

ADVOCATES & NOTARY PUBLIC
COMMISSIONERS FOR OATHS
Plot No. 39 LDA, Ingira Road, P. O. Box 10620 Arusha.
Mob: +255767 533 433 or +255 785 533 433: E-mail: albert@albertmsandolegal.com

Mawakili huwa hamguswi. Wenzetu nyie mahakamani ndio kazini kwenu. Wacha nijinyamazie au "kuanzia sasa nitakubaliana na kila hoja yako".
 
Zito na Albert waliwahi kushawishi mgomo mkubwa sana pale UDSM mwaka 2002/3 kupinga Third Phase Cost Sharing. Walipoona mambo magumu waliingia mitini na kuwaacha wanachuo solemba. Hawa jamaa ni wasaliti na wana uchu wa madaraka na uroho wa utajiri wa haraka haraka. Msiomfahamu huyu jamaa msishabikie tu.

Kwani ukisema ukweli unapoteza nini. Najaribu kufikiria nguvu unayotumia kupingana na mimi naishia kucheka. Nikusaidie jibu rahisi. Huniwezi hata nikiwa nimelala. Utakachoweza kufanya ni kujiridhisha nafsi yako kwamba nimejibizana na Albert na kwa kiasi fulani utakuwa umegusa joho langu (go back to your bible studies).

Mgomo niliokuwa na Zitto unaozungumzia ulikuwa kuhusu kushinikiza Mkilli Gervas (RIP) na wengine viongozi wa wanafunzi Muhimbili waachiliwe. Mgomo huo ulifanyika na ukafanikiwa 100%. Waliachiwa na mashtaka yalifutwa.

Walikuwa wameengineer huoo mgomo ni:

Omar Ilyas,

Albert Msando.

Imma Mvula

Zitto Kabwe

Julius Rugemalira,

One Mwaikwabe

Na wengine ambao sikumbuki majina.

Sasa historia yako ya UDSM na Daruso sijui unaitoa wapi. Jaribu kuangalia upya na uwe mkweli wa nafsi yako.

Safari inaendelea. Keep an eye on me. But Tanzania will come out of the ditch by the work of CHADEMA. And, be reminded CHADEMA will grow brother, it is growing at a pace you have never witnessed before.
 
Mawakili huwa hamguswi. Wenzetu nyie mahakamani ndio kazini kwenu. Wacha nijinyamazie au "kuanzia sasa nitakubaliana na kila hoja yako".

Hutakiwi kukubaliana na hoja zangu bila sababu ila,

Hutakiwi kunikebehi bila sababu.

Hutakiwi kunisingizia jambo bila sababu.

Hatutakiwi kutukanana hata mara moja. Tujibizane kwa hoja.

Toa hoja kwa nini si sahihi kushitaki wabunge wa CDM.

Toa hoja kwa nini suala la tafsiri ya sheria kuhus Viti Maalumu lisiende mahakamani.

Ni jambo jepesi na lenye raha likijadiliwa bila hasira wala kukurupuka.

Mimi nitaendelea kuwa Chadema leo kesho na siku zote. Sina sababu ya kuwa mtumwa au mamluki. Kwa kipi ambacho nitafaidika nacho? utu wangu ni muhimu zaidi na naamini ninao uwezo wa kutosha kuweka mkate na ugali maharage kwenye sahani watoto wangu wakala wakashiba. Na uwezo huo nitautumia kuwasaidia watanzania wengine waweze pia.

Ahsante.
 
Umenikera kwa muda mrefu. Inachokusaidia ni ID yako tu.

ALBERTMSANDO LEGAL CONSULTANTS
ADVOCATES & NOTARY PUBLIC
COMMISSIONERS FOR OATHS
Plot No. 39 LDA, Ingira Road, P. O. Box 10620 Arusha.
Mob: +255767 533 433 or +255 785 533 433: E-mail: albert@albertmsandolegal.com

KUMB. NA. AMLC/CHADEMA/ARUSHA/02/2011. 31st January 2011

Mkurugenzi wa Manispaa Arusha,
S. L. P 3013,
Arusha – Tanzania.

Mheshimiwa,

YAH: NOTISI YA SIKU THELATHINI (30) KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA SHERIA CHA 106 CHA SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA MIJI), 1982 KAMA ILIVYOREKEBISHWA KILA MARA.

TAARIFA ZA WAJUMBE WALIOHUDHURIA MKUTANO WA KWANZA WA KAWAIDA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ARUSHA ULIOFANYIKA TAREHE 17.08.2010
Tafadhali rejea yaliyotajwa hapo juu.
Sisi ni washauri wa kisheria wa Madiwani ambao majina na anuani zao yameorodheshwa hapa chini na kwa mantiki hiyo tumeagizwa kukuandikia kama ifuatavyo;
a) Taarifa za Wajumbe waliohudhuria mkutano wa kawaida wa tarehe 17.12.2010.
Mheshimiwa Mkurugenzi, baada ya mkanganyiko uliojitokeza wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri tarehe 17.12.2010 kuhusu uhalali wa Mjumbe Mary Chitanda – Mbunge na vurugu zilizojitokeza kwenye Mkutano huo tumepokea taarifa kwamba mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010. nakala ya barua ya wito na barua ya kuahirisha mkutano huo zimeambatanishwa kama KIELELEZO ARUSHA 1 na 2.
Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa mujibu wa barua yako ya tarehe 15.12.2010 agenda za Mkutano huo zilikuwa;
1. Kufungua Mkutano
2. Uchaguzi wa Mstahiki Meya pamoja na Naibu Meya
3. Uundaji wa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na Bodi
4. Kufunga Mkutano.

Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa mujibu wa barua yako ya tarehe 17.12.2010 Mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010 saa nne asubuhi. Tunapenda kunukuu maneno kutoka kwenye barua hiyo kama ifuatavyo;
"Mkutano utaendelea ili kumalizia agenda zilizosalia katika mkutano wa tarehe 17.12.2010" (msisitizo umeongezwa).
Mheshimiwa Mkurugenzi, kwa tafsiri rahisi ya maneno hayo ni kwamba Mkutano huo wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Arusha ulianza na kuna agenda ambazo zilijadiliwa tarehe 17.12.2010 na nyingine zikasalia.
Mheshimiwa Mkurugenzi, kutokana na taarifa tulizopewa na wateja wetu Mkutano huo haukuanza wala haukufunguliwa kama ilivyo kawaida ya mikutano. Ili kujiridhisha na hoja hizo za wateja wetu tunaomba ufafanuzi na uthibitisho wako katika haya yafuatayo;
i) Muda halisi ambao Mkutano huo ulifunguliwa/ulianza. Tafadhali tambua na kuzingatia kwamba Mkutano huo unawezekana kuanza baada ya Madiwani kuwa wameapishwa na kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Kanuni. Tafsiri hii inafikiwa kwa kusoma maneno ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Arusha ambayo ni;

Kila Diwani kabla ya kushika wadhifa wake kama Diwani na kabla ya Mkutano wa Kwanza wa Halmashauri;

Hivyo basi ni dhahiri kwamba kiapo cha Madiwani ni LAZIMA kifanyike kabla ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Halmashauri na si wakati wa Mkutano. Mkutano huo hauwezi kufunguliwa au kufanyika kabla ya kiapo cha Madiwani.

ii) Majina na sahihi za Wajumbe wote waliokuwepo wakati Mkutano huo unaanza au baada ya Mkutano huo kuanza ili kuthibitisha akidi halisi ya waliohudhuria Mkutano huo na ushiriki wao. Mheshimiwa Mkurugenzi ni matumaini yetu kwamba taarifa na uthibitisho huu unapatikana kwa kuangalia daftari la mahudhurio ambalo kila Diwani lazima asaini kabla ya kuanza Mkutano.

iii) Agenda ambazo zilijadiliwa siku ya tarehe 17.12.2010 na zile ambazo zilisalia na kujadiliwa siku ya tarehe 18.12.2010 kama ulivyoeleza kwenye barua yako ya taarifa ya Mkutano huo ulioahirishwa.

iv) Majina na sahihi ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano siku ya tarehe 18.12.2010.

Mheshimiwa Mkurugenzi, hoja ya msingi ya wateja wetu ni kwamba maelezo yaliyotolewa kwamba walihudhuria ‘Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha' tarehe 17.12.2010 na kwamba Mkutano huo uliahirishwa mpaka tarehe 18.12.2010 ni uongo na yana nia ya kupotosha ukweli kwa makusudi. Naambatanisha nakala ya karatasi ya daftari la mahudhurio inayoonyesha majina ya waliohudhuria ‘mkutano' tarehe 17.012.2010 na tarehe 18.12.2010 na pamoja na sahihi zao. Kama unapingana na nakala hiyo tafadhali tupatie nakala yako halisi ya mahudhurio.
Mheshimiwa Mkurugenzi, ili kutibitisha kwamba Mkutano huo ulifunguliwa na uchaguzi ukafanyika baada ya akidi (quorum) ya 2/3 inayotakiwa kwa mujibu wa Kanunu za Kudumu ni vizuri ukatoa uthibitisho wa majina na sahihi za wajumbe wote waliohudhuria.
b) Mawasiliano na Madiwani
Mheshimiwa Mkurugenzi, tunapenda kukutaarifu kwamba kuanzia tarehe ya barua hii Anuani za Madiwani wote waliohorodheshwa kwenye barua hii ni kama inavyoonekana na si vingenevyo mpaka pale utakapopewa taarifa za mabadiliko ya anuani. Imejitokeza kwamba barua zinapelekwa au zinakabidhiwa watu tofauti na baadaye kusemekana kwamba Diwani amepewa taarifa.

c) Notisi ya siku 30
Mheshimiwa Mkurugenzi, endapo utashindwa kutupatia uthibitisho wa hayo yote yalitajwa kwenye barua hii wateja wetu hawatakuwa na njia tofauti zaidi ya kufungua mashtaka dhidi yako kama Mkurugenzi wa Halmashauri na pia dhidi ya Halmashauri baada ya siku thelathini (30) ili Mahakama kuomba yafuatayo yafanyike;
aa) Manispaa ya Arusha itoe nakala halisi ya mahudhurio ya Wajumbe siku ya tarehe 17.12.2010 na 18.12.2010.
bb) Mahakama iweze kutoa tafsiri na muongozo kuhusu yafuatayo;

i) Ni wakati gani Mkutano wa Kwanza wa Kawaida wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha ulifunguliwa/ulianza.

ii) Ni wakati gani idadi ya wajumbe waliofikisha akidi (quorum) ilifikiwa ili Mkutano hu uanze kwa mujibu wa sheria.

iii) Uhalali wa kuendelea na Mkutano bila kuwa akidi inayotakiwa kisheria.

Natanguliza shukrani,

…………………………………….
For: AlbertMsando Legal Consultants

Nakala:
i) Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Dar es Salaam – Tanzania.
ii) Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI,
Dar es Salaam – Tanzania.
iii) Mkuu wa Mkoa,
Arusha - Tanzania.
iv) Mkuu wa Wilaya ya Arusha,
Arusha - Tanzania.
v) Katibu Mkuu – CHADEMA.
Dar es Salaam – Tanzania.

Msando,
Usikasirike sana hadi ukaipoteza thread hii. Mimi nakuona jasiri sana. Umejisajili humu kwa jina lako halisi. Na hoja yako hii inagusa moja kwa moja maslahi ya watu. Watakuyumbisha kwa namna mbalimbali. Simamia kwenye hoja yako. Hizo siasa za vyuoni waachie wao waendelee nazo. Unalotaka kulifanya halijafanywa na wanasheria wengi nchi hii.
Watu hawajui kwamba kinachotutesa nchi hii ni utekelezaji, usimamizi na tafsiri mbovu za vifungu vya KATIBA na sheria zetu.
 
Mawakili huwa hamguswi. Wenzetu nyie mahakamani ndio kazini kwenu. Wacha nijinyamazie au "kuanzia sasa nitakubaliana na kila hoja yako".

Unaingiza siasa za vyuoni kwenye thread hii bila sababu. Ijadili hoja yake au uisome kwa wengine.
 
Hutakiwi kukubaliana na hoja zangu bila sababu ila,

Hutakiwi kunikebehi bila sababu.

Hutakiwi kunisingizia jambo bila sababu.

Hatutakiwi kutukanana hata mara moja. Tujibizane kwa hoja.

Toa hoja kwa nini si sahihi kushitaki wabunge wa CDM.

Toa hoja kwa nini suala la tafsiri ya sheria kuhus Viti Maalumu lisiende mahakamani.

Ni jambo jepesi na lenye raha likijadiliwa bila hasira wala kukurupuka.

Mimi nitaendelea kuwa Chadema leo kesho na siku zote. Sina sababu ya kuwa mtumwa au mamluki. Kwa kipi ambacho nitafaidika nacho? utu wangu ni muhimu zaidi na naamini ninao uwezo wa kutosha kuweka mkate na ugali maharage kwenye sahani watoto wangu wakala wakashiba. Na uwezo huo nitautumia kuwasaidia watanzania wengine waweze pia.

Ahsante.

Nani kakutukana?

Kama baba yako kakukosea wewe mwanawe, unachotakiwa ni kumaliza tofauti zako na yeye na sio kwenda kumshitaki. Hujafanya jitihada zozote za kuhakikisha suala hilo linamalizika au walau linapatiwa ufumbuzi katika majukwaa ya ndani ya chama.
Je ulifanya hivyo ikashindikana? Ninachokiona hapa ni kama vile unataka kutuaminisha kuwa ulifanya jitihada hizo zikagonga mwamba, kitu ambacho sijajiridhisha (baada ya kusoma hii thread) kuwa umekifanya.
Ashakum si matusi: Mkeo akikunyima unyumba utakwenda kumshitaki mahakamani?
 
Unaingiza siasa za vyuoni kwenye thread hii bila sababu. Ijadili hoja yake au uisome kwa wengine.

Mkuu sijaingiza siasa za vyuoni kama unavyodai. Nimejadili hoja yake kwa namna ambavyo mimi ninaona. Tatizo lenu kuna kundi fulani humu jamvini halitaki likosolewe. Na kwamba hoja ikitolewa na mmoja wa watu wa kundi hilo basi sisi wengine wote tuisifie na kuimwagia thanks. Tukiijadili kwa maono kinzani kinyume na vile mnavyotaka basi matatizo. Kama hivyo ndivyo basi waambieni mods wawaondoe wale wote wenye mtazamo tofauti na ninyi.
 
Hili wala sio la vikao vya Chama chochote kile. Sheria ikpindishwa au kupewa tafsiri mbovu itanyooshwa MAHAKAMANI tu. Ndio maana mimi sikuwaunga mkono CHADEMA na maandamano yao ya ARUSHA juu ya uchaguzi wa Meya. Bora wangeandamana kwa uchaguzi wa Rais.
 
Mkuu nadhani imeelezwa mara kadhaa ndani ya thread hii kwa nini option ya maandamano ilionekana kushinda hiyo ya mahakamani. Ni kuwa hukumu ya kesi ingetolewa miaka kadhaa baadae na hivyo kupoteza ule uhai wa suala lenyewe. Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la ubungo ya Mh. Mnyika dhidi ya Keenja na. 1 ya mwaka 2006 hukumu yake ilitolewa lini? Huo ni mfano mdogo tu lakini zipo mamia kwa mamia ya kesi za namna hiyo. Nina uhakika unalifahamu hilo.
 
Mimi hii nimeipenda. Ikifanyikiwa itakuwa fundisho kwa wote wanaopenda kupinda sheria ili iwafae kwa wakati fulani wakibank kwamba watu wengi ni mbumbu wa sheria. kila la heri msandoAlberto
 
Back
Top Bottom