Nawaageni nakwenda mwezini

We ni Mhaya wa wapi?
space-shuttle-atlantis-sts-27-in-1972-xl.jpg




Waswahili husema mtu ajuwa atokako hajuwi endako.Mwenzenu nina safari ya kwenda mwezini.Uzuri wa safari ni kuaga,na wa mwanzo kuagwa ni nyumbani kwako.Kwa maana hiyo ndio maana nimeamua nianze kuwaageni nyinyi hapa nyumbani.
Baadae nitasafiri kupitia nchi kadhaa za ulaya kuaga ndugu na marafiki.Nitakaa zaidi nchini Uiengereza.Halafu nitaelekea America kwa madhumuni hayo hayo.Huko nitakuwa na shughuli maalum ya maandalizi ya safari kabla kwenda Urusi eneo la Kazakhstan ambako nitakaa kwa muda mfupi.Nikitoka huko nitakuwepo nchi za Ghuba kwa muda kiasi kabla kurudi nyumbani tayari kwa safari.
Nawaombeni ushauri ili kufanikisha safari hii.Nini nichukue na nini niwache.Namna gani nitaweza kushinda upweke kwenye chombo cha usafiri na huko niendako.
 
Ami unavyoongea inaonyesha kabisa wewe mzoefu wa kwenda huko 'mwezini'. Kwani siku za nyumba ulikuwa unaandaa nini kwa safari yako? Sisi hatuna uzoefu wa kwenda huko, na hatujui tukuandalie mikate, mihogo ya kuchoma au chapati za kusukuma!
 
Mimi nimefuzu u pilot wa hizo roketi. Naomba niwe rubani, japo msaidizi katika safari yako
Nimekuja likizo kidogo.Wajua na mambo ya uchaguzi mkuu tena.Halafu kule space station nilikokuwa muda wote huo mambo si mazuri.Mfumo wa kupoza (cooling system) umefeli.Nimeacha wenzangu wanajaribu kurekebisha kwa kutoka na kutembea nje ya chombo.
Mbona sijakuta vyeti vyako?.Nilitaka niwasilishe ofisini kwetu ufanyiwe majaribio kupima ubora ya cheti chako.Nilikuahidi nitakufahamisha maeneo ambayo nitahitaji msaada wako,ngoja nikukumbushe baadhi ya kozi zetu za urubani wa roketi nataraji bado hujasahau ile kozi ya ya Emergency exits.
Bila shaka katika kozi hii unakumbuka kosa lilopelekea kuungua mpaka majivu wanaanga wenzetu watatu tarehe 27 Januari 1967 pale viwanja vya mambo ya anga vya cape Kennedy.Ilikuwa ni katika jaribio la hatua za mwisho ili Apollo 1 iweze kuruka kwenda mwezini siku za karibu.Chombo ilikuwa kimekuwa fully pressurized na Oxygen (100percent).Grissom,Ed White na Roger Chaffee wakapanda jukwaa na wakaingia ndani juu ya roketi ya Saturn 1.
Muda si muda vijana wakaanza kusikia harufu isiyokawaida ndani ya chombo,mafundi wakafika lakini harufu ikapotea.Saa 1 harufu ikarejea.Rubani mkuu Grissom nafasi kama ya kwangu akalalamikia mawasiliano hafifu na chumba cha kuongozea,akasema "Ikiwa siwezi kuongea nanyi maili chache tu,itakuwaje tutakapofika mwezini?".Baada ya majaribio machache muda wa mwisho kuwashwa ukakakaribio na hesabu ya dakika 10 za mwisho ikaanza.
Dakika ya mwisho vipimo vikaonesha kuongezeka kiwango cha oxygen ndani ya mitambo yote,hatimaye ikasikika nyendo zisizo za kawaida za wanaanga wale,ikafuatiwa na chafya na sauti za kukwama halafu mmoja wao yawezekana Grissom akasema "Kuna moto ndani ya chombo!".Grissom ilikuwa avute kagia fulani pale kushotoni pake ili kutoa hatch na cabin yao ijitenge na sehemu za chini zenye mitambo zaidi. pressure.Hilo ilikuwa haliwezekani bila msaidizi wake (co pilot) kupunguza pressure kwanza kwa kubonyeza katufe fulani.Sijui ilikuwa tatizo ni nini Ed White hakufanya hivyo mapema.
Baada ya hapo ikawa wazi kwao kwamba moto uliokwishaanza utawaunguza wakasikika wakisema " a bad fire .....we are burning up".Katika muda mfupi uliofuata moto ukaripuka kote na kuwaangamiza wote na chombo kuporomoka na mnara wake.Ilikuwa ni majonzi makubwa kwa nchi nzima kwani runinga ilikuwa ikionesha moja kwa moja.Jumla ya wataalamu 1500 waliunda tume mbali mbali kuchunguza tukio hili ambao ilikuwa watafute tatizo siyo kuficha ukweli na kulindana.

Katika somo hili utakumbuka habari za mwanaanga wa kirussia Col.Vladmir Komarov aliyeondoka peke yake miezi mitatu baada ya ajali ya moto mnamo tarehe 23 April 1967 na Soyuz 1.Hata mke wake hakumuaga,alipata taarifa kupitia vyomba vya habari akiwa tayari yuko orbit ya 3 dakika 25 tangu aruke pale alipotoa salamu kwa wanachi wa Urusi na kuwapongeza watu wa Vietnam aliosema ni mashujaa waliokuwa wakipambana na mvamizi jambazi Amerika.
Lakini baada ya masaa 27 angani matangazo yalisitishwa,lilipotolewa tangazo lilisema Komarov alifariki wakati akiwa safarini kurudi pale chombo kilipooneka kikishuka kwa kuyumbayumba.Inawezekana uchofu kwa kuwa bila co pilot kulimfanya asiweze kushughulikia baadhi ya vijambo kati ya utitiri wa mambo ya roketi,wewe itakuwa unajuwa kwa vile umepitia hii shughuli.Huyu ni mwanaanga wa mwanzo kufa akiwa angani.

Hivyo na mimi nahitaji msaada wako lakini kwanza lazima nijulishwe uwezo wako wa kuwa msaidizi wangu katika anga.
 
Safari njema ila kama kuna kitimoto inapatikana huko nifungie kiduchu!!Nasikia kunaviumbe hai wanapatikana huko na waendao huko hupiga menu kwakujificha!! makobe wa mwezini!!..lol:becky:
 
Back
Top Bottom