Nawaageni nakwenda mwezini

Picha yenyewe ndiyo hii

moon_r3.gif
Hapo ni asubuhi mapema mwezini.Dunia inachomoza kwa karibu na mwangaza wake kumwilika juu ya ardhi ya mwezi.
Ni kimya sana.Huwezi kusikia sauti ya kiumbe chochote.Hata sauti za UFO kama wapo upande wa pili wa mwezi huwezi kuwasikia.Tofauti na duniani nyota huwa zinaonekana kwa uwazi na mn'garo mkubwa.
Ni pahala pazuri sana kwa wale waliochoka na dunia.
 
chukua na ka laptop ukaitangaze JF mwezini.
Hata mimi ningependa kufanya hivyo na hii ingekuwa ni sehemu muhimu ya kunipunguzia upweke huko mwezini,hata hivyo ndugu Klorokwin nakuarifu kwamba hilo kwa sasa haliwezekani huko mwezini.
Kwa kweli huu utafiti wa jinsi ya kuanzisha internet huko mwezini ni moja ya majukumu yanayonipeleka huko.Kwa kuanzia hatukusudii kutengeneza mtandao wa internet wa kukuwezesha wewe kufanya majadiliano na wana JF au kuangalia U-tube,bali wa kutuwezesha kuendeleza utafiti wa kujua hii core(kiini) cha mwezi kimetenngenezeka na nini?.Jee ni ujiuji wa madini kama wa dunia au ni kitu kigumu.
Ili uweze kujua hivyo ni lazima ufanye miripuko ya kiseismoloji ambayo hutembea mpaka katikati ya mwezi au dunia kwa hapa duniani na hatimae kurudi yalipoanzia.Kwa kupima mwendo wa mawimbi (seismology) ndipo tunaweza kujuwa iwapo kiini cha mwezi ni kitu gani.
Kazi hiyo ni lazima ifanyike kwa eneo kubwa na kuunganishwa na vituo vitakavoweza kuwasiliana ili kutuma data.Huwezi kuwa na vituo vingi vitakavyoweza kuwasiliana bila kuwa na mawasiliano kama ya internet wakati ambapo huwezi kuwa na watu idadi hiyo huko mwezini ili kuchukua hizo takwimu (data).
Kwa maelezo hayo ndugu yangu Kloro. itakuwa umeelewa kwa nini laptop itakuwa ni mzigo wa bure kwenda nayo mwezini na umeelewa moja ya kazi ninayokwenda kuifanya huko.
 
Usisahau kubeba maji ya kunywa yanaweza kukusaidia maana nasikia kuna joto sana huko.
 
Usisahau kubeba maji ya kunywa yanaweza kukusaidia maana nasikia kuna joto sana huko.
Hapana!,Fisherscom umeelewa vibaya au uliyemsikia hafahamu.
Mwezini maji yapo kama ambavyo tumegundua hivi karibuni October 9,2009.Tumeyapata katika mji wa mapango wa Cabeus huko kusini ya mwezi.Tatizo ni kuyafikia kwani yapo katika hali ya barafu na chini sana ardhi ya mwezi.Pamoja na hivyo nathamini ushauri wako kwani juhudi za kuyachimba maji hayo hazijakamilika.
Kuhusu joto inategemea umesimama wapi.Kwani nyakati za mchana mwezini joto hupanda mpaka 101°C (214°F) kiasi kinachoweza kuchemsha na kuyakausha maji.Lakini usiku hali ya joto hushuka mpaka -184°C (-300°F).Hii ni baridi kali sana ambayo haivumiliki na binadamu.
Kumbuka kwamba usiku mmoja au mchana mmoja ni sawa na siku 14 za hapa duniani.Sisi mara nyingi kule mwezini huwa tunajaribu kufika asubuhi mapema ili tuwahi kuondoka kabla magharibi haijaingia kuepuka hali mbaya ya hewa ya usiku na kwa ajili ya kufanyakazi vizuri kwa vyombo vyetu.
Hata hivyo huwa tunavaa nguo maalum ambazo zinahimili mabadiliko ya hali ya joto ambayo hutokea papo kwa papo baina ya usiku na kuingia mchana.Nguo zetu tunazoziita spacesuits huwa zsinakuwa na aina maalum ya manyamunyamu(fabrics) ambayo huzuia mabadiliko hayo ya joto kufikia miili yetu.Kwa juu hizi nguo zina gamba la kurudisha miale (reflect) ili isipenye ndani.Pia kwa dharura ikitokea hizi nguo zina pump za kutoa nje maji maji yanayoweza kufanyika ndani pia kifaa cha kutoa joto la ziada.
Huyo hapo chini ni mimi nikiwa katika space suit.
 
unaomba ushauri kwa watu ambao hawana ujuzi na mambo hayo? si ukaombe NASA na huko Urusi? ndio maana unapew majibu yasiyo na shepu. ila safari njema
 
Mimi nimefuzu u pilot wa hizo roketi. Naomba niwe rubani, japo msaidizi katika safari yako
 
Mimi nimefuzu u pilot wa hizo roketi. Naomba niwe rubani, japo msaidizi katika safari yako
Nimefurahi sana kupata kijana kama wewe ambaye atakuwa tayari kufuatana nami mwezini.Lakini kweli cheti chako ni cha kurusha roketi!.Nina shaka kuwa huwa unarusha ndege ndogo ndogo tu za watalii.Nitayarishie photocopy zako na weka vizuri rekodi zako za urubani ili niwasilishe kwa wakuu wetu uangaliwe idadi ya masaa ambayo umeruka angani.
Ningependa nipate na mpiga picha mmoja kutoka jukwaa na photograph humu,lakini nadhani wengi kule ni vilaza hawawezi kuandamana nasi.Watajisikia kufa kufa kama dada Firstlady wakivaa spacesuit.Wewe na mimi hata spacesuit ikikomewa na funguo kuachwa duniani hatujali.
Nimetingwa na shughuli kidogo nikirudi nitawasiliana nawe zaidi nikuoneshe maeneo ambayo nitahitaji co-piloting katika msafara huu.
 
Naomba ikiwa wewe hujaolewa tuende pamoja.Utakuwa mke wangu wa 3.Wake zangu wawili hawaiwezi safari kama hii.Mmoja ni mgonjwa wa presha na mwengine hajafaulu mazoezi magumu ya kuingia katika safari kama hii.Ikiwa utakuwa tayari niambie.

mhh hapa nilipo nijkianza zile safari za mwezi za kina mama tu hapatoshi,sasa nikiufuata huko huko si ndio balaa??NO THANKYOU!
 
sAFARI NJEMA ILA UJUE INAEMEKANA HAKUNA KIUMBE ALIYEWAHI KUFIKA MWEZINI
GONGA HAPA NA HAPA PIA hAPA

UNAKWENDA NA CHOMBO GANI HUKO IKIWA WANAODAI KUWA WALIKWENDA HUKO MWAKA 1969, LEO WANADAI HAWANA TEKNOLOJIA YA KUWAPELEKA HUKO? KWA TAARIFA gonga HAPA and here
 
sAFARI NJEMA ILA UJUE INAEMEKANA HAKUNA KIUMBE ALIYEWAHI KUFIKA MWEZINI
GONGA HAPA NA HAPA PIA hAPA

UNAKWENDA NA CHOMBO GANI HUKO IKIWA WANAODAI KUWA WALIKWENDA HUKO MWAKA 1969, LEO WANADAI HAWANA TEKNOLOJIA YA KUWAPELEKA HUKO? KWA TAARIFA gonga HAPA and here

Lumbe nakushukuru kwa mapenzi yako kwangu.Umeeona mbali.Hawa jamaa huenda wamekusudia wakanitoe kafara huko mwezini,ndio maana nimepangiwa niwe wa mwanzo kushuka.
Lakini sikio la kufa halisikii dawa.Mimi safari ya mwezini bado ninaayoo!!.Nataka niwe wa mwanzo kufa huko.Isipokuwa sasa nitakuwa na tahadhari na hawa jamaa.Kwanza nitabaki kwenye space station kwa muda kuuchungulia mwezi.
Pale space station (ISI) si neno kwa sababu mara nyingi huwa tunakwenda.Sasa hivi wenzangu sita wako huko.Juzi rafiki yangu alikuwa anakwenda kuwapelekea matunda na maji,almanusra asababishe ajali kama ile ya Bp kule Lousiana.BBC News - Russian cargo ship 'under control' official says
Ngoja nikuhadithie maisha yetu kule ISI:Moja ya matatizo tunayokumbana nayo ni kula,tunayo dining room lakini ni kama ada tu kwani sahani na vikombe wala havikai juu ya meza,huwa vinaelea.Kutokana na weightlessnes chakula kama uji ukiumimina ili uutie mdomoni unaruka na kuenea mpaka kwenye dari.Tuna sehemu maalum ya kulala lakini ni kwa ajili ya kukaa pembeni tu inapokuwa huko kwenye zamu kwa sababu hakuna usiku.
Kwa vile space station imo kuizunguka dunia muda wote basi jua huchomoza kila baada ya dakika 90.Ndio maana tukilala tunakaa mbali na dirisha ili mwangaza wa jua usitukere.Kitanda kimoja tunaweza kulala wawili,mmoja juu na mwengine kwa chini uvunguni na wala hadondoki sakafuni.
Angalia huyu dada ambaye huja kutuamsha kila mara tukibadilishana zamu.
YouTube - Kawabata Makoto: Morning On The Moon
 
Back
Top Bottom