Nawaageni nakwenda mwezini

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,151
10,860
space-shuttle-atlantis-sts-27-in-1972-xl.jpg




Waswahili husema mtu ajuwa atokako hajuwi endako.Mwenzenu nina safari ya kwenda mwezini.Uzuri wa safari ni kuaga,na wa mwanzo kuagwa ni nyumbani kwako.Kwa maana hiyo ndio maana nimeamua nianze kuwaageni nyinyi hapa nyumbani.
Baadae nitasafiri kupitia nchi kadhaa za ulaya kuaga ndugu na marafiki.Nitakaa zaidi nchini Uiengereza.Halafu nitaelekea America kwa madhumuni hayo hayo.Huko nitakuwa na shughuli maalum ya maandalizi ya safari kabla kwenda Urusi eneo la Kazakhstan ambako nitakaa kwa muda mfupi.Nikitoka huko nitakuwepo nchi za Ghuba kwa muda kiasi kabla kurudi nyumbani tayari kwa safari.
Nawaombeni ushauri ili kufanikisha safari hii.Nini nichukue na nini niwache.Namna gani nitaweza kushinda upweke kwenye chombo cha usafiri na huko niendako.
 
...Namna gani nitaweza kushinda upweke kwenye chombo cha usafiri na huko niendako.

Kwa nini uwe mpweke, kwani Mama Salma, na Membe, na wapiga picha na wasemaji wako hawatakusindikiza kama kawaida?
 
mhhhhhhh makubwa haya...waenda for good au unarudi????nakushauri usirudi kabisa,oa huko huko na kuendesha maisha yako...huku bongo kumeoza siku hizi!!!!!

good luck!
 
Kweli pombe si nzuri. Mi nilifikiri unatuaga kuelekea kwenye mwezi ule wa kina mama LOL!
 
Aaah! M'bora ni wewe uagaye kila unapoanza safari,

Na si safari tu ya kikawaida bali ni safari ya maili kilomita nyingi hali ukiwa angani/hewani.

Japo i' safari kama zilivyo nyingine lakini hii yako ni ya kihistoria na kumbukumbu tosha kwa wale tusotarajia/tuso na uwezo wa kufika mwezini, hongeraa.

Hali kadhalika safari za maeneo kama hayo ni za hatari na huhitaji uvumilivu mkubwa na hasa ukichukulia dunia ni pana na huko mwezini utakutana na watu wa haiba tofauti, nakushauri uvumilie bughdha au kauli zao mbovu na uzipuuze.

Mie nilipoiona hii taarifa nilishangaa kidogo lakini nkajisemea mwenyewe '' aah! nashangaa nini au kwakuwa mie sifikirii ipo siku ntaenda mwezini'' Lakini baadaye nilipoisoma vizuri,

Nikagundua mtoaji taarifa hii ni msafiri mzuri na huko mwezini ni kama nyumbani na haupiti mwezi ukaacha kudhuru.

Ndugu, mie sina matata pia jamaa hapa wamenihakikishia kuwa una baraka zote.

Ukifika huko usisite kutujulisha na vivyo hivyo ukirudi.

''SAFIRI KWA AMANI''
 
mhhhhhhh makubwa haya...waenda for good au unarudi????nakushauri usirudi kabisa,oa huko huko na kuendesha maisha yako...huku bongo kumeoza siku hizi!!!!!

good luck!
Naomba ikiwa wewe hujaolewa tuende pamoja.Utakuwa mke wangu wa 3.Wake zangu wawili hawaiwezi safari kama hii.Mmoja ni mgonjwa wa presha na mwengine hajafaulu mazoezi magumu ya kuingia katika safari kama hii.Ikiwa utakuwa tayari niambie.
 
Bado sijapata ushauri wa kitaalamu kuhusu safari yangu hii.Jee niende moja kwa moja kwa kutumia teknolojia ya kizamani au nisimame kwenye space station kwanza?.
 
mhhhhhhh makubwa haya...waenda for good au unarudi????nakushauri usirudi kabisa,oa huko huko na kuendesha maisha yako...huku bongo kumeoza siku hizi!!!!!

good luck!


mmh mi hiyo avatar yako tu .... hakyanani Embe linatamanisha hilo....duh........ i am serious
 
Msafiri Kafiri!...Nenda bila mzigo wowote, utakula utakachokikuta mbele ya safari!...Jifunge mkanda kiunoni, chukua fimbo yako, anzisha mwendo!
 
Msafiri Kafiri!...Nenda bila mzigo wowote, utakula utakachokikuta mbele ya safari!...Jifunge mkanda kiunoni, chukua fimbo yako, anzisha mwendo!
Nashukuru kwa ushauri wako lakini nahisi haujatosha kwa safari kama hii.Hapo zaidi nakubaliana na wewe kuhusu kufunga mkanda kiunoni,lakini kuhusu kula nitakachokikuta huko mwezini,nahisi hunitakii mema.
 
Mimi nataka Ukienda huko Mwezini nakuomba uje na Mtoto wa Ufo uniletee zawadi. Nitashukuru sana kwa sababu nina hamu niwe naye huyo Ufo nipate kumfuga nyumbani kwangu. hebu angalia picha yake hiyo

ufo 14.jpg
 
Mimi nataka Ukienda huko Mwezini nakuomba uje na Mtoto wa Ufo uniletee zawadi. Nitashukuru sana kwa sababu nina hamu niwe naye huyo Ufo nipate kumfuga nyumbani kwangu. hebu angalia picha yake hiyo

View attachment 11329
Sisi kule tunatua upande unaoelekeana na dunia.Yapo maeneo mengi yanaofikika lakini mimi nitatua pale pale Sea of Tranquility alipofikia babu yangu.Hawa viumbe sina uhakika wanakaa wapi lakini nataraji sana wako upande wa pili wa mwezi ambao kutokea duniania daima hauonekani.Sisi huwa tunauona wakati tukikaribia kufika kwani huwa tunazunguka zunguka kabla kutua maeneo yetu.
Upande huo wa pili mbali na giza kuna mapango na mabonde marefu sana,kwa hapa kwetu fikiria mabonde yaliyopo Lushoto kabla hujafika Soni na zaidi ukipandishia Vuga.Huku yawezekana ndiko wanakozaliana.Ningekwambia nikipata rover nitakwenda kufukuzana nao au kuwatega lakini kwa rover si rahisi,ni lazima nituwe kule na ni hatari sana.Maeneo ya kutuwa yapo machache kama vile Mare Moscoviense,,Mare Ingenii na Mare Orientale.Lakini kwa vile shughuli zangu nyingi zitakuwa huku upande wa dunia, kwa hivyo sitojaribu kwenda huko mara hii kukutafutia zawadi yako.
Pamoja na hivyo,mbona umechaguwa zawadi ya hatari.Unayo habari kuwa hawa viumbe hawafugiki kama ambavyo labda umekusudia na hawatabiriki.Nchini Venezuela vitoto vya UFO vilidondoka juu ya nyumba ya familia moja,baada ya muda watu wote walikufa.Inasemekana hivi vitoto viliacha mionzi mikali.Mwaka 2005 UFO walipita juu ya ikulu ya Amerika-white house ikabidi watu wote wajifiche kwenye mahandaki.Tarehe 5/06/2010 kwa mara ya mwisho UFO wameonekana Australia.Soma mwenyewe vituko vyao uone na kama bado ndiyo zawadi uipendayo.List of UFO sightings - Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa ninavyowajuwa vurugu zao nakushauri uchaguwe zawadi nyengine.Kwa leo nakupa zawadi ya picha aliyoniletea babu yangu Neil Armstrong,mwaka 1969.Nitajaribu kukusimulia habari zake baadae.
 
Back
Top Bottom