Naunda kamati ya kuchunguza wabunge wa kamati ya nishati na madini iliyovunjwa

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Baada ya kutafakari kwa kina, nimegundua kuwa kamati nyingi zinazoundwa ama na bunge au serikali aua na chombo chochote kile cha serikali ni kwa ajili ya kula fedha za wananchi tu bure. Hata kama za kudumu za bunge zote ni hadaa na zinakula fedha zetu bure kabisa bila kazi yeyote.

Kamati hizi za bunge zote zinatuhumiwa ama baadhi au kamati nzima kula rushwa kabla ya kutenda kazi, haiingii akili unayemchunguza anakupa usafiri, malazi, chakula na wakati mwingine posho. hizi kamati sio huru wala hazina tija kwa watanzania.

Ukijaribu kuangalia maddudu ya Tanesco ziko kamati nyingi sana zimeyafanya na zinaendelea kuyafanya ila wanatuona WaTZ wote vilaza ndio maanaa wanatuimbia ngonjera kila siku nasi tunakubali.

Tuanze na tuhuma hizi za wabunge wa hii kamati kula rushwa. Kwa sababu wana JF wako kila mahali na ndani ya wizara ya nishati na madini na wanaishi na hawa wabunge ama kufanya nao kazi au kufanya biashara zao. Naomba kwa mara ya kwanza wanaJF mfanye kazi kubwa sana ya uchunguzi bila kumpendelea mtu au chuki.

Rushwa ziko za mfumo na njia nyingi naomba tuchunguze rushwa za namna zote kwa wanakamati hawa.

1. Rushwa ya fedha
2.Rushwa ya kuapatiwa biashara na wizara ya nishati na madini moja kwa moja au kwa njia za panya
3. Rushwa ya kazi kwa ndugu , watoto na jamaa
4. Rushwa ya ngono
5. Rushwa ya kusaidia cheo au debe
6. Rushwa ya chakula malazi na usafiri
8. Rushwa ya ada au kozi mbali za shule.
9. Rushwa ya udhamini wa wizara au miradi ya maendeleo isiyokuwepo kwenye bajeti
10. Rushwa ya nguo kama suti, viatu, manukato, safari za nje na mikutano
11. Rushwa ya posho

Kila mbunge aliyekuwepo kwenye ile kamati iliyovunjwa tumchekeche mpaka tujue ukweli.

Pili Kamati ya Ngwilizi na yenyewe tuichunguze kama imekula rushwa ya kuchunguza kiini macho ili kuficha ukweli.

Chief Mkwawa wa kalenga
Polisi mzuri ni mwananchi mlinda nchi ni mwananchi msema kweli ni muathirika wa uchumi huu wa TZ . Huu ndio muda tuikomboe nchi yetu
 
Kweli kabisa na binafsi naunga mkono hoja hii 100%.WABUNGE WETU kwa kiasi kikubwa wamejisahau. hawajuiwajibu wao ipasavyo.wamejisahau kama walivyo jisahau zamani wafanyakazi wa iliyo kuwa kampuni hodhi ya biashara,RTC.Walidhani watakuwepo milele hata wasipo wajibika. kamati nyingi za bunge wako hivyo!! hutanguliza masilahi binafsi na kusahau wajibu wao kwa taifa. fedha huwafanya kuwa vipofu, fedha huwafanya wasijue kuwa Tanzania kuna watu wenye akili za kuchambua mambo ingawa hawako bungeni.natushirikiane,kwa pamoja ukweli utajulikana. LIVE LONG TANZANIA, LIVE LONG JF.
 
Iliyokuwa Kamati Ya Madini na Nishati:

Nani Msafi nani mchafu kati ya hawa?Mbunge Mussa Silima aliyekuwepo kwenye kamati hivi sasa ni marehemu.

1; Seleman Zedi
2; Diana Chilolo
3, Januari Makamba
4; Dr.Anthony Mbassa
5; Dr,Festus Limbu
6; Lucy Mayenga
7; Prof. Kulikoyega Kahigi
8; Amos Makalla
9; Vicky Kamata
10;Abia Nyakabari
11;Charles Mwijage
12;Catherine Magige
13;Kisyeri Werema Chambiri
14;David Silinde
15;Josephine Chagula
16;Munde Abdalla
17;Sarah Msafiri
18;Ole Sendeka
19;Mariam Kisangi
20;Shafin Sumar
21;Yussuf Nassir
22;Mwanamrisho Abama
23;Yusuph Haji Khamis
24;Suleiman Masoud
25;Ali Mabrouk Salim
26;Pamela Pallangyo
 
Back
Top Bottom