Ndio maana nikawarudisha watu nyuma wakumbuke kwamba UDA ilikufa kwa sababu - WALISEMA -Nyerere sio mchumi huwezi kutoza watu Tsh 1 kwa usafiri japokuwa dollar ilikuwa Tsh17 hiyo ilikuwa kama senti 6 kisha ikapandishwa hadi Tsh 5 bado haikutosha leo hii watu tunalalamika na kuongezeka kufikia senti 13 ya dollar...
Jamani hata ile shilingi moja ya Nyerere ilikuwa kubwa mara ngapi ukilinganisha na Tsh 100 ya leo?... Ni sawa na senti ngapi 6 na ushee, watu wote wanalia ingawa binafsi hata hiyo Tsh 300 ya daladala bado ni ndogo sana haifiki hata senti 20 ya dollar...Halafu tunaambiwa ati nchi imeendelea tunapaa.. haya ebu wekeni kiwango cha daladala sawa na wakati wa Nyerere ihata senti 30 tu ya dollar (Tsh 800) tuone hicho kilio cha wananchi -Tumeendelea!
Mkandara.
Kufa kwa UDA ni matokeo ya kuwa viongozi dhaifu na wenye tamaa; walipoamua kuiua UDA hawakuangalia maslahi ya Taifa na wananchi; usafiri wa ndani ya miji ni muhimu kwa wakazi husika; hii inawasaidia kupunguza gharama za maisha; mtu ambaye hajawahi kutembea ndiye atakayekubaliana nao. Moja ya sababu ya kupanda gharama za maisha Dar es salaam ni usafiri wa daladala; wananchi wengi hivi sasa wanashindwa kupanda daladala kutokana na nauli, sasa jiulize mfanyakazi wa kawaida ambaye ana watoto wawili atayamudu vipi maisha? Hapa ndipo rushwa inapoanza tukumbuke wafanyakazi hawalipwi kulingana na hali ya maisha; tukurudi kwenye UDA ilikuwa inatoa huduma kwa wananchi, lazima tukubali kuna baadhi ya huduma ni serikali tu ndio inayoweza kumudu kuzitoa; hivi tujiulize kwa nini nchi kama Marekani pamoja na kuwa na sera za kibepari hairuhusu watu binafsi kutoa huduma za usafiri ndani miji? Ukienda San Franscisco Bay area, Washington DC metro area, Houston , Boston miji yote ina metro buses ambazo zinatoa huduma, serikali kuu na serikali za majimbo ndizo zinazogharimia uendeshaji; kimsingi nauli za usafiri ndani miji mikubwa kinachoangaliwa sio FAIDA inaangaliwa ni HUDUMA. Mwl. Nyerere alioona mbali zaidi.
Chama
Gongo la Mboto DSM