SOBY
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 1,268
- 458
Serikali yetu siyo ya majimbo (not federated states).....Mkuu ukiangalia baadhi ya sababu alizotoa Magufuli inawezekana wakazi wa Kigamboni wanaonewa. Kwa mfano, magufuli amesema kuwa kupandiswa kwa nauli, kutasaidia kununua kivuko kipya kwa ajili ya safari za Bagamoyo na feri. Kama ni hivyo kwa nini gharama za hicho kivuko cha Bagamoyo walipie wakazi wa kigamboni ambao hawatakitumia? Kama mdau mmoja alivyouliza kwenye thread nyingine, kwa nini "asiwapandishie bei za mabasi na daladala wanaosafiri kati ya dar na bagamoyo?"
Kama Magufuli angekuwa amewashirikisha watu wa Kigamboni kwenye maamuzi yake ya kupandisha nauli halafu wakamwuliza hilo swali angewajibuje? Kwa nini watu wa Kigamboni wagharimie usafiri wa watu wa Bagamoyo? Maana sasa tutaambiwa na gharama ya viwanja vya ndege itapanda kwa ili kusaidia kujenga uwanja wa ndege bagamoyo. Tutaambiwa gharama za bandari inabidi zipande ili kujenga bandari Bagamoyo.
Kuhusu la wabunge, of course, nao ni wa kulaumiwa. Magufuli anasema upandishaji wa nauli ulitangazwa kwenye gazeti la serikali toleo namba 367 Aprili mwaka jana. Ina maana wabunge wote wa Dar Es Salaam hawakuliona hilo tangazo? Kwa nini wamesubiri mpaka sasa ndio wanaanza kulalamika? Lakini pamoja na hayo mimi naangalia zaidi at the root of the problem which is serikali.
Kwa hiyo sioni tatizo la wakazi wa Dar (Jiji ambalo GDP yake ni kubwa kuliko baadhi ya nchi za Africa) kutozwa kodi au nauli ambayo itaweza kuleta maendeleo sehemu nyingine. As long as it's fair. Nchi yetu haiko kimajimbo, kodi zinazotoka Kahama zinajenga uchumi wa Dar, mabbe Kigoma etc.. hiyo ndiyo maana ya watu kuishi nchi moja.
Sasa kuna tatizo gani wananchi wa Kigamboni, kufacilitate maendeleo ya Bagamoyo? Mbona wakazi wa Dar wamekuwa wakilipa maendeleo ya mikoa mingine since day one? That's very common, actually ndiyo undugu huo... you have infrastructures so use those infrastructure to lift others who lack the same infrastructures.
All in all napataga wakati mgumu sana kuwaelewa wabunge wetu, most of them are vuvuzelas.