Natamani wasanii wetu watoke na kibao kama hiki cha Kenya cha Jambo wageni wetu...kenya hakuna matat

zkambele

Member
Sep 18, 2009
7
0
Mara nyingi watalii wanaoingia Tanzania wanaimbiwa kibao cha Kenya ambacho ukweli ni kizuri. Kwa kuwa ni wimbo wa kenya basi unakuta tunatoa Kenya penye Kenya tunaweka Tanzania na inakuwa haina maana sana kwani hata ukienda kwa internet au popote records zinakuwa na "Kenya", hapa huwezi toa Kenya ukaweka Tanzania. Je, wasanii wetu hawawezitoka na kibao kama hiki au kizuri zaidi? Leo mgeni kaniambia nimtumie wimbo huo wa jambo Bwana ambao aliimbiwa na kiongozi wake akiwa safari Tanzania, ila inakuwa si nzuri sana maana unamtumia wimbo ambao unasema karibu Kenya hakuna matata wakati mgeni mwenyewe alitembelea Tanzania tu!! Nadhani kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na wimbo wetu ambao wageni watakuwa wanaimbiwa wakiwa Tanzania na itasaidia kuweka kumbukumbu nzuri na hata kuadithia Tanzania kwa jamaa zao wakiambatanisha an wimbo? Kama wengine wanaweza kwanini sisi tusiweze??

Zeph
"Impossible is a word found in the Fools Dictionary only" Zig Ziglar!!
 
Back
Top Bottom