Nini kimewapata wasanii wetu? Hakuna wimbo mzuri kabisa kipindi hiki cha msiba. Wamezidiwa na TOT? Hakika Komba atakumbukwa

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,255
42,169
Wasalaam wana jamvi!

Baada ya msiba wa Rais mstaafu tulitegemea wasanii wetu ndio watoa faraja wakuu katika kipindi cha maombolezo kwa tungo nzuri zenye mantiki na maana kuu.

Baada ya msiba tumeshuhudia wasanii wakikurupuka kuimba lakini nyimbo ambazo ni mbaya zisizo na mantiki wala maana.

Hakuna msanii ambaye ameimba wimbo ambao unaweza kabisa hata kuitwa huu ni wimbo bora wa kipindi hiki kama ilivyo kuwa kwenye misiba mikubwa ya Ruge Mutahaba na Hayati Nyerere.

Bado najiuliza wasanii wetu waneishiwa vya kuimba? Ni wavivu wa kusoma historia za viongozi wetu? Walishindwa kitumia kitu cha Hayati Mkapa kutunga nyimbo bora?

Hivi kweli TOT wamewazidi wasanii wetu wote lukuki katika kutunga? Au TOT ndio wafatiliaji wazuri? Wasanii wetu ni wavivu wa kutafuta habari?

Bado najiuliza ni wimbo gani mzuri unao uzidi wimbo wa TOT kipindi hiki? Wasanii wetu ni wazi kazi wanayoifanya hawakuitendea haki? Ni haki kuitwa wafanyakazi hewa?

Wasalaam!
 
Wasanii wetu wengi hawajui historia ya nchi hata vitu vidogo vinawapiga chenga,msanii unakuta hata hajui mawaziri atatunga nini,usiwafananishe na Komba aliyehudumu kwenye jeshi na bunge, anajua historia ya nchi siyo kama hawa inama lizame kwa chini
 
Hahahaahaaaaa....
Eti inama lizame kwa chini!!.
 
Wasanii wengi ni zero iq nyimbo zao tu bado mbaya Sasa kutunga nyimbo ka za komba watasubiri Sana kwa kweli. Kuna wimbo TOT wameimba kuhusu mkapa ni wimbo mzuri tu.
In short hii bongo fleva ni mziki wa kijinga na wahuni nyimbo za band na kwaya zitadumu milele
 
Wasanii wetu wengi hawajui historia ya nchi hata vitu vidogo vinawapiga chenga,msanii unakuta hata hajui mawaziri atatunga nini,usiwafananishe na Komba aliyehudumu kwenye jeshi na bunge, anajua historia ya nchi siyo kama hawa inama lizame kwa chini
 
Wakina Diamond na wcb yake walizoea kuimba nyimbo za kuvuana chupi na kutafuta kiki, kwenye mambo sensitive amekuwa mweupe sana
 
Wasanii wengi ni zero iq nyimbo zao tu bado mbaya Sasa kutunga nyimbo ka za komba watasubiri Sana kwa kweli. Kuna wimbo TOT wameimba kuhusu mkapa ni wimbo mzuri tu.
In short hii bongo fleva ni mziki wa kijinga na wahuni nyimbo za band na kwaya zitadumu milele

Hakika huo ndio wimbo bora umetulia na umetungwa vyema na kupangiliwa vizuri sana....hakika ukisikiliza unaona hawa ndio watunzi? Wako wapi wasanii wanao jigamba kuwa wao ni watunzi wazuri? Yuko wapi Mjomba mpoto?
 
Back
Top Bottom