Natafuta mtu anayekusudia kununua gari toka japan wiki/mwezi huu tusaidiane ktk transactions .

Jack2005

Member
Sep 18, 2011
6
2
Salaam!

Mimi ni mtanzania, kwa sasa naishi Japan kwa muda. Natafuta mtu ambaye ana kusudia kununua gari au bidhaa yoyote toka hapa Japan ili tusaidiane ktk transactions za pesa kwa faida ya wote wawili.


Mimi: nakusaidia kulipia gari lako hapa japan kwa kutumia YEN, na hivyo nakuondolea risk ya pesa yako kutapeliwa/kupotea na pia kuepuka gharama za kutuma pesa.

Wewe: Badala ya kutuma USD Japan, una ziweka ktk account yangu ya Tz, na hivyo mimi nita faidika kwa kuto badilisha pesa yangu YEN-USD.

Ili kujenga trust, nita kutumia details muhimu kuhusu mimi, nawe uta zihakiki kujilidhisha. Pia, nita kuelekeza ofisi ya mwanasheria hapo Dar es salaam; mwanasheria ata kusaidia kuku hakikishia usalama wa pesa yako na ikibidi kwa maandishi. Tuta amua, nani alipe kwanza, ili mradi uwe na cash. Naweza nika lipia kisha nawe uka lipa baada ya kulidhika kuwa malipo yako yame fanyika, but hili litafanyika chini ya advocate ili kusiwe na utapeli.

Una weza nitumia namba yako ya simu nami nita kupigia mara moja tuongee. Au kama una tumia Face book bado tuna weza rahisisha mawasiliano. Bidhaa yako isizidi thamani ya US$ 6,500/-.


Asante sana na tafadhali kama una nia nijulishe tufanye mambo fasta, usihofu kabisa kwa maana tayari nime fanya na mtu mwingine na haku kuwa na shida. Wewe nitumie details zako mie nita ku guide tu.
 
Asante sana King'asti na Bw. Nicas Mtei. Yes, huyo King'asti anatakiwa kuwa wa kwanza kuchangamkia dili.
 
Utawapata japo si wengi. Je watajuaje kuwa wewe siyo wale wale tuliowazoea mtandaoni wakifanya vitu vyao kuwaliza wachovu?
 
Utawapata japo si wengi. Je watajuaje kuwa wewe siyo wale wale tuliowazoea mtandaoni wakifanya vitu vyao kuwaliza wachovu?

Asante 'Father of All'. Kimsingi, mwenye nia anitumie tu namba ya simu, e-mail au face book account. Mimi nita wasiliana naye kwa njia hizo na kumpatia taarifa zangu zaidi ambazo anaweza kuzihakiki na kujilidhisha. Zaidi, nita m-guide kwa advocate apate ulinzi wa sheria na kuhakikishiwa usalama wa pesa yake.

Nami nita wasiliana na kampuni husiku hapa JP na kumsaidia ktk process zote za malipo. Na recommend Japanese used cars. | tradecarview.com.
 
Wewe unapata faida gani kwa huo msaada ilihali makampuni kama Autorec na Beforward yapo hapa Dar kupunguzia wateja gharama na kuondoa risk????
 
Kwa jinsi ulivojieleza it sounds good to be true. . . ningekuwa na mpango wa kuagiza gari ningekutumia maana ningesave kama usd 500 hv.
 
Kwa jinsi ulivojieleza it sounds good to be true. . . ningekuwa na mpango wa kuagiza gari ningekutumia maana ningesave kama usd 500 hv.

Asante! Yes, hakuna utapeli hapa, na kwa mtindo huo ni lazima u-save kiasi cha kutosha. Namsubiri mtu alieko tayari tufanye transactions. Naamini ata furahi na kulidhika sana, maana nina wasiliana na kampuni yake moja kwa moja (kwa simu) na kumsaidia ipasavyo. Mwenye nia usikawie tafadhali. Kama una simu nita kupigia pia, ilimradi uwe serious na sio kupotezeana muda na resources.
 
Mda wa kwenda mahakamani au wa Lawyer ni sawa na ule wa kwenda Bank na Kulipa pesa, kusave sana sana utasave dole 50 ambayo n fee ya bank kama Crdb,, na pia nani awe wa kwanza kumpa mwingne pesa? na je kama ww unaishi Tokyo na Kampuni husika niliyochagua gari iko say Hiroshima kutuma pesa ni gharama pia ..mi nadhani hii yako nayo ina risk though wenye interest wtakuja...
 
Mda wa kwenda mahakamani au wa Lawyer...

Mwenye nia ata fanya uamuzi sahihi baada ya kutathimini mambo mengi. Ninacho sisitiza ni mawasiliano na mtu mwenye nia; niko friendly sana, nita m-advise accordingly naye apime mwenyewe kama kweli ata save au la. Ila tayari nime fanya hivi na mtu mwingine na ame pata faida ya kutosha zaidi ya kuwa na amani juu ya pesa yake. Gharama ya kutuma pesa ktk bank yoyote within Japan ni ndogo sana, hilo halina shida. Kuhusu nani alipe wa kwanza sio issue pia, kinacho hitajika ni trust, na hiyo tuta elewana na mtu mwenye nia na halita hariibika neno.
 
Back
Top Bottom