FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,079
- 40,733
Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.
Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.
Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.
=================================
By @ Maulaga59
Najaribu kuangalia changamoto wanazopata maafisa wa sensa wanaotumwa na serikali katika kukusanya taarifa muhimu za idadi ya watanzania.
Ukweli ni kwamba kwa sababu ya mazingira ya Tanzania yalivyo kijiografia ni vigumu sana hawa maafisa kuweza kupata takwimu sahihi za kusudio lao. Kuna sehemu ambazo huwa siyo rahisi kufika kwa gai au kwa mguu kwa sababu mbalimbali kama vile mapori, mabonde, milima, wanyama wakali na kadhalika.
Wenyeji wa maeneo hayo wao wanao uzoefu hata wa kufika makao makuu ya wilaya lakini si kwa wageni na muda mfupi wanaokuwa wamepewa kufanikisha zoezi.
Balozi wa nyumba kumi wangepewa semina za kufanya zoezi hilo wangeweza kuja na takwimu sahihi zaidi kuliko zile za maafisa waliotumwa.
Kila balozi angeweza kupeleka takwimu za watu wake kwenye ofisi ya kata na ofisi ya kata ingeratibu zoezi hilo katika eneo lake, kisha kupeleka ngazi za juu hadi ngazi ya taifa.
Zoezi hili siyo tu lingeleta takwimu sahihi zaidi bali pia lingepunguza gharama kubwa ambazo serikali hutumia katika kufanikisha zoezi zima.
Kwa huu utaratibu unaotumika kila baada ya miaka 10 watu wengi huwa wanaachwa bila kuhesabiwa hasa kwenye maeneo magumu kijiografia.
Nadhani miaka ijayo kazi hii ifanywe na mabalozi wa nyumba kumi.
Nawasilisha.
==================================