Nape, Umeyasema haya kwa kukusudia, Umetumwa na Chama au Umekosea kwa bahati mbaya?

Mkuu betlehem
Kauli ya Nape Nnauye sielewi inakupa shida wapi kwenye uchaguzi wa Kenya 2007 waliaonzisha vurugu ni walioshinda uchaguzi au walioshindwa?

Chama
Gongo la mboto DSM
Take a cup of coffee and relax, si kila hoja inahitaji propaganda uchwara, kaa pembeni angalia michango ya wenzako unaweza ukaja kuongea la maana.
 
Baada ya Jk, wa pili kueneza udini kwa kasi ni Nape Nnauye! Mbaya zaidi yeye ameongezea na ukabila sijui anapata faida gani huyu kijana kuona watanzania wanagawanyika!

Vijana wa Chadema mbona mnajichanganya sana kwenye hili la udini? JK muislamu; Nape Nnauye mkristo hivi mnaelewa mnachokiongea au nyie ndio mnaotawaliwa na dhambi ya udini?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kwa hoja hii, anamanisha hata wakishidwa watatumia jeshi ilikunusuru hali halisi.

Ni ujinga sana kufikiri namna hii.

Yaani hiyo ndo alichomaanisha huyu Nape. Mi huwaga sina muda wa kumsikiliza na anakipeleka chama shimoni na yeye kubaki historia kama katibu mwenezi wa mwisho. May be he is trying to create such a history to his political party
 
Take a cup of coffee and relax, si kila hoja inahitaji propaganda uchwara, kaa pembeni angalia michango ya wenzako unaweza ukaja kuongea la maana.

Najadiliana na mtoa mada na nina sababu ya kumuuliza nilichouliza ili tuwe kwenye mstari mmoja kama unalo jibu msaidie huna jinyamazie!
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Naipenda sana siasa lakin sio wanasiasa najaribu kuvuta picha uchaguzi mkuu ujao ukiwa huru na wa haki hiv ni wapi watu kama nape watazificha sura zao?? Eeeh mwenyez mungu nipe uzima ili nipate kushuhudia
 
Ndugu mleta hoja ninakushukuru ila ninadhani Nape ni janga la kitaifa kwa CCM wangealia nafasi nyingine ya kumpa ama wamuondoe tu. Propaganda zinazidi mpaka anatia kichefuchefu. Kwa kweli binafsi siwezi kusikiliza chochote anachoongea Nape kama sina cha kuangalia au kusikiliza ni bora nikazima TV au Radio maana anaboa kupia kiasi. JK angalia cha kumfanya huyu dogo. Inaelekea hata malezi yake yalikuwa si mazuri utotoni. Hana lolote lililobora kwa Chama. Ninashauri nafasi yake angepewa mtu ambaye atahakikisha uhai wa Chama Chetu vinginevyo TUMEKWISHA
 
Tatizo la Nape hajui wajibu wa CCM kama chama kilichoshika dola na wajibu wa Chadema kama chama cha upinzani. Katika hoja za Chadema ilitakiwa CCM ijibu kwa vitendo na wananchi waone sio kujitetea kwa kashfa,propaganda za kijinga na kejeli.
Wananchi walipoichagua CCM (kama waliichagua)hawakuipa dola ili ije ipambane na vyama vya upinzani bali iwakomboe toka katika lindi la umasikini,ujinga na maradhi. Sasa yote hayo yameongezeka maradufu na chati ya CCM imepanda tuu katika propaganda,matusi na kejeli. Kila siku studio ya chama inatoka na single mpya kuhusu Slaa,Mbowe,Mnyika,udini,ukanda na takataka zingine nyingi.
Nape hajengi chama bali anakibomoa,na kama cheo chake kingekuwa pengine cha kupigiwa kura na NEC ya CCM wangeshamuondoa ila kwa vile ni cha mapenzi ya mwenyekiti ndio maana bado yupo hapo.Maana kama wengi wanavyo mfahamu mwenyekiti huwa hayaoni mambo kwa jicho la tatu hivyo hata maamuzi yake yamehojiwa sana katika nyanja nyingi bila majibu.
Nape jitambue kuwa wewe ni mtaji mkubwa sana kwa vyama vya upinzani,unawasaidia katika harakati zao za kuiua CCM bila kutumia gharama kubwa.
 
Unasemaje sasa kulingana na tuhuma za Nape, zinawaharibia au zinakijenga zaidi chama???

Hapo hakuna tuhuma alichosema ni kuwekea mkazo dhidi ya siasa za chadema ambazo zinataka kutukita kwenye vurugu za ukabila na ukanda kwa maana hiyo ni sahihi kabisa

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Vijana wa Chadema mbona mnajichanganya sana kwenye hili la udini? JK muislamu; Nape Nnauye mkristo hivi mnaelewa mnachokiongea au nyie ndio mnaotawaliwa na dhambi ya udini?

Chama
Gongo la mboto DSM
Kwahiyo hapa tukubaliane Nape si Mtoto wa Musa Nnauye na ndio maana hakuwemo kwenye orodha ya Wanafamilia. Musa Nnauye alikuwa Mwislamu.
 
Tatizo la Nape hajui wajibu wa CCM kama chama kilichoshika dola na wajibu wa Chadema kama chama cha upinzani. Katika hoja za Chadema ilitakiwa CCM ijibu kwa vitendo na wananchi waone sio kujitetea kwa kashfa,propaganda za kijinga na kejeli.
Wananchi walipoichagua CCM (kama waliichagua)hawakuipa dola ili ije ipambane na vyama vya upinzani bali iwakomboe toka katika lindi la umasikini,ujinga na maradhi. Sasa yote hayo yameongezeka maradufu na chati ya CCM imepanda tuu katika propaganda,matusi na kejeli. Kila siku studio ya chama inatoka na single mpya kuhusu Slaa,Mbowe,Mnyika,udini,ukanda na takataka zingine nyingi.
Nape hajengi chama bali anakibomoa,na kama cheo chake kingekuwa pengine cha kupigiwa kura na NEC ya CCM wangeshamuondoa ila kwa vile ni cha mapenzi ya mwenyekiti ndio maana bado yupo hapo.Maana kama wengi wanavyo mfahamu mwenyekiti huwa hayaoni mambo kwa jicho la tatu hivyo hata maamuzi yake yamehojiwa sana katika nyanja nyingi bila majibu.
Nape jitambue kuwa wewe ni mtaji mkubwa sana kwa vyama vya upinzani,unawasaidia katika harakati zao za kuiua CCM bila kutumia gharama kubwa.
 
Nape alifanya mkutano na wananchi wa Goba (Dar es salaam) tarehe 17/2/2013. Mimi sikuwepo katika mkutano huo lakini nimesikiliza sehemu ya hotuba yake kupitia kipindi cha Chombo Kazini cha Redio Uhuru cha jana saa 8;30 usiku. Katika mazungumzo yake alisema mambo mengi ila mimi nitazungumzia machache tu yaliyonifanya nipate shida kidogo usiku wa jana.
Miongoni mwa mambo aliyosema ; alisema CCM inalinda amani na CHADEMA inavuruga amani. Alipokuwa akifafanua hoja hii, alitoa mfano wa uchaguzi wa Kenya akasema hivi "Mnaona nchini Kenya kwenye uchaguzi wa 2007, Kibaki na Odinga walikuwa na misuguano, Kibaki akaamua kujiepusha Odinga akaingiza watu mitaani na kusababisha mauaji".

Kauli hii imenipa shida sana hata nikajiuliza kama ndugu Nape katumwa kusema haya!, Je! Ndo msimamo wa chama au kaongea tu pengine bila kukusudia!. Mkuu Nape Nnauye; Unatakakuwaambia watanzania vurugu baada ya uchaguzi nchini Kenya zilisababishwa na upinzani? Mheshimiwa Nape unataka utuambie kwamba uchaguzi wa 2015 CCM ina mpango wa kuchukua nafasi ya Kibaki 2007 na CHADEMA wachukue nafasi ya Odinga?

Nape; Unaongea nini! Suala la uchaguzi 2007 nchini Kenya inaonekana wazi kwamba chama tawala kiliwadhulumu wapinzani na hili lipo clear Dunia nzima; Nape, unatoa taswira gani ya chama kwa jamii? Mkuu kwa hili mim[/COLOR]i betlehem umenikatisha tamaa kweli!. Hivi unadhani ni nani atakae endelea kukutetea kwa utaratibu huu; Hakika hata mtu aliepata division four hawezi kusimama na kutetea jambo hili na sasa naanza kupata mashaka kwamba hizidivision "0" 60% zimetokea kwa kukusudiwa ili kupata waungaji mkono wa hoja kama hizi.[/FONT][/SIZE]

Mh.Nape ; wewe umendelea kusema "CHADEMA ni chama cha kibaguzi". Hivi hoja ya kwamba ukisema chadema ni chama cha kibaguzi kwa misingi ya dini na ukabila utawawekea mazingira ya wao nao kusema CCM ni cha kibaguzi hujaielewa tu bado?

Ndugu yangu Nape, huoni unaendelea kuigawanya jamii na kuchochea chuki za kidini na kikabila? Ina maana pamoja na
Mzee Mwanakijiji kutukosoa kwa kejeli za wazi katika uzi wake wa PENDEKEZO LA WASTANI: Tusiishie kutengana kwenye kuchinja; tutengane kwa kila kitu... wewe umeamua uwe mtu wa kwanza kutomuelewa! Kweli mkuu!


Ndugu yangu Nape; wewe umewalaumuCHADEMA kwa kutoa namba ya simu ya Spika na hatimae Spika katukanwa: Kulaumu ni sawa maana hata mimi nililaumu, lakini kwa hoja ya kwamba " ijapokuwa kutoa namba ni sahihi lakini mazingira haya kuwa sahihi".Sasa wewe unasema "kwa nini watoe namba ya spika na wasitoe namba za wake zao "

Hivi ndugu yangu Nape; Uko serious kwenye siasa, au unafanya masihara!. Hivi unadhani huu ni mudawa kuendelea kufanya siasa za hila badala ya hoja? ndugu yangu Nape; elewa kwamba wenzetu wa CHADEMA wana vijanawenye akili ambazo ziko fasta zaidi ya google. Wanaweza kutafakari kitu na kukitolea maelezo ya kitaalam ndani ya sekunde. Unadhani kwa siasa za hila tutatoboa?


Mkuu Nape; wewe umekuwa ukitumia maneno yakejeli dhidi ya CHADEMA. Kwa mfano; tarehe16/2/2013 wewe na Lema mlikuwa mnahojiwa na Deustche Welle, wewe ulikuwa unatumia maneno ya kejeli mpaka mtangazaji akakuonya. Sitaki kuyataja maana unayafahamu vyema. Je! huoni kwamba kufanya hivyo unawasukuma hawa wenzetu wa CHADEMA kutukejeli? Ona sasa wanamuita Rais/mwenyekiti wetu eti ni dhaifu! (Tunajidhalilisha watanzania.)

Ndugu yangu Nape; elewa kuwa hakuna mtu yeyote amabaye walau anafikiri hata kidogo atakaye kutetea kwa hoja hizi. Kwa mtindo huu hatuwezi kutoboa 2015. Na sio tu kwamba tutaangushwa bali tutaangushwa kwa aibu kubwa. Hakuna mtu mwenye akili ambaye atakubali aibu hii imkumbe akiwa ndani ya CCM. Tuangalie chama kisije kikafika 2015 kikiwa kimebakina viongozi wa Lumumba pekee huku wafuasi hakuna. Mkuu dawa ya homa kali ni sindano japo inauma. Sasa inapotokea mwana familia anaumwa tumuache afe? hapana; mimi betlehem nita hakikisha anapata sindano za masaa ili aweze kupona japo akilia kwa uchungu mimi itakuwa inaniuma sana!. Pamoja na sindano; Ikitokea akifa kwa sababu ya ukali wa homa, mungu atakuwa kampenda zaidi.

Nape, ikiwa nimekusingizia au hoja zangu si sahihi? Karibu uchangie mada na unikosoe!.
mawazo yakao yako sawa,lakini ccm wameshaamua tuingie kwanye vita kuliko wao kuwa tayari kuachia dola,hivyo maneno ya nape hakuna kiongozi hata mmoja ataona yana hatari,maana hivyo ndivyo wanavyotaka
 
Batlehem,

Kwa utashi na busara zako tunaweza kulifikisha taifa hili mahala pazuri. KImsingi huwa najiuliza sana huyu Nape huwa anajua anachoenda kukizungumza mbele za watu. Marehemu Prof. Seti Chachage alishawahi kuniambia na namnukuu "UKIONA NGOMA INALIA SANA UJUE INAKARIBIA KUPASUKA" haya maneno yananishawishi kwa namna mbili Mija, Nape ndio kwisha habari yake naamini hata nyumbani anasalimiwa kwa sababu ni baba, lakini pili kwa yeey kuwa mmoja wa wasemaji wa chama ni ishara tosha kuwa chama kinajichimbia kaburi.. Ni hayo tu
 
Nilishasema,nape sio mwanasiasa,the guy is just a polical goon,nape always hana hoja zaidi ya kejeli na matusi.siasa zake ni za kihuni sana,suala la kusema wakatoe namba za wake zao was so pathetic,sikutegemea kama nape anaupeo mdogo wa kufikiria namna hii.kilichotokea 207 kenya kila mtu aliona.nashawishika kusema nape wamejipanga kutumia mbinu ya kibaki wakishindwa uchaguzi ujao.let me remind you mr nape,kuna the hegue wewe ropoka tu.
 
Did he really say that???????!:nono::A S 39::lalala:

Kwa Nape kusema hayo sio ajabu, Tabora alisema CDM wanatushikisha ukuta, afu Mwanza alisema mimba changa zinawasumbua,...Ndo katibu mwenezi huyo. Ataki cost sana chama chake kwa kauli zake
 
Back
Top Bottom