NAPE: Tumetuma Vijana wapeleke mashambulizi mitandao ya kijamii

Faizafoxy et al mko wapi, hivi ni kweli nape amewatuma?
 
Ukiona kijana hashiriki kwenye mijadala mpaka aombwe na Nape , jua huyo kijana nae ni mgonjwa.
 
Hivi kwa nini ni Nape pekee anayeleta taabu mtandaoni na kwenye magazeti? kachuuzwa ninii??

Kwa taarifa yako nape haleti tabu yoyote zaidi ya neema, kosa dogo ni faida kwa wanamageuzi na yeye amefanya mengi tu
 
Nilimsikiliza Nape Juzi akihojiwa Mlimani TV, moja kati ya mikakati yao ni kuwafikia vijana wengi popote walipo. Kati ya njia wanazozitumia ni kutuma vijana waingie kwenye mitandao ya kijamii ambako wanaamini kuna vijana wengi na hii itawasaidia kuwapata.

Hili wimbi la wanachama wapya kwenye hii mitandao, hususani jamiiforums, ambao wana itikadi za kimagamba limenifanya niamini kauli hii ya Nape. Lakini waje wakitambua vijana wa kileo wanajitambua na propaganda za magamba haziwezi tena kuwashawishi.

Hongera Nape lakini hii strategy, kama zilivyo nyingine, naamini haitafanya kazi kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa chama chenu cha magamba ni mbovu na ndio tatizo.

What a poor and desparate strategy! Any way CCM watumeni tu lakini ukweli will prevail kuwa akili ya kushikiwa popote pale duniani siyo humu JF tu haijawhi kushindana ikaishinda akili isiyo ya kushikiwa.

Hapa JF issue siyo kubishana hapa ni maswala ya substance na objectivity. Njia ni kujirekebisha sio kutuma vijana wa mashambulizi ambao wameonekana kupwaya kuliko Makamba.
 
Siku zote nimekuwa nasisitiza na bado ntaendelea kusisitiza kwamba Nape ni BOGUS. Inapofika hatua Chama tena Chama tawala kinatuma watu badala ya watu hao kujituma wenyewe kukitetea Chama chao basi ujue hata hao watu waliotumwa hawana imani na Chama chao.

Kinachowasukuma vijana hao si dhamira za moyoni bali ni njaa tu. Malaria Sugu, Ritz, nk ni baadhi tu ya hao waliotumwa na Nape kujibu mashambulizi humu Jamvini. Lakini historia inaonyesha kwamba watashindwa tu maana siku zote ukweli na uongo hujitenga kama tulivyoweza kuwagundua kabla ya Nape mwenyewe kusema wametuma vijana kujibu mashambulizi mitandao ya kijamii.

Nape pole, your real BOGUS!
 
Hao vijana alio watuma hawataweza kufanya lolote hapa JF, hawata weza maana wametumwa, hawajasukumwa na dhamira zao kutetea kile wanacho amini kina tija kwa maslahi ya taifa wamekuja hapa Jf kusimamamia maslahi ya chama bila kujali kinachojadiliwa, wametumwa kukutea chama si kujenga hoja zenye maslahi kwa taifa. Wanatumika kushibisha matumbo yao yenye njaa. Wanaangalia shibe ya matumbo yao na kusahau ndugu zao watanzania kule vijijini wasio kuwa na uhakika na kipande cha nguru wala usiga wa kupitisha lepe la usingizi. Anae watuma ana mishahara 2, ana tumbo kubwa na anatembelea mgari wa dorari wenye mikanda ya manyoya, likisimama lina nesa kama muanzi upigwao na upepo, anao watuma wanakuja kuwatetea watu waliopigika, hawana hata vyupi vya ndani! Kama wanavyo zina viraka kama msafara wa magari ya loliondo kwa babu, wanakula upepo badala ya chakula huku wakiwa wamevalia fulana na kofia zenye picha ya jembe na nyundo (MAISHABORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA). Kigumu chama cha magamba.
ZIDUMU FIKRA ZA NAPE KUWATUMA VIJANA HAPA JF.
 
Ni bora angeenda vijijini kama kuwaadaa vijana wa kule ambao wengi wao wanaonekana bado hawana mwamko.
Lakini inakuwaje CCM inafikiria kushinda uchaguzi tu muda wote kuliko mikakati ya maendeleo!!
 
Hili game awataweza .Hata kabla ajasema tunajua kwani moja ya mikakati nikupambana na wanajf .Makao makuu ccm wameajiri vijana wa3 kuwauganishia IT pale kwa ajiri hiyo . Wanajulikana na wala usijisifu . nichangamoto tu
 
Mfikishieni ujumbe, kuwa vijana wake wamefeli, badala ya kujenga, wao wanabomoa.

Huyu Jamaa nilimsikiliza juzi akihojiwa na Clouds FM, kama yeye binafsi uwezo wake wa kuelewa ndio ule, sijui hao anaowaita vijana wake watakuwa na uwezo gani!

Jamaa ana uwezo mdogo sana wa kuelewa anachoulizwa na vilevile ajibu nini kwa swali aliloulizwa mpaka ikafika mahali Mtangazaji wa clouds, Kayanda akawa anamsaidia.

Huenda miongoni mwa vijana wake ni kama hawa wanaoongea pumba humu kama Malariasugu, Geniusbrain, yule dada ustaadh, na kuna mpemba mmoja.
 
Ukiona kijana kama NEPI anaongea pumba kwenye TV tena kwa kujiamini basi ujue ubongo wake unamatatizo makubwa sana, bora angekuwa mvuta bangi tungejua ni bangi tuu hizo lkn kama havuti basi ana laaana.
Kama kiongoz wa juu alitakiwa apange jinsi ya kuwafanya watu wakose cha kusema kwa kuwatendea wananchi maisha watagemeayo kama walivyooahid kwenye kampeni, lkn kupeleka mashambiliz kwenye mitandao wakati upo uchi..ni upuuzi, hii ni sawa na "kuvua taulo kufunika TV watoto wasiangalie picha chafu na kuacha nyeti zako wazi watoto wakizinagalia".

Akili za NEPI + Mkuu wa Kaya = O, Eti naye alituma mawaziri wazunguke majimbon kueleza mazuri ya serikali..huu si upuuzi. MAZURI YANAELEZWA AU YANAJIELEZA YENYEWE KAMA YAPO!! kama mazuri hayapo ukiwaeleza wananchi ndio watakubali hivi hiv tu kijinga kijinga.

Kwa akili hiz za viongoz wake, Chama Cha Mavuvzela kimefikia ukingoni,KIFO chake ki karibu sana.
 
Ukiona kijana hashiriki kwenye mijadala mpaka aombwe na Nape , jua huyo kijana nae ni mgonjwa.

hakika ni wagonjwa, hivi wanategemea nani atazikubali pumba zao hapa? Mi naona wanapoteza muda tu., siyo JF wala FB wanakoweza kuishi wagonjwa wa aina hii, tusubiri kifo chao muda si mrefu.
 
Nilimsikiliza Nape Juzi akihojiwa Mlimani TV, moja kati ya mikakati yao ni kuwafikia vijana wengi popote walipo. Kati ya njia wanazozitumia ni kutuma vijana waingie kwenye mitandao ya kijamii ambako wanaamini kuna vijana wengi na hii itawasaidia kuwapata.

Hili wimbi la wanachama wapya kwenye hii mitandao, hususani jamiiforums, ambao wana itikadi za kimagamba limenifanya niamini kauli hii ya Nape. Lakini waje wakitambua vijana wa kileo wanajitambua na propaganda za magamba haziwezi tena kuwashawishi.

Hongera Nape lakini hii strategy, kama zilivyo nyingine, naamini haitafanya kazi kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa chama chenu cha magamba ni mbovu na ndio tatizo.


Kumbe humu ndani kuna WATUMWA...waliopewa laptop za bure .....na posho kila mwezi....,wanatakiwa wajuwe kuwa JF watu wana mkoma nyani giladi toka moyoni toka enzi hizo ,kwa mapenzi ya nchi yao na hawalipwi zaidi wanajitoa....

Watu wanaolipwa humu ndani utawagundua kwa hoja zao dhaifu...na hata wanayoyaandika ukiyasoma utagundua HAWAYAAMINI...na yumkini utakuta wameingia kwa majina mawili ....hasa wa vyuo jina moja la mshahara,.....na jina lingine la kumkoma nyano giladi......CCM wajuwe wanaliwa tu........

Wameshindwa kutambua mchango wa member wachache huku ambao wamekuwa wakiitetea CCM kwa moyo .....wanaenda kukodisha merceneries wa vyuo ambao ni wazi inajulikana hawana mapenzi na CCM zaidi ya kuwachuna tu...
 
Kaulì yake ina ukweli maana wanatokea kina lowasa humu den wanakimbia kujibu kbs ww nepi ujipange xwa xwa
 
Ninamuhurumia sana huyu kijana kwani hadi sasa yeye na katibu mkuu wake hawajui ngoma wanaoicheza nadhani hata wao wapo pale kwa ajili ya mishahara na marupurupu tuu. Ila nadhani amefanya jambo la busara kuleta vijana wake hapa ili wajifunze mapya ya ukweli nadhani pia itasaidia CCM kubadilika. Waje na hoja za msingi na siyo matusi au mistari ya mipasho kama walivyozoea. karibuni sana Napeboyz:)
 
Back
Top Bottom