Nape: Sikuwahi sema kuwa Mafisadi wataondolewa CCM baada ya siku 90

Status
Not open for further replies.
SI swala la kudai wala vikao kuamua upya bali vikao VILISHAFANYA UAMUZI NA UAMUZI NI WAJIPIME NA KUONDOKA WENYEWE WASIPOFANYA WATAFUKUZWA NA CHAMA.

SWALA LA LINI NI PERIOD KUTOKA KIKAO KILICHOPITA CHA NEC MPAKA KIKAO KIJACHO CHA NEC, AMBACHO KWA MUJIBU WA KATIBA HUWA KINAKUTANA KILA BAADA YA MIEZI MINNE. Lakini SI LAZIMA IWE MIEZI MINNE KAMILI,KATIBA YA CCM INARUHUSU KUWA NA VIKAO MAALUMU KATIKATI KABLA YA MUDA HUO,HIVYO NEC INAWEZA KUKUTANA KABLA YA MIEZI HIYO KATIKATI KAMA ITAONEKANA IPO HAJA. NA INWEZA IKAKUTANA BAADA YA MIEZI MINNE KUTOKANA NA MAZINGIRA,KWA MFANO NAFASI YA MKITI KAMA IMEBANA TUNAWEZA KUSOGEZA MBELE SO SI SWALA LA SIKU EXACTLY.

ANGALIA HATA BUNGE KUNA MUDA UMEPANGWA LAKINI LINAWEZASOGEZA SIKU ZA KUANZA AU KUMALIZA KUTEGEMEANA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO.

Kikubwa hapa NI KUWA WAHUSIKA WAMEITWA NA KUJULISHWA UAMUZI WA NEC NA KUWA UPO MUDA WA WAO KUTEKELEZA WASIPOFANYA KIKAO KIJACHO CHA NEC NI KUWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI ITAKAYO ONYESHA IMETEKELEZWA KWA KIASI GANI NA KUTEKELEZA SEHEMU YA PILI YA UAMUZI.

KUMBUKA ILISEMWA HAPA JF KUWA UAMUZI HUU HAUTATEKELEZWA NA KUWA HAYO YALIKUWA MANENO (yalitumika maneno makali, machafu) YA NAPE NA CHILIGATI SI UAMUZI WA CHAMA, AKATOKA DR. KIKWETE MWENYEKITI WA CHAMA AKASEMA PALE DIAMOND ALIPOONGEA NA MAASKOFU KUWA ANACHOSEMA NAPE NI UAMUZI HALALI WA CHAMA, WATU WAKAFUMBA MACHO NA MASIKIO NA KUENDELEA KUDAI NI YA NAPE NA KUWA WATUHUMIWA HAWATACHUKULIWA HATUA ZOZOTE HATA KUJULISHWA TU. WAMEITWA NA KUPEWAA UAMUZI WA NEC, WATU WAKAKIMBIA JF, HATA WALE WALIONITUKANA NILIDHANI WATARUDI KUPONGEZA HATUA ILIYOFIKIWA, SIKUWAONA.

NINACHOWEZA KUHAKIKISHIA HAPA UAMUZI HUU WA KUWAWAJIBISHA BAADHI YA WATUHUMIWA HAUTABADILISHWA KWA KELELE ZA BARABARANI NA SARAKASI ZA WATUHUMIWA, TUMETHUBUTU KUAMUA, TUTATEKELEZA MAAMUZI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

NAPE Mdogo wangu!

Utayakumbuka maneno yangu; Lakini kwa kifupi ni kwamba..

Tuachilie mbali hiyo HALMASHAURI KUU YA CCM au KAMATI KUU YA CHAMA, MWENYEKITI WA CCM na KATIBU MKUU WAKE au WEWE NAPE NNAUYE.......

Mnafahamu wazi kwamba CCM haina ubavu wa kuwafukuza katika Chama watu wafuatao:-
  1. Edward Lowassa (Rais ajaye)
  2. Andrew Chenge na,
  3. Rostam Azizi
CCM HAMUWEZI NA HAMTAKAA MJARIBU, Kinachofanyika sasa ni kutafuta namna ya kulimaliza hili suala kisiasa, mnataka mwishoni mseme wameomba radhi, au mnataka kutumia njia zilizomzimisha "HO-KO", kwa hawa hamtaweza KUTUBUTU!

Take my word
 
Kumjadili Nape na statements zake ni kupoteza muda .Dogo hana ajualo watu wana mwangalia .Nape ni mtupu nilisha waeleza hapa .Just ignore the boy na sarakasi za Chama chake .
 
Haya, mduara umeanza! Sasa Nape anasema hakuwapa siku 90! Sijui kama Nape anajua kwamba enzi za watanzania kudanganywa danganywa zimeisha na watanzania wa leo wanafuatilia mambo mpaka mwisho.

Wenye busara walishawaonya CCM kwamba ingewawia vigumu kupambana na mafisadi kwa siku 90, wao wakaendelea kusisitiza kwenye mikutano mpaka kwenye Redio na TV. Leo anahunyahunya eti hawakutamka kufukuzwa kwa hawa waheshimiwa sana ndani ya chama chao kabla ya kipindi hicho kupita.

Mimi nasema hii ni sarakasi tu na hakuna lolote litakalotokea maana kama ni magwanda tu wapo wengi mno wa kujivua labda kumkumbusha tu Mheshimiwa huyu lipo lile jopo zima la vibaka waliotuingiza mkenge IPTL kina Mollel, Manyanya, Kikwete, na wengine, kisha twende kwa wale wa Richmond, Kagoda na EPA nzima, Meremeta, Buzwagi, TICS, waliolangua viwanda na mali za taifa nyingine wakizihonga kwa marafiki na vimada wao, waliohusika kuuza nyumba za serikali na nyingine kuzihonga kwa mahawara zao, wote waliohusika na utapeli wa ununuzi wa nyumba kule Italy (Licha ya hawa "wahusika" wawili wanaohenya mahakamani peke yao; kwani wao ndiyo waliokuwa waamuzi wa mwisho?) waliohusika na Aggreco, Songas hadi walioliua TTCL kwa kuvuta mshiko, na wooote.......

OOOh orodha ni ndefu mno na inamgusa kila mwana gamba. Nasema kwamba hakuna mwana magamba asiyeijua ladha ya rushwa labda aliyezaliwa leo na hata huyo naye atafungwa kwa nepi iliyonunuliwa kwa fedha ya wizi tena wa mchanaaa kweupeee!

Suluhu ni moja tu, kukitosa CCM na kuanza upya.
 
Nape wewe ni mchanga sana kwa siasa za CCM, wenzako magamba yamekomaa wewe unataka uyang'oe! Usipo angalia utang'oka wewe magamba yatabaki!

Ulianza na siku 90, Mukama akasema labda kikao cha chama kijacho, wewe ukasisitiza-siku 90 ziko palepale, leo unarusha mistari. Tunasubiri za Mukama ziishe tuone nini kitatokea.

Wewe Nape nenda kwenye mikutano ya wanafunzi ukacheze kiduku kama ulivyozoea maana hao ndo saizi yako, kazi ya kung'oa magamba muachie JK.
 
Walifikiri siku 90 ni karne moja zitafika wao hawapo hata wakisema 120 zitafika tu.
 
I'm not crossing my fingers.Yaani miezi mitatu inakaribia kuisha mara mnaleta kibwagizo kipya cha miezi miNNE?Fool me once shame on you,fool me twice shame on me.
Hata kama ingekuwa miezi sita kinachoangaliwa hapa ni maamuzi kulingana na mazingira halisi ya chama. Chama siyo mbio kwamba kama wamesema baada ya siku tisini then siku ya tisini saa usiku watekeleze uamuzi. Kumbuka maamuzi ni sayansi kwa hiyo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia realitiies na hata kama wakiamua kubadili maamuzi watafanya provided ni kwa manufaa ya chama chao.
 
Walifikiri siku 90 ni karne moja zitafika wao hawapo hata wakisema 120 zitafika tu.
Watanzania bwana, mbona mnashadadia sana hili swala.

Nchi yetu haiwezi kwenda kwa namna hii. Watu badala mfanye kazi za kujenga nchi yetu mmekalia kusubiri siku tisini utadhani kipindi kile sekondari watu walivyokuwa wanasubiri siku ya kufunga shule. Hata kama leo hii CCM itawafukuza wanachama wake wote hiyo haitakuwa na manufaa yoyote kwa watu binafsi tusipojituma na kufanya kazi.

Ushauri wangu ni kuwa tusizame sana kwenye mambo haya mpaka tukasahau mambo ya msingi ya kujituma na kujieletea kipato kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu siyo kila siku Lowasa, Nape.

Tufanye kazi jamani.
 
Hata kama ingekuwa miezi sita kinachoangaliwa hapa ni maamuzi kulingana na mazingira halisi ya chama. Chama siyo mbio kwamba kama wamesema baada ya siku tisini then siku ya tisini saa usiku watekeleze uamuzi. Kumbuka maamuzi ni sayansi kwa hiyo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia realitiies na hata kama wakiamua kubadili maamuzi watafanya provided ni kwa manufaa ya chama chao.

Real??? Nafikiri hii linge-eleweka kama kingekua sio chama tawala. Lakini kwa mtizamo wangu: CCM kama chama tawala kinahitaji kufanya maamuzi sio kwa manufaa ya chama bali Taifa.
 
Ni kweli! Wasipojivua gamba analopita nchi nzima kututangazia hatuwezi kumwelewa. Na hapo watakuwa wameliwekea maua kaburi la chama chao.
 
Kwa nguvu gani aliyo nayo ya kuwaeliminate akina el.tupo baba yetu macho na kusubiri kwa uchu 2015
 
Nape bado hajitambui. Kama kweli amedhamiria kuvua gamba ili kusafisha Chama mbona bado hajawapa Rostam azz, lowasa na chenge barua? Nimegundua Nape ametumwa kucheza mchezo asio uweza
 
Nape ni kama mgonjwa aliyeko ICU yaani ahera hayupo duniani hayupo basi ana hang tu katikati ..boraniangalie futuhi kulikokumsikiliza nape
 
Nimefurahi kusikia kwamba NAPE anaogopa nguvu ya umma. Sijui kama kweli ataweza kuvua magamba ya wenzao wakati yeye mwenyewe ni gamba la kuanzisha CCJ.

Source: Tanzania Daima Ya leo
Nape: Kujivua gamba lazima

CCM wana ile sera inayosema kinyozi hajinyoi. Ila kwa hili la kukisaliti chama NAPE lazima ang'oke. Afadhali yote ila hili la usaliti ni baya Halina tofauti na ile habari ya Yuda kumsaliti yesu, ambapo suluhisho ilikuwa ni Yuda kujinyonga tofauti na wenzake wakina PETRO ambo wallimkana tu Bwana baadae wakatubu wakaendelea kupiga mzigo, hili la Nape na Sita na Mwakyembe Halivumiliki. Hawa ni nyoka wabaya ambao wanasumu kali. Kilichopo kwao ni madaraka tuuu ndiyo maana walipotulizwa kwa vyeo wametulia, kinachoendelea kwa mtu kama NAPE ni kuendeleza siasa za majungu, chuki na fitina. Watanzania hawataki hayo wanataka maisha yao yabadilike NAPE!!!
 
Zile siku za tisi alizotoa Nape Nnauye, kuwa zikifika ni ama za mapacha ama za CCM zimetimia na kilele chke ni jumapili tarehe 10 july 2011. Usanii wa Nape tayri umedhihirika kwani amekwisha nukuliwa na vyombo kadhaa vya habari akiikana kauli yake hiyo. Ila kwa kumbukumbu ni kwamba alitoa kauli hiyo tena sio mara moja na kwa msisitizo mkubwa, hata alipohojiwa Mukama na waandishi wa habari kuhusu siku tisini zile alikataa na kusema hakuna kitu kama hicho.

Leo Nape akiwa anatembelea gazeti la Mtanzania daima amekaririwa akisema kuwa kulikuwa na makosa ya kutekeleza na maagizo ya kikao kile kwani kuna mambo hayatekeleziki. wachunguzi wa mambo wamebaini kuwa swala la kuwatoa wafadhili hawa ndani ya CCM ni jambo lisilowezekana, labda waondoke na mkuu wa kaya.

Huku EL akionekana kujizatiti kwa ajili ya uchaguzi wa Raisi 2015, kambi yake ya fedha ikiongozwa na maney maker iko sawa sawa kuhakikisha kijana wao waliompachika pale wizara ya Nishati na madini anahakikisha umeme hauwaki ili waendelee kupata deal la kuwauzia watanzania umeme kwa kupitia makampuni yao kadhaa ya mfukoni.

Nawatakia wana CCM usingizi mwema , na Nape namtakia kazi njema ya kuwalaghai Watanzania. Mapacha ndio roho ya CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom