Nape shughulikia redio zinazoajiri ma-MC wa kitchen party kuwa watangazaji

Kama ni kweli wanatukana mbona wanapata matangazo? Na tafsiri ya kupata matangazo ni kuwa na wasikilizaji.

Nadhani Tatizo sio vyombo vya habari, Tatizo kubwa ni aina ya jamii tuliyonayo.
 
Watangazaji wa Clouds wenye elimu wawili tu......utashangaa TCRA wakapiga kimya.
Weye Mzionist Watu wengi Kama wewe wanafikiri kila kitu lazima uwe Na shahada 1 mpaka 7.
Wote hao ni wasomi Lakini hawana ELIMU Au kwa Kiswahili fasaha
(Hekima) hekima ya babu Na bibi zetu ambao walikuwa hawana shahada ya vyuo vikuu. Wametusomesha kila kitu Leo hii wewe unaingia JF.
Kila biashara inataka faida Kama mtu Hana hiyo Elimu unayo itaka Lakini mbunifu Na hekima nampa kazi Na kampuni yangu ikafanikiwa sana tu
Fungua macho uone dunia inaendeshwa Na Watu wasio Na vyeti vya chuo.
 
dah hao wadada siijui wa mamahuwa siwapendi kinoma yani wanaongea shit kinoma mara mcharazo mara kuchambana ni umbea nakusutana sipend kusikiliza ila nna jirani yangu hapa uswahiln kama hajasikiliza hao wapuuz basi siku haijapita kabisa
 
Weye Mzionist Watu wengi Kama wewe wanafikiri kila kitu lazima uwe Na shahada 1 mpaka 7.
Wote hao ni wasomi Lakini hawana ELIMU Au kwa Kiswahili fasaha
(Hekima) hekima ya babu Na bibi zetu ambao walikuwa hawana shahada ya vyuo vikuu. Wametusomesha kila kitu Leo hii wewe unaingia JF.
Kila biashara inataka faida Kama mtu Hana hiyo Elimu unayo itaka Lakini mbunifu Na hekima nampa kazi Na kampuni yangu ikafanikiwa sana tu
Fungua macho uone dunia inaendeshwa Na Watu wasio Na vyeti vya chuo.
Ubunifu sio kuongea upuuzi we mgogo...kwanini radio za wanaojali taaluma hawanaga upuuzi?? Jitu kilaza litajuaje somo la maadili ya utangazaji...asilimia kubwa pale ni watu wa mitaani tu wanabrainwash vijana wetu....ngoja niingie tcra, nitahakikisha kunakua na sheria kabisa kikomo cha elimu kwa watangazaji maana ndio wanaoharibu taifa.
 
Hivyo vipindi kimaudhui si ngono,ni mafunzo ya kawaida kwa wote,ukichunguza viliigwa toka kwa makungwi na wafundaji,usiku utamtangazia nani biashara?Mchana kuna wasikilizaji wengi.
 
Vipindi hivi ukichunguza hurushwa kati ya saa 5 na 6 adhuhuri na huambatana na burudani pamoja na matangazo ya biashara,kimsingi hufundisha kujiweka safi, ni kama vinakumbushia mambo ya kawaida na ni kipengele tu katika kipindi husika,huwezi kukirusha usiku,kwani walengwa wengi watakuwa wamelala, vya usiku vipo vinazungumzia mahusiano zaidi.
 
Usemavyo ni sawa lakini wanatakiwa kuongea kwa kuzingatia wanasikilizwa na watu wa rika zote. Tatizo hapa wanaongea kama wanamfunda bi harusi. Hao watangazaji uelewa mdogo...
 
Ubunifu sio kuongea upuuzi we mgogo...kwanini radio za wanaojali taaluma hawanaga upuuzi?? Jitu kilaza litajuaje somo la maadili ya utangazaji...asilimia kubwa pale ni watu wa mitaani tu wanabrainwash vijana wetu....ngoja niingie tcra, nitahakikisha kunakua na sheria kabisa kikomo cha elimu kwa watangazaji maana ndio wanaoharibu taifa.
Mkuu wewe umekazania kikomo cha Elimu.Hii nchi imeteketezwa Na hao wasomi unao waabudu.Wasomi wengi Kama ndio wanatuharibia dunia hii.
Tunahitaji wasomi Au sio wasomi wenye hekima.
Wewe unafikiri watumishi TCRA hawana hekima Kama wewe.
Kwa sababu wewe hupendi hayo sio wote hawapendi Na sababu unaona hiyo radio Ina wadhamini wengi sana.
Kalage baho Na Ubozo wako.
 
Kuna kiredio huku kwetu Mtwara, kinaitwa redio Newala, kuna watangazaji maboya sana, kuna mdada anaitwa Selister Emmanuel, mtangazaji huyu anaharibu radha ya kusikiliza hii redio. Mtangazaji anatumia nguvu katika kutangaza utafikiri yupo kwenye mashindano ya kupiga domo. Hizi ajira siku hizi kwa upande wa redio zimekuwa za kijinga jinga sana hazifuati taratibu, wala hazizingatii maadili.
Hahahaa
 
vipindi vyangu vya radio ni BBC (dira/amka) na magazeti basi uwa sivumilii huo upuuzi
 
Hasa limeibuka wimbi la vipindi vya redio nyingi vinavyo anza SAA NNE hivi watangazaji wake in hatari ,maneno wanayapolomoa tu, afu mixture taarabu! hawachagui cha kuongea,wanaboa sanaa
Vinaitwa
Leo tena
Yaliyomo yamo
Barizi la kokoni
 
Vipindi hivi ukichunguza hurushwa kati ya saa 5 na 6 adhuhuri na huambatana na burudani pamoja na matangazo ya biashara,kimsingi hufundisha kujiweka safi, ni kama vinakumbushia mambo ya kawaida na ni kipengele tu katika kipindi husika,huwezi kukirusha usiku,kwani walengwa wengi watakuwa wamelala, vya usiku vipo vinazungumzia mahusiano zaidi.
Wewe nawe ni wale wale, Mpwani, kutukana mbele ya wanao si tatizo. Yani huoni tatizo na vipindi hivyo
 
Haaaaa kwani kuna ubaya gani? Hao wake zenu mnataka wafundwe na manyakanga tu na masomo? Mwanamke mazngira,mwanamke usafi
Mwanamke mchafu akosa mme
Na mme mchafu akosa mke
Siku hizi tunaambiana live bila chenga
 
Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.

Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.

Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.

Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.
Mkuu kuna vitu sijavielewa kwenye uzi wako shida ni ma-Mc kuwa watangazaji au vipindi hivyo unavyoviongelea kuruka muda ambao ww unaona haufai?kama vingerushwa muda unaoona ww mzuri sifa ya hao watangazaji ingekuwa sawa kwako?mtangazaji anapangiwa kipindi muda fulani na uongozi ndiyo unaopanga hivyo vipindi na mtangazaji anakuwa host tu,nafikiri hukujipanga kujua ni nani unayetaka kumlaumu kati ya radio,mtangazaji au muandaaji wa kipindi.
 
Kuna kipindi TV1 single lady cha kutafta mabwana na wanawake wa kulala nao .Kina rushwa mapema mno
Mkuu kumbe nawe umekiona hcho? Yani juz ilikuwa pata shika jirani yangu kawanyuka watoto bakora coz wanang'ang'ania aweke hyo station jamaa baada ya kufuatilia maudhui ya kipndi akagundua ni uchafu mtupu acha atembeze bakora
My take, kipindi hcho bora kifutwe hakina maadili ya kitanzania kabisa, mimi sioni utofauti na dangulo pale wanazana legally, ni uchafu mtupu... Kinaitwa mchezo wa karata
 
Back
Top Bottom