Nape shughulikia redio zinazoajiri ma-MC wa kitchen party kuwa watangazaji

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,664
1,565
Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.

Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.

Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.

Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.
 
nilisikia kipindi hicho nikiwa kwenye basi toka Moro to Dar leo. kweli waliboa sana hawa wadada
Wanaboa sana, watangazaji wanahisi kuongea habari za kiswahili swahili ndiyo utangazaji siku hizi
 
Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.

Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.

Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.

Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.
Hawezi kuigusa Radio ya Pombe hiyo anasikiliza muda wote Ikulu na amevisifia hivyo vipindi kwa kupiga Simu kabisa.
 
Kipindi kama hicho ukiwa na wanao ndio unaomba ardhi ipasuke ujifiche
Mkuu ni shida,kwa kweli hasa ukiwa na watoto au wakwe kwa kweli unatamani ardhi ikumeze mpaka watakapomalza ndipo urudi tena.
Serika watusaidie hili.
 
Clouds imepanda chati kwa mambo makubwa mawili. Djs wakali na watangazaji wabunifu. Kwao issue sio cheti bali kipaji na ubunifu. wakianza kukagua elimu clouds na Efm watakuwa wa kwanza kupotea kwenye ramani.
Hii redio Ya matangazo sio?
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom