Nape shughulikia redio zinazoajiri ma-MC wa kitchen party kuwa watangazaji

Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.

Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.

Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.

Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.
Nina Imani Nape anasoma hizi comments, true dat
 
Watangazaji wa Clouds wenye elimu wawili tu......utashangaa TCRA wakapiga kimya.
 
v
Naunga Mkono Hoja, sasa hivi hizi radio zimekuwa jehanam ya kuharibu vijana, yaani hakuna maadili ni upuuzi mtupu unaozungumzwa na mashangingi yaliyo kubuhu ndiyo wamegeuka watangazaji!

Haswaa.............! kwa Clouds sijui hawa watangazaji huwa wanawatoa wapi? maana hawana maadili ya ki-Tz kabisaaaa!
 
Hata kwenye tv, maadili hakuna, mtangazaji alivyovaa Mungu mwenyewe ndiyo anajua
 
Kuna kiredio huku kwetu Mtwara, kinaitwa redio Newala, kuna watangazaji maboya sana, kuna mdada anaitwa Selister Emmanuel, mtangazaji huyu anaharibu radha ya kusikiliza hii redio. Mtangazaji anatumia nguvu katika kutangaza utafikiri yupo kwenye mashindano ya kupiga domo. Hizi ajira siku hizi kwa upande wa redio zimekuwa za kijinga jinga sana hazifuati taratibu, wala hazizingatii maadili.
 
Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.

Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.

Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.

Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.

Hivi vipindi vipo vingi mno kwenye radio na TV Staions nyingi tu hata mimi binafsi nimewahi kupost hoja kama hii baada ya kukerwa na maneno ktk kipindi cha TV kinachorusha saa moja jioni kikiongelea mahusiano, namna sijui kuishi na mme mke nini cha kufanya, Nikahoji mtoto wangu wa miaka nane, saba, sita, anahaja gani kujifunza maisha kuishi na mke au mme? wengi walinisapoti na wachache wakaniita mkosaji.

Ukweli kuna vipindi havina tija redioni ama kwenye kwa kuwa vinarushwa muda usio sahihi.
 
Clouds imepanda chati kwa mambo makubwa mawili. Djs wakali na watangazaji wabunifu. Kwao issue sio cheti bali kipaji na ubunifu. wakianza kukagua elimu clouds na Efm watakuwa wa kwanza kupotea kwenye ramani.
Sheria zinasemaje? Kipaji, Elimu au vyote?
 
Kuna kipindi TV1 single lady cha kutafta mabwana na wanawake wa kulala nao .Kina rushwa mapema mno
 
Kuna siku nami nilipita njia ya singida kuna karedio hapo singida nako ni noma kanaitwa ...... Ninoma kunademu limefyatuka na manjemba yanaigiza kama yamezaliwa pwani yaani ni kero mada zao maadili ziroziro mnauye fuatilia ukatumbue hako karedio wanyaturu wataharibikiwa watoto
 
Huu ndiyo Uhuru wa habari maana wakifungiwa tutalalamika kuwa Uhuru wa habari unakandamizwa.
 
Naunga Mkono Hoja, sasa hivi hizi radio zimekuwa jehanam ya kuharibu vijana, yaani hakuna maadili ni upuuzi mtupu unaozungumzwa na mashangingi yaliyo kubuhu ndiyo wamegeuka watangazaji!
Huo ulio zungumzwa sio maadili mabaya ila wakati wa hayo mazungumzo.Watu wengi hawajui usafi wa mwili ni darasa la bure hata kwako.Au walikuongelea wewe?
 
Back
Top Bottom