benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa nchini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.
Nape amesema kuwa Rais Samia alipowaapisha Viongozi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji amewataka Viongozi hao wawasikilize wakosoaji wote na ikiwezekana wawajumuishe kwenye michakato mbalimbali ya kuboresha mambo mbalimbali katika nchi yetu na kusema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutumia lugha zisizofaa wanapotoa maoni yao sio sawa.
“Tukosoane, turekebishe, tutoe maoni bila ya kutukanana. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerer alitufundisha tukosoane kwa hoja bila ya kutukanana. Kosoeni, toeni maoni, msidhalilishane na wala msitukanane na hasa inapokuwa ni Rais wa Nchi yetu mana yeye ni sura yetu sote”. Amesema Nape
“Kutukanwa kwa Mama ni kosa na hata kama hajakuzaa moja kwa moja unapomtukana basi ni sawa na kutukanwa kwa wazaza wote, tunao wajibu wa kuwaadhibu wote wanaotukana wazazi wa Nchi hii, kwani wazazi hawa wametulea, wametutunza, wametufikisha hapa tulipo salama na tusisahau kuwa utamaduni wa nchi yetu ni kuheshimiana” Ameongeza Waziri Nape.
Waziri Nape pia amempongeza Rais Samia kwa nia yake ya dhati kutaka kuona haki ikitendeka nchini na kusema kuwa mageuzi anayofanya katika kuboresha na kukusanya maoni ya watanzania kuhusu maboresho ya taasisi zinatoa haki nchini.
“Tunaposhuhulika na Haki Jinai, moyo wa Rais unataka haki. Haki italiinua Taifa letu,” amesema Nape.