Nape Nnauye na John Mnyika yupi mwanasisa bora kwa 2012?

Nani kati ya wawili hawa anastahili kuwa mwanasiasa bora 2012?

  • Nape Nnauye

    Votes: 9 3.5%
  • John Mnyika

    Votes: 251 96.5%

  • Total voters
    260
  • Poll closed .
Hapa naona mnataka kufananisha maji na mafuta.
Chadema nzima inapambana na NAPE mmoja huu ni uthibitisho tosha kuwa Nape ni jembe.

hapa tunapiga kura kamanda hatushindani na mtu na mwenye kura nyingi za yes ndiye atakayekua mshindi
 
Mbona jibu ni rahisi sana, ni nani kati ya hao anawakilisha wananchi bungeni? So this doesn't need poll hata kidogo, bora ungesema kati ya John Mnyika na hata Aden Rage mbunge wa Tabora mjini
 
J.J Mnyika,he is great guy.
Mchumia tumbo nape mnamuonea sana,endelea kulea kitambi na kubwabwaja bwana nape.
 
Nyie acheni kumpandisha joto Nape!! Mtamfanya afungue account mia ili ajipigie kura kuonyesha kuwa CCM bado ina mvuto!!!
 
Unawez kukuta hata NAPE naye kampigia MNYIKA kura maana jamaa huwa hata yeye hajikubali kubali.......
 
Mnyika bado mtoto mchanga. Kila akiongea pumba kila akichangia bungeni utatamani uingie uvunguni. Mlisikia kituko chake jana? Huyu ni kiongozi aliyekula kiapo anaongoza kwa kushabikia utoto wa kisiasa. Yule mlemav wa arusha goodbye lema alimtafuta chokoraa arusha na kumvalisha nguo za alishababu na kujidai eti ni mpiganaji wa jwtz lakini hata kikosi chake akifahamu. Halafu mnyika akadakia na kuunga mkono huo utoto na kuhusisha na mambo ya meremeta???? Yeye huyu aliwahi kumkashifu mheshimiwa rais na kumuita dhaifu wakati huyu mnyiku tangu achaguliwe ubungo hajawahi kufanya lolote zaidi ya kufungua matawi kwenye vijiwe vya wahuni. Sasa 2015 atapimana ubavu na jembe nape mnauye.
 
Wapiga kura wanafahamika jf ina wenyewe. Ni wale wale ndo maana walijitia kupiga kura ya slaa na zitto lakini ukweli utabaki ni ukweli huwezi kulazimisha. Chadema inakufa na hii ni dalili ya kurusha miguu kabla israeli ajawapumzisha kwa nccr na tlp. Hahahahahaha
 
Mbona ndie ktibu uenezi? au mlikua mmechanganyikiwa wakati mnampa huo wadhifa
Hili swali ungewauliza akina Lowasa na wenzake, ila nahisi alipewa kanafasi hako ili kumziba mdomo baada ya kutaka kuwaumbua kwenye ule utapeli uliofanyika kwenye ujenzi wa Jengo la vijana.
 
Nape ashindanishwe na Hawa Ng'umbi, wote waligombea ubunge 2010 kupitia CCM kabla ya mchujo wa kichama
 
Hivi Nape Nauye si ndie jana amekimbia Mdahalo na Yericko Nyerere?

Kama huyo Nape alikimbia mdahalo na mtu ambae hata siasa haijui utamlinganisheje na Mnyika?

Ni kumdharirisha tu mwanasiasa makini Mnyika
 
Back
Top Bottom