butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,320
- 7,381
Si alikuwa anasifiwa juzi tu!Nape strikes again.
Ukishaonja kula nyama za watu, kamwe hutoacha.
Yuleyule aliyetuondolea bunge live wakati huo akiwa waziri wa habari kipindi cha utawala wa Magufuli, Leo tena akiwa na dhamana hiyohiyo ya Waziri wa habari ameufungia kimyakimya mtandao maarufu wa Clubhouse.
Mtandao wa Clubhouse, ni mtandao ambapo watu popote pale walipo duniani huingia kujadiliana vitu mbalimbali kwa Sauti. Kupitia mtandao huu watu hujadili mada mbalimbali za maisha yao, ikiwemo uchumi, mambo ya kijamii, siasa n.k Nape mwenyewe ashaalikwa katika mada mojawapo kujadili ishu za anwani makazi.
Kutokana na elimu ya kuwaamsha watu na maarifa makubwa ambayo watanzania wamekuwa wakipata kupitia mtandao huo, serikali ya CCM imeona ni tishio kwao. Sasa Nape kama kawaida yake kaufungia mtandao huu ili Watanzania waendelee kuwa gizani.
Nape alipofungia bunge live wananchi walimlaani sana, baadae alipowekwa nje ya madaraka na JPM alikiri kuwa anajuta kushiriki maamuzi yale ya kufungia bunge Live. Leo Nape karudi madarakani kafungia tena mtandao wa Clubhouse ili Watanzania wasiweze kucongregate na kujadili mambo muhimu ya nchi yao.
Tukumbuke Nape huyuhuyu ndo alikuwa kinara wa kutetea sheria kandamizi ya vyombo vya habari wakati alipokuwa waziri wa habari kipindi cha JPM.
Tunamtaka Nape na TCRA, wafungulie mara moja mtandao wa clubhouse. Haiwezekani Rais Samia anasema kuwa anataka kuifungua nchi, na uhuru wa maoni uwepo, na kukosoa utawala wake ruksa, halafu anakuja Waziri kimyakimya bila kuutarifu Umma anafungia mitandao.
Kwa hivi sasa bila kuwasha VPN huwezi kuupata mtandao huu kwa sababu Nape Nnauye kaufungia.
Huyu Nape anajisahau sana, hii mitandao anayoiona ni mibaya ndiyo hiyohiyo iliyokuwa sauti ya pekee kumtetea kipindi kile katolewa bunduki njenje. Hivi huwa hawajifunzi kitu hawa?