Nape: CHADEMA wamepanga kufanya fujo mkutano wao Morogoro

Duh!! Chama Kimewekwa rehani kwenye Mikono ya Mwigulu, Nape na Lusinde!! Duh Maskini nchi yangu!!
 
Kama umeangalia vyombo vya habari, NAPE kasema kapata taarifa kuwa CHADEMA wamepanga kufanya fujo kwenye nkutano wao wenyewe morogoro mjini. Swala la kujiuliza, inawezekana kweli mkafanya fujo kwenye mkutano wenu wenyewe kama kweli siyo vichaa. NAPE are you serious with this?.

Leo Mapema Dk Slaa alisema kuwa CCM wametuma vijana kati ya 10-20 ili wafanye fujo kwenye mkutano wa CHADEMA huku wakiwa wamevaa magwanda yanayofanana na ya CHADEMA ili ionekane ni CHADEMA wamehusika. Kwa haya maneno ya NAPE inaonekana intelijensia ya CHADEMA iko makini

Wewe nawe unafikiri kwa kutumia (ban) huwezi ona nani mkweli hapo CCM ni chama Dume hakiwezi salandia mikutano ya mabinti CDM
 
Nepi ya mavi ni bonge la tahira hacha wamtumie vibaya mkama anajifacha kasoma alama za nyakati,anajua mwisho wake ngoja yeye mwisho wake atauona sijawai kijana primitive kama nape anadhani siasa za propaganda zitaiokoa ccm dokta slaa huwa haropoki ******we na ukoo wako nape.

Magamba wanafanya uchaguzi mwaka huu, na tunategemea nape asiwemo kwenye sekretatriete ijayo, nafasi zote za wakuu wa wilaya zimejazwa, baada ya uchaguzi chama kitashikwa na Lowasa, Rostam, chenge na wapambe wao, je Nepi hiyo ya mavi ina pa kutokea?
 
Tatizo la Nape ana nidhamu ya uoga, huruka yakujimendekeza na kimbelembele, jambo hilo litakuja kumgharimu siku moja,mara apatapo jambo hatulii,anakurupuka tu kujibu kama ngonjera vile.

Kijana,uwe unatuliza akili,mawazo nakutafakari hoja kabla ya kujibu.Watu wanataka ukanushe mambo kwa facts,siyo blaablaa kama vile kusema DK SLAA anazeeka vibaya,jenga hoja na vigezo kukanusha tuhuma,watanzania siyo watu mbumbu bwana,ulisoma wapi wewe?
 
nape bana,sijui akiri yake inauvundo?? kweli itakuwa wanjitengenezea fujo ndio maana singida alikufa kada wa ccm.
nape kaoshe akiri yako inaumande.
 
Magamba wanafanya uchaguzi mwaka huu, na tunategemea nape asiwemo kwenye sekretatriete ijayo, nafasi zote za wakuu wa wilaya zimejazwa, baada ya uchaguzi chama kitashikwa na Lowasa, Rostam, chenge na wapambe wao, je Nepi hiyo ya mavi ina pa kutokea?
inaonekana unamuogopa sana Nape, amewashika pabaya CDM, na bado, utatukana mpaka utakula ban.
 
Nape ni zaidi ya janga, ni tishio kwa usalama wa Taifa.
 
Duuuu kaaazi kweli kweli, Kila Track itakayotoka lazima Nape awepo najiuliza kazi yake kama CDM wasingekuwepo daaa
 
Leo yametimia yale yaliyokuwa yakisemwa kuwa CCM wamejipanga kufanya vurugu kwenye mkutano wa leo wa CHADEMA.
 
Ila kazi ya Nape ni ngumu jamani. Kazi ya kuzibua choo cha CCM ambayo inavimbiwa kila siku si kazi rahisi kabisa. Hizo harufu za kila kila siku si lazima uchanganyikiwe tu
 
Napeee ndio mwisho wa Akili yake jamani ila itabaki kuwa Akili za ccm ndio upumbavu wa CDM usiku mwema Tehe Tehe Tehe
 
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, umeibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

Akizungumza kwa njia ya simu jana Kamanda Shilogile, alisema kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine.

Shilogile, alisema wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

“Tumewaambia viongozi wao watapanda magari lakini wananchi watafute njia ya kufika huko na si kwa maandamano hilo hatuwezi kuruhusu,” alisema.

Alipoulizwa makubaliano yaliyofikiwa awali baina yao na Chadema juu ya kupanga njia ya kupita kwa maandamano hayo, Shilogile alisema hakukuwa na makubaliano.

Kwa Upande wake, Kigaila alisema wanachojua wao ni kwamba mikutano yao ipo kisheria na kwamba wametoa taarifa polisi kama inavyotakiwa hata kufikia hatua ya kukubaliana kwenda kupanga njia ya kupita.

Alisema sababu alizotoa Shilogile hazina mashiko kwa kuwa barabara za Morogoro ni sawa na za miji mingine na kwamba ndani ya Mkoa huo kulifanyika maandamano mengine tofauti na ya Chadema.

“Sisi tutafanya maandamano huyo kamanda awepo asiwepo, alie au acheke kwa sababu tuliacha tarehe nne kwa kuwa walitueleza kuwa kuna shughuli zitaingiliana leo hoja anazotoa hazina msingi,” alisema Kigaila.

Wakati huo huo; Chadema kimetoa siku saba kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kukiomba radhi chama hicho pamoja na kutoa faini ya Shilingi bilioni tatu.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Mnyika alisema Chadema imefikia uamuzi huo kufuatia taarifa ya Nape aliyoitoa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni, kwamba chama hicho kimekuwa kikichangisha fedha kwa wananchi katika mikutano yao kama geresha ya kuhalalisha fedha kinazopokea kutoka nje ya nchi.

“Chadema kimeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Nape, kufuatia madai ya uzushi na uongo aliyoyatoa Agosti 12, mwaka huu, kuwa anao ushahidi kwamba chama kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kwa wafadhili kutoka nje,” alisema.

Aliongeza, “Izingatiwe kuwa matamshi yake yalitangazwa na vyombo vya habari vya kielektroniki ikiwemo vituo vya televisheni, radio na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na kutolewa katika kurasa za mbele za magazeti mbalimbali Agosti 13, mwaka huu.”

Mnyika alisema kufuatia tuhuma hizo, bodi ya wadhamini wa Chadema iliagiza wanasheria wamwandikie barua ya kumtaka kukiomba radhi chama, kwa kutumia njia ile ile aliyotumia kukashifu na kukifitinisha kwa Watanzania, ikiwemo kuzusha kwamba upo uwezekano wa chama hicho kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani.

“Tayari Nape ameandikiwa barua ya kisheria tangu Agosti 24, ya kumtaka aombe radhi na kulipa fidia ya Sh. bilioni tatu kwa matamshi hayo ya uzushi na uongo yenye maana ya kuwapotosha waliyoyasikia na kuyasoma, kwamba Chadema kinawalaghai wananchi, kina viongozi wasio waaminifu na kwamba kiko tayari kuuza nchi kwa uroho wa madaraka,” alisema.

Mnyika alisema kipaumbele cha chadema katika suala hilo ni kuombwa radhi na kwamba kiwango cha fidia ya fedha ni kwa ajili ya fedheha na fundisho kwa kitendo cha uzushi na uongo kilichotolewa na kiongozi huyo.

“Katika kauli yangu ya awali nilitoa wito kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kueleza Watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake, hivyo ukimya wake mpaka sasa kuhusu matamshi hayo inakifanya Chadema kuwa na imani yenye shaka kwamba Nape hakutumwa na chama chake kutoa matamshi aliyoyatoa,” alieleza.

Mnyika alisema endapo Nape atashindwa kutekeleza agizo ndani ya siku alizopewa, watamfikisha mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

NIPASHE ilipomtafuta Nape kuzungumzia juu ya suala hilo, alisema atatoa majibu leo kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Imeandikwa na Elizabeth Zaya na Nuru Mfaume, Dar.





CHANZO: NIPASHE

 
....Amewaomba polisi wamuombe Dr Slaa ushahidi kuwa CCM wameingiza silaha kwa ajili ya vijana wao waliopo makambini, akiri kuwa uwa CCM uwa wanawaweka vijana makambini kujadili mambo mbalimbali.

....Asema CHADEMA wamepanga kujifanyia fujo kwenye mkutano wao utakaofanyika Morogoro mjini.

My take:

Hivi itawezekanaje wewe kujifanyia fujo kwenye mkutano wako mwenyewe?

Source: ITV
Kwa kauli hii ya NEPI kwa yaliyotokea leo 27.08.2012 Moro yalipangwa na CCM kwani hawa jamaa huwa hawawezi kukaa na kitu moyoni ndo maana akaropoka akimaanisha fujo zitatokea.
 
Back
Top Bottom