Nape awajibu CHADEMA, asema siku saba ni nyingi mno!

dar tu serikali ya magamba imeshindwa kupeleka vifaa vya sensa KATA YA BUNJU makarani wamekaa wanasubiri madodoso. Na huko mikoani ndo ikoje. haya ndo mambo ya kuita wanahabari cio hiyo hoja ya NAPE.
.
Mkuu hapo penye red hata huku mikoani makarani wanakaa tu hawana madodoso, penseli, mabegi n.k... Cha ajabu TBC nimeshangaa eti zoezi linaendelea vizuri. Kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza...!
 
KOMRAD NAPE LIVE NA WANAHABARI MUDA HUU CCM LUMUMBA K/KOO. AWAJIBU CHADEMA..

."..siku saba walizonipa nyingi sana,ushahidi upo kwa kila nachosema...waende mahakamani leo wasisubiri siku saba....wakati huo huo wamsaidie mzee Slaa kuja na ushahidi mahakamani wakusema CCM IMEINGIZA SILAHA,TUNATAKA AJE AOMBE RADHI kwa njia ile ile na tutadai fidia bilion 3, na tayari wanasheria wameshaanza hatua"
ASANTENI.

My take.siasa ya tanzania imeharibika,kila mtu ni mbabe,wanaoumia ni wananchi.
noting constructive will come from nape's lips
 
Nape ameishiwa sana tunamwomba ajibu hoja za msingi asijaribu kukwepa ukweli.
 
Wakutane mahakamani

Hivi ndo mnasema NApi ni Mkuu wa wilaya gani vile?
ana pata wapi muda wa kuwahudumia wananchi?
 
Jumanne, Agosti 28, 2012 05:51 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

nape.jpg
Nape Nnauye

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema hatakiomba radhi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kutokana na hali hiyo, amesema CHADEMA wanaweza kwenda mahakamani kama wakitaka kwa kuwa tuhuma alizotoa dhidi ya chama hicho ni za kweli.

Nape aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli iliyotolewa juzi na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kwamba Nape anatakiwa kuiomba radhi CHADEMA kutokana na kauli yake aliyoitoa kwamba, chama hicho cha upinzani kinafadhiliwa mabilioni ya shilingi na wafadhili kutoka nje ya nchi.

Katika mkutano huo, Nape alisema hawezi kuwaomba radhi CHADEMA na kwamba yuko tayari kuburuzwa mahakamani ili akatoe ushahidi wa kile alichosema.

"Mtu mzima hatishiwi nyau, katika hili wala wasisubiri kupoteza muda, hata leo waende mahakamani nitakutana nao huko.

"Ila ninachowatahadharisha ni kwamba, nao wamwambie babu yao Dk. Slaa, ajiandae na ushahidi dhidi ya kukishutumu Chama Cha Mapinduzi kuingiza silaha kinyemela nchini.

"Kama hatafanya hivyo ndani ya siku saba kuanzia sasa, tutamburuza mahakamani na tunamtaka kulipa fidia ya Sh bilioni 3 na Sh 1.

"Hivi sasa tayari chama kimewaagiza wanasheria wa chama ambao wanaandaa barua ya kisheria, ili kumpelekea Dk. Slaa ili aweze kuthibitisha madai yake haya.

"Kwa hatua hii ni dhahiri sasa CHADEMA, wameshindwa kufanya kazi ya siasa na wamejigeuza waratibu kwa kufanya utabiri, eti wanahoji kauli niliyotoa ni yangu au chama hali ya kuwa mimi ndiye msemaji wa chama.

"Wanamtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa atoe kauli juu ya tamko la chama chetu dhidi yao, hakika hawana jipya na wanatafuta kwa kutokea kisiasa nasi CCM tumejipanga kuwatumikia Watanzania," alisema Nape.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alisema chama chake hakina haja ya kutoa ushahidi hivi sasa, bali kitatoa ushahidi huo mahakamani, ambapo pia ikithibitika kuwa Chadema kweli imeingiza fedha kutoka nje kitambue kuwa sheria ya vyama vya siasa inapinga na kitendo hicho kitakiingiza chama hicho matatani.

Juzi Chadema kilisema kitamburuza Nape mahakamani.

Akitangaza uamuzi wa bodi ya wadhamini wa chama hicho, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema Nape atafikishwa mahakamani baada ya kukituhumu kinapokea mabilioni ya fedha za misaada kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi.

Agosti 12, mwaka huu, Nape inadaiwa alisema Chadema inapokea misaada ya fedha kutoka kwa wafadhili walioko nje ya nchi.

Kauli hiyo inaelezwa kuwa ilitangazwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Agosti 24, mwaka huu wanasheria wa CHADEMA walimwandikia barua Nape na kumtaka kuomba radhi ndani ya siku saba kwa uzito ule ule kupitia vyombo vya habari na kulipa fidia ya Sh bilioni tatu kutokana na kusema uongo.

MTANZANIA ilipomtafuta Mnyika alisema Nape alitakiwa kujibu hoja na si kupotosha.

"Nape na CCM wajibu hoja kwa kuwa Dk. Slaa, alitaja hadi namba ya silaha na CCM na ilipaswa kueleza ziliingiaje. CCM huwa inatoa madai dhidi ya CHADEMA ya uongo ila hukumu ya kesi ya Igunga ilithibitisha uongo wao," alisema Mnyika.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
hana hoja nape huyo ni kelele tu nyingi xo sipotezi muda muda kumjadili
 
Baada ya CHADEMA kumtaka Nape Nnauye kukiomba radhi chama na kukilipa fidia ya shilingi Bilioni 3 kwa kukidhalilisha kutokana na madai yake kwamba CDM kinapokea mabilioni ya fedha kutoka nje ya nchi lakini kuwachangisha fedha Watanzania kama danganya toto Nape ameibuka na kudai kuwa hayuko tayari kuomba radhi.

Bwana Nape kama kawaida yake ya uropakaji wa maneno aliwaambia CHADEMA kuwa wawahi Mahakamani kwa kuwa ana ushahidi wa uhakika na kile alichokisema.Alienda mbali zaidi na kusema kuwa mtu mzima hatishiwi nyau hivo basi CDM wawahi Mahakamani hata kama ni leo maana siku 7 walizompa ni nyingi na tuko tayari kukutana nao Mahakamani.

Kama hiyo haitoshi akaleta madai ya kitoto eti kuwa na yeye anawataka CHADEMA wathibitishe madai yaliyotolewa na Dr. Slaa kuwa CCM wameingiza kontena la silaha au waombe radhi kwa CCM na walipe Shilingi Bilioni 3 na shilingi 1! Kama ungemsikia Nape wakti anaongea na media ndipo ungejua huyu jamaa ni hamnazo na limbukeni wa siasa! Maneno kama eti siasa ni mchezo wa ajabu, CHADEMA wamwembie BABU yao alete ushahidi kwangu ni maneno ya mtu kebehi na dharau. Huwezi kumwita Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani ati ni babu wala huwezi kusema siasa ni mchezo wa ajabu. Kwake Nape anafikiri siasa ni mchezo kweli? Anathubutuje kumwita Dr. Slaa kama Babu kama siyo ukosefu wa adabu? Kikwete na Dr. Slaa ni nani babu wa mwenzake?

Hii inaonyesha tu Nape ni mtu wa aina gani! Huyu mwisho wake ni kuua CCM. Time gonna tell>
 
Sijaona kosa la Nape kwenye hili alichowaambia cdm ni ukweli mtu. Hebu tujiulize, kweli Slaa sio babu ? Slaa ana ujana gani wakuitwa kijana ? mie naona amempa heshima zaidi Slaa kwa kutambua umri wake na kuwa ni mkubwa kwake. CDM Nape hawalazi usingizi kila siku huyu jamaa CDM mnahangaika nae, na yeye yuko 1, nyie mko zaidi 50, na bado hamumuwezi, kubalini tu huyu jamaa amewazidi kete ya kisiasa.

hili jitu ni pumbafu sana kwa kweli mimi binafsi namchukia huyu jamaa kwa matendo yake na ujinga alionao unawezaje kumuita kiongozi kwa maneno ya kijinga na kuudhi shule jamani zinasaiidia jamaa alikuwa kachoka akaamua atoke na jengo la umoja wa vijana ndio limefikisha hapo alipo ndio maana analeta dharau
 
KOMRAD NAPE LIVE NA WANAHABARI MUDA HUU CCM LUMUMBA K/KOO. AWAJIBU CHADEMA..

."..siku saba walizonipa nyingi sana,ushahidi upo kwa kila nachosema...waende mahakamani leo wasisubiri siku saba....wakati huo huo wamsaidie mzee Slaa kuja na ushahidi mahakamani wakusema CCM IMEINGIZA SILAHA,TUNATAKA AJE AOMBE RADHI kwa njia ile ile na tutadai fidia bilion 3, na tayari wanasheria wameshaanza hatua"
ASANTENI.

My take.siasa ya tanzania imeharibika,kila mtu ni mbabe,wanaoumia ni wananchi.
CCM kwa kuiga ni kiboko hata ID t2015ccm Umeiga ya T2015CDM wapuuzi wakubwa sana nyinyi hata ubunifu hamna

wewe umejiunga juzi acha kuiga
Join Date : 14th August 2012
Posts : 147
Rep Power : 332
Likes Received 20

Likes Given 20
 
mimi nadhani kuna siku ambayo nape atakuja kujutia maneno yake. hata hivyo maneno mengi iiiiiiiiiiiiiiiii. ushauri nape nadhani mengine tumia busara ya kukaa kimya
 
Na sasa! Huyu anaongea nini? Kama wao anahisi kuwa Dr Slaa aliwasingizia kuhusu kuingiza silaha nchini si wangekwenda Mahakamani tu? Kwa nini asubiri CDM wamtake aombe radhi ndo na yeye atishie kuwapeleka mahakamani! Yaani watu wengine unaweza kufikiri wamekua kumbe ndo baado watoto kabisa! Yaani yale yale ya enzi zile eti nikusemee umekula sukari naye anajibu na mimi nikusemee ulikula sukari! Kwa nini usiseme siku zote hizo? RA hakukosea kusema amechoshwa na siasa uchwara! Now I got what he meant!

naongezea kuwa, jamaa huwa anaongea with confidence, confidence yenyewe ya kujua kuna walinzi nyuma yake. hapo hajageuka kuangalia nyuma kama hao anaowafikiria kuwa wako nyuma yake, hawapo kabisaaaa! siku akigeuka akaona kuwa hawapo atazirai au kufa.
sio kwamba confidence yenyewe ina rationale, anaongea kama mwenye umri chini ya miaka 10, tena mtoto mwongo ambae hajajua wala kuupanga uongo. nampa pole zake mwe!
 
Mnampa kichwa sana kumjadili Nape humu, kichwa chake hakina akili yule dogo, yuko kama baba yake. Amesahau kuwa baba yake Mzee Nnauye alizikwa nyumbani kwa mzee Yusuph Makamba kwa sababu hakuwa hata na Nyumba ya maana ya kuzikwa. Nape Acha kuwa kama babako. Ushauri tu wa bure, ongeza busara kidogo we bw mdogo.

Sasa babake nape anahusikaje hapo,wewe unajua utazikwa wapi,nadhan kichwa chako ndo hakina akili
 
Back
Top Bottom