Nape awajibu CHADEMA, asema siku saba ni nyingi mno!

Hivi ukiwa mwana ccm ni lazima u act uchizi ama? Manake ukiangalia wana ccm wale ambao ndo figure ya chama kichwani(reasoning) ni weupee hakuna kitu hebu mwangalie mwigulu, cheki mukama, msikilze nape na kubwa lao jk..duh kwel dalil ya mvua

mkuu sio vizuri kutukana,hayo ni matumizi mabaya ya jukwaa.
 
Nape usichanganya mambo mawili hasa unapogusia masuala ya kisheria. Hoja iliyopo mbele yako kwasasa ni wewe kutoa uthibitisho pasi shaka kuwa CHADEMA wanapata mshiko toka nje. Suala la nyie kuwa mnaandaa janjaweeds kwenye makambi ya wananchi na mmeagiza silaha ni hoja nyingine na huenda mwendesha mashitaka wa serikali akaona haina tija na kuitupilia mbali kama alivyofanya kipindi mahita ni IGP mlivyomtuma na visu vyenye nembo ya CUF au umeshasahau?

Safi sana kugundua hili Nape asifanye watu watoto ana takiwa athibitishe madai yake kwanza ndio nae afungue kesi ya kutaka Dr athibitishe kauli yake!

Naona nape anajibu mambo kama watu wa mitaani wanavyo fanya!

Nape una haki ya kudai Dr athibitishe tuhuma zake lakini kwa sasa cdm wamekuwai na utatakiwa uthibitishe kauli yako ndio nawe udai dr slaa athibitishe.

Me naona anafanya mchezo wa watoto
 
Mwenye updates za hukumu ya Mch mtikila atujuze naona kimya!
 
Yataka ujasiri wa hali ya juu kwa KIJANA wa Kitanzania kushabikia CCM, kwa mazingira yalivyo sasa. Kama si fisadi mtegemewa, basi yuko njiani kupelekwa Mirembe.
 
Nape wacha kututia kichefuchefu kwa siasa za kitoto na kinafiki.Vyombo vya dola viko chini ya chama tawala CCM.

Nini kinawazuia kuchukua hatua kwa pesa chafu za CHADEMA kama ushahidi upo sambamba na suala lakujivua gamba, ushahidi upo mnawapa muda watu kujisalimisha badala ya kuchukua hatua mara moja.

Hivi tuna serikali na vyombo dola?Kwa kauli yako inamaanisha ya kua hatuna Rais,hatuna serikali na hatuna vyombo vya dola,kwani kama vipo vinategemea ridhaa ya watuhumiwa ili vichukue hatua.

Kama ilivyokua kwa mafisadi wa EPA wakati Mh.Rais alipowabembeleza kurudisha pesa ili wasamehewe,hii imekaaje,Nape kifo cha nyani(CCM)Miti yote huteleza.Nape inamaana ukiibiwa mkeo au mali zako utampa muda mwizi ajisalimishe?MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Nape umeshakaa kwenye kona mbaya, nadhani waliokutuma kuusema mchemko ule, bado hawajakutuma uombe radhi! Una kila dalili za kuanza kuweweseka, unajua ulikosea, ila huuoni mlango wa kutokea! Ulikuwa wapi kutoa madai ya kumtaka Slaa kukanusha na kudai fidia?
Watoto wa mjini wanasema 'msala huo mwanangu', na imeshakula kwako!
Ni kweli mkuu, imekula kwake, hii nafasi ya Katibu mwenezi sijui ikoje ikoje hivi, aliyepita kabla ya Nape alikuwa balaaaa! na huyu pia Balaaaa! bo! labda wakifute tu hiki cheo, ni ushauri tu kwa CCM.
 
Mnampa kichwa sana kumjadili Nape humu, kichwa chake hakina akili yule dogo, yuko kama baba yake. Amesahau kuwa baba yake Mzee Nnauye alizikwa nyumbani kwa mzee Yusuph Makamba kwa sababu hakuwa hata na Nyumba ya maana ya kuzikwa. Nape Acha kuwa kama babako. Ushauri tu wa bure, ongeza busara kidogo we bw mdogo.

Wanajamiiforum, naomba tuwaheshimu wazee wetu Kama Nnauye, waliolitumikia taifa letu kwa uaminifu na uadilifu, kujilimbikizia Mali sio sofa Nouri sanaaa!,,!!!!
 
Wanajamiiforum, naomba tuwaheshimu wazee wetu Kama Nnauye, waliolitumikia taifa letu kwa uaminifu na uadilifu, kujilimbikizia Mali sio sofa Nouri sanaaa!,,!!!!
Mkuu achana na WANAFIKI wakubwa CHADEMA.
Mtu akitumikia Taifa kwa uaminifu wanamcheka, akiiba mdomo juu.
CDM pango la wahuni tu.
 
Greti Thinkaz mnanishangaza..ama ndio kusema hamkutegemea Nape ajibu alivyojibu..! Uwezo wa Nape kwenye siasa za Tanzania ndio ulipoishia, ni wazi viatu vya ukatibu mwenezi wa CCM Taifa alivyovaa vinambana!
 
Ccm hakuna kitu wanachoweza kukifanya bila kuongozwa na cdm wako km vipofu.
 
Nepi is fighting for his own survival maana Bw. wa magogoni akitoka tu, naye fadhila alizofanyiwa na mkulu zinafikia kikomo maana anasimama kwa Nguvu za mkulu, hana pumzi wala kibesi ndani ya Chama. Anapigania siku zake za mwisho katika siasa za kinafiki ndani ya Magamba.

"Asamehewe maana hajui alitendalo; alianza kwa majungu na fitina, atamaliza kwa majungu na fitina"
 
Hivi ukiwa mwana ccm ni lazima u act uchizi ama? Manake ukiangalia wana ccm wale ambao ndo figure ya chama kichwani(reasoning) ni weupee hakuna kitu hebu mwangalie mwigulu, cheki mukama, msikilze nape na kubwa lao jk..duh kwel dalil ya mvua
Umemaliza point zote! Teh teh teh!!!!!!!
 
jmn, tutulie tulii tuangalie muv inavyokwenda, hakuna haja ya kumwaga povu kwani mwisho wa ck ukweli utajulikana kuwa nani muongo na nani mkweli.
Duh, siasa ina vtk sana.
 
Back
Top Bottom