Nape asema CHADEMA ni chama cha Kigaidi

Waraka mlioandaa baada ya kuandaa mikakati ya mauaji; waraka mlioandaa kuhalalisha mauaji!!. Haitawasaidia! Damu ya watu inayomwagika itawahukumu.
Mungu mwenye haki anawajua wenye haki wake.
CCM die now; let my people live.

hIVI Tendwa yuko wapi kufuta hiki chama, chama kipya kiendwe kipambane na fisadi CCM. hivi ANPE HAJUI SHERIA MPAKA APAYUKE KWENYE MITANDAO?
 
Chadema ni chama rafiki wa renamo yale magaidi yaliyowaua wana msumbiji zaidi ya mamilioni na hata walishawahi kumtangazia baba wa taifa kati ya watu hatari wa kuuwawa. Sasa hapa tunapata picha gani?? Dhlakama ni swaiba wa chadema. Du ama kweli amani yetu iko tehani na hawa watu mungu atuepushe nao
 
Kwa kile kilichoonekana kuwa ni mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa Amani kunakoandamana na umwagaji wa damu ambako siku zote Chadema wamekuwa wakiyafanya, Nape awashukia na kusema kuwa chama chao kina mlegwa wa kigaidi.
matukio hayo ambayo yanazidi kshamiri siku hadi siku, yamekuwa yakifanywa na wafusi wa CHADEMA kwa amri ama maelekezo ya viongozi wao, kwa mfano; katika mkutano wa ndani wa viongozi wa chadema ambao ulipanga mkakati mpya wa kusabotage serikali iliofanyika nyumbani kwa Mbowe mikocheni pamoja na mambo mengine ulimuagiza Rwakatare kuelekea Iramba ili kuandaa kikosi kazi na kuendesha zoezi la kumchafua Mwigulu, Rwakatare alisafiri tarehe 11 kuelekea Singida kusimamia zoezi hilo ambalo tayari limeshasababisha maafa. Ambapo tayari wafuasi wa CCM na MWIGULU wameshapata madhira makubwa kwani Kijana mmoja wa CCM ameuawa na wengine ni majeruhi tangu kuanza kwa zoezi hilo chini ya Rwakatare.

Ifuatayo ni VIDEO ya NAPE akioanisha matukio ya CHADEMA na UGAIDI.

NNAUYE::CHAMA CHA KIGAIDI..................... - YouTube

Hakuna mtu awaye yote ccm anasimama jukwaani kunadi sera zake kwa wananchi! Hawasemi ni kwa nini Tanzania inazidi kuwa maskini? Kwanini mauaji ya wandishi wa habari, uhasama kati ya polisi na raia yanazid? Uhalifu unazid kila kukicha watu wanatekwa na kungo' olewa kucha bila nail cut na meno bila ganzi, polisi wanauwawa kwa kupigwa mawe, magorofa yanadondoka hovyo, migogoro ya ardhi imeshamiri kila kona ya nchi, watu wanatumia simu na mitandao ya kijamii kukashfu viongozi na migogoro ya kidini nani achinje na nani asichine inakuwa kwa kasi ya kutisha. Mauji ya viongozi wa kidini kumwagiwa tindikali na kupigwa risasi bila kosa lolote, makanisa kuchomwa moto nk. Haya yote ccm imeyafumbia macho na badala ya kukaa pamoja na kujadili hatma ya hili Taifa, wanasimam majukwaani kuviteta na kushtumu vyama vya siasa ambavyo havina dola wala serikali. Nape badala ya kuonesha kukomaa kisiasa katika kutafuta suluhisho kila siku amekuwa anasimama majukwaani na kuongea sera zisizo na mashiko ktk mustakabadhi wa taifa! Epuka umaarufu wa majukwaani unaovuma kama upepo uvumao toka mashariki unaishia magharibi, fanya kazi uliyopewa ya kuiokoa Tanzania na ufisad pia haya majanga haya
 
kumbe kuwa mwana haramu ni soo.hadi fikra.

Wakati cdm wanavyoonyesha kuwa wapo full digital.akina nape na ,akina mulugo na analogia nyingene za kizamani wanakimbizana na mavi ya fikra na ya keli kujipaka na kupaka wengine,wataishia kukimbiwa na watu kabla ya kuikuta cdm..Mulugo ana trademarks na patent za ukilaza nae yupo front ktk vita ambayo lissu ni mpiganaji.huu ni mzaha.Ccm hawana tofauti na kampuni ya vilaya yenye kila kitu ktk begi la documents.
 
Naona mumetengeneza kamuvi kafupi kakifara,magamba yote hayana akili mpaka mwenyekiti wao.
 
CCM waliwahi kusema CUF ni chama cha kigaidi.

Sasa wanasema CHADEMA ni chama cha kigaidi.

Ili kufikia hatua ya kuitwa chama cha kigaidi....CCM huanza na

CUF ni chama cha wapemba, baadae CUF ni chama cha kiislamu.

Ilisemwa CHADEMA ni chama cha wachaga, CHADEMA ni chama cha Kaskazini, CHADEMA ni chama cha kikristo.

Ilipofikia hatua ya CUF kuitwa Chama cha kigaidi lililofuatia ilikuwa ni mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi mkuu na uundwaji wa serikali ya Umoja wa kitaifa....Je historia itajirudia?
 
nape hajatuambia km wake zao cuf wameacha ugaidi na lini.
Hajatuambia marafiki zao sudan,libya,syria ,iran,north korea,pakirtani hadi wanapewa vibali ya kuiba faru wa msaada na tembo,km wameacha ugaidi. Na lini.
 
Kuna mbinu za kuingia Ikulu ambazo chadema waziiga na zinafanana na chama NAZI
Magwanda yanafanana
Kutia hofu
Utekaji
Kukata kucha watu
Kuifanya serikali iliyopo isitekeleze mambo yake
kuhutubia kwa njia ya kufoka foka
Kupotea watu mashuhuri
Haya yote yalifnywa na NAZI ya hitler hatimae yaliyo tokea tunayajua

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Lkn CCM kupitia kwa Mwigulub MB si wamekiri kuwa walifadhili ugaidi kwa kumpa Ludo hela?Sheria za ugaidi zinasema wazi kuwa aliyefadhili ugaidi nae ni gaidi!Kumkamata Ludo pekee kumuacha MFADHILI ni uonevu!
 
Kwa kile kilichoonekana kuwa ni mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa Amani kunakoandamana na umwagaji wa damu ambako siku zote Chadema wamekuwa wakiyafanya, Nape awashukia na kusema kuwa chama chao kina mlegwa wa kigaidi.
matukio hayo ambayo yanazidi kshamiri siku hadi siku, yamekuwa yakifanywa na wafusi wa CHADEMA kwa amri ama maelekezo ya viongozi wao, kwa mfano; katika mkutano wa ndani wa viongozi wa chadema ambao ulipanga mkakati mpya wa kusabotage serikali iliofanyika nyumbani kwa Mbowe mikocheni pamoja na mambo mengine ulimuagiza Rwakatare kuelekea Iramba ili kuandaa kikosi kazi na kuendesha zoezi la kumchafua Mwigulu, Rwakatare alisafiri tarehe 11 kuelekea Singida kusimamia zoezi hilo ambalo tayari limeshasababisha maafa. Ambapo tayari wafuasi wa CCM na MWIGULU wameshapata madhira makubwa kwani Kijana mmoja wa CCM ameuawa na wengine ni majeruhi tangu kuanza kwa zoezi hilo chini ya Rwakatare.

Ifuatayo ni VIDEO ya NAPE akioanisha matukio ya CHADEMA na UGAIDI.

NNAUYE::CHAMA CHA KIGAIDI..................... - YouTube

[h=2]CCM na CHADEMA: Je, ni wapinzani wanaofanana?[/h]
Jibu rahisi ni HAPANA hawafanani! bado niko katika kutafakari juu ya nani ni afadhali ya mwenzie. Kwa mwenendo wa matukio haswa ya KIMAFIA yanayotokea yananipelekea kuichambua historia ya ukombozi wa taifa hili kama ambavyo ukombozi ulivyofanikishwa katika mataifa mengine Duniani.

CCM wakiwa ni washika dola, naamini wana nafasi nzuri ya kufanya ''umafia'' ( refer to harakati za kudai UHURU- TANU) kwani wamekumbana na mengi katika kuhakikisha utawala/ serikali yao inaendelea kutawala kama ilivyo kwa serikali nyingi zilizoko madarakani (this is FACT not opinion).

CHADEMA nao wakiwa ni wapinzani wanaokaribia kutawala nao wana nafasi ya kufanya ''Umafia'' pia. Huwezi Kutawala nchi bila kuwa na ''umafia'' (This is FACT as well ) huku ukitegemea kura tu za wananchi ambazo mie naamini huwa baraka za mwisho tu baada ya vita kubwa za chini chini, za siri na wakati mwingine za hatari. Wanasiasa wote wanajua hili.

Natarajia kuendelea KUSIKILIZA PAMBIO nyingi tu zenye melody tofauti tofauti toka kwa vyama hivi huku nikiwataadharisha WENYE KURA kuwa 2015 kura yako iwe kwa TANZANIA, hiyo ndio itakuwa hukumu ya kweli!​
 
Waraka mlioandaa baada ya kuandaa mikakati ya mauaji; waraka mlioandaa kuhalalisha mauaji!!. Haitawasaidia! Damu ya watu inayomwagika itawahukumu.
Mungu mwenye haki anawajua wenye haki wake.
CCM die now; let my people live.
we dada/mama, waraka unaoongelewa ni ule uliovuja toka kamati kuu ya CDM, sijui una maanisha nini unapose''''waraka mlioandaa baada ya kuandaa mikakati ya mauaji''''''!!!!!!! zinduka
 
Nape: Kauli zako zinaandikwa mbinguni. Mwogope Mungu usilewe madaraka na propaganda za kidunia. Kama huwezi kusema ukweli unaoufahamu nyamaza kimya. Wokovu wako uko wapi? Mbona unalitukanisha jina la Jehova kijana? Acha kumkufuru Mungu kwa thamani ya chama kinachopita na kinchoweza kufutuka mwaka 2015!
 
Kwa kile kilichoonekana kuwa ni mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa Amani kunakoandamana na umwagaji wa damu ambako siku zote Chadema wamekuwa wakiyafanya, Nape awashukia na kusema kuwa chama chao kina mlegwa wa kigaidi.
matukio hayo ambayo yanazidi kshamiri siku hadi siku, yamekuwa yakifanywa na wafusi wa CHADEMA kwa amri ama maelekezo ya viongozi wao, kwa mfano; katika mkutano wa ndani wa viongozi wa chadema ambao ulipanga mkakati mpya wa kusabotage serikali iliofanyika nyumbani kwa Mbowe mikocheni pamoja na mambo mengine ulimuagiza Rwakatare kuelekea Iramba ili kuandaa kikosi kazi na kuendesha zoezi la kumchafua Mwigulu, Rwakatare alisafiri tarehe 11 kuelekea Singida kusimamia zoezi hilo ambalo tayari limeshasababisha maafa. Ambapo tayari wafuasi wa CCM na MWIGULU wameshapata madhira makubwa kwani Kijana mmoja wa CCM ameuawa na wengine ni majeruhi tangu kuanza kwa zoezi hilo chini ya Rwakatare.

Ifuatayo ni VIDEO ya NAPE akioanisha matukio ya CHADEMA na UGAIDI.

NNAUYE::CHAMA CHA KIGAIDI..................... - YouTube

He! akili ni nywele ......, kwahiyo ugaidi wa CHADEMA unajidhihirisha katika nini? katika katiba yao? katika sera zao? au kwa kuwa ni chama chenye nguvu kinachoipa jakamoyo kibibi CCM? maana labda ukiipa jakamoyo CCM basi unakuwa Gaidi,Mdini, mtu wa kanda n.k

Askari Polisi waliotoa ushahidi wao katika kesi ya Ndago wamedai kuna kiongozi wa CCM alitekeleza mauaji katika eneo lile na waliokamatwa kuhusika na tukio lile wooooote wamesimamiwa dhamana na CCM.

CHADEMA kimekuwa ni chama cha Kigaidi tangu lini? je mnataka kuitangazia Dunia kuwa watanzania ni magaidi? pamoja na serikali yao? na kuwa tutengwe na kuogopwa kwa kuwa ni magaidi? maneno ya hofu ya kupoteza uongozi wa nchi yasitufanye tukashindwa kuijenga nchi yetu jamani tuwe makini kwa kauli zetu sidhani kama Tanzania ina ubavu wa kuhimili misukosuko ya kigaidi kama itakuwepo na tusiipalilie au kuijenga katika fikra za watoto wetu.

ama kweli UCHI WA AKILI NI MBAYA ZAIDI KULIKO UCHI WA MWILI
 
we dada/mama, waraka unaoongelewa ni ule uliovuja toka kamati kuu ya CDM, sijui una maanisha nini unapose''''waraka mlioandaa baada ya kuandaa mikakati ya mauaji''''''!!!!!!! zinduka

Kwanza mimi si wa jinsia hiyo.

Pili, nitakuwa wa mwisho kuwa mhanga wa siasa zinazodhoofisha fikra. Fikra zangu zitaendelea kufanya kazi bila kuathirika na hii michezo michafu ya CCM. Mikakati ya mauaji kupangwa na CHADEMA?? Ili CHADEMA inufaikeje kupitia mikakati hiyo??. Kwa akili ya kawaida tu, CHADEMA haina hata chembe ya faida katika 'mikakati ya mauaji inayopangwa na CHADEMA' zaidi sana mnufaikaji ni CCM. Kwa nini tusiamini kwamba CCM wanafanya mikakati hii kwa jina la CHADEMA ili wavune manufaa makubwa??!!

Mwisho, unahitaji ukombozi.
 
Back
Top Bottom