Nape anapotoa Maagizo kwa Waziri Magufuli...

NnyaMbwate

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,678
1,204
Katika Taarifa ya Habari ya TBC1 ya saa 2 usiku huu, Bwana Nape Nnauye akiwa Songea anaonekana akimwagiza "rafiki yake" Waziri wa Ujenzi Mh. Dr. John Maghufuli aende Songea akakague ujenzi wa barabara ya Namtumbo. Anaendelea KUAGIZA kuwa ikiwezekana Mkataba wa ujenzi uvunjwe, atafutwe mkandarasi mwingine. Hii imekaaje? Nawasilisha.
 
ha!,ha!,ha!,......wakubwa! Nimecheka sana,ama kweli hii ndio serikali iliyokufa inasubiri kuzikwa.Yaani katibu mwenezi wa chama anamuagiza waziri?dah!....
 
Hii inaitwa verbal diarrhoea.

Ni ugonjwa unaowashambulia sana wanasiasa uchwara.

Dalili zake kuu ni kusema ovyo, kuropoka,kusema bila kufikiri,

Dawa ni kuachana na siasa
 
Magufuli anatekeleza ilani ya magamba na Nape ni mtoto mwenye mbwa wa magamba....Magufuli lazima afuate!!umesahau CC iliridhia kuvunjwa baraza la mawaziri???
 
Hata mimi nimesikia nikashangaa! Huenda ndiyo dhana ya CHama Kusimamia Serikali! Hivi waziri anapata maagizo toka wapi na kwa nani? Naona sasa kunakuwa na multiple chains of command.

Huenda anakumbuka enzi za Chama kushika hatamu amesahau kwamba sasa hivi maana ya kusimamia ni eyes on hamd off. We have a long way to go.
 
Nape hajui maana ya uenezi!mwacheni chadema inaendelea kuzoa wanachama kila kona
 
Nape alistahili kuendelea kuwa mkuu wa Wilaya, nashangaa kwa nini hakuteuliwa katika uteuzi huu wa mwisho
 
Nape si ndio makamu wa raisi
Katika Taarifa ya Habari ya TBC1 ya saa 2 usiku huu, Bwana Nape Nnauye akiwa Songea anaonekana akimwagiza "rafiki yake" Waziri wa Ujenzi Mh. Dr. John Maghufuli aende Songea akakague ujenzi wa barabara ya Namtumbo. Anaendelea KUAGIZA kuwa ikiwezekana Mkataba wa ujenzi uvunjwe, atafutwe mkandarasi mwingine. Hii imekaaje? Nawasilisha.
 
Katika Taarifa ya Habari ya TBC1 ya saa 2 usiku huu, Bwana Nape Nnauye akiwa Songea anaonekana akimwagiza "rafiki yake" Waziri wa Ujenzi Mh. Dr. John Maghufuli aende Songea akakague ujenzi wa barabara ya Namtumbo. Anaendelea KUAGIZA kuwa ikiwezekana Mkataba wa ujenzi uvunjwe, atafutwe mkandarasi mwingine. Hii imekaaje? Nawasilisha.
Kwa hali hii hoja ya Mh. Zito ifanye kazi inaonyesha nchi hii haina waziri Mkuu hadi Nepi or sorry Nape anatoa maagizo kwa waziri.
 
Huu unaweza kuwa ni utaratibu mpya wa publicity wa chama kumuagiza waziri nini cha kufanya kupita vyombo vya habari? Nape anafahamu kitu kinachoitwa 'protocol? Alishindwa nini kwenda kumuona waziri Magufuli badala ya kutoa order kwenye media? Hajui namna nyingine ya kufikia Magufuli?

Na kwa mtindo huu uhusionao kati ya cabinet na Nape utakuwaje?
 
Hata wewe ukitaka kutoa maagizo kwa Waziri unaweza. The question, however, will be whether or not the minister will act acording to those instructions.
 
Kiitifaki chama tawala kiko juu zaidi ya serikali...so alichokifanya Nape ni sahihi.
 
Kiitifaki chama tawala kiko juu zaidi ya serikali...so alichokifanya Nape ni sahihi.

Kama atakuwa amesema atamshauri waziri nakubaliana nawe ila kama kasema atamwagiza waziri kakosea kwasababu katika mfumo wa serikali link ya chama na serikali ni rais. Hivyo Nape hana mamlaka ya kumuagiza waziri tena hata mwenyekiti. Anachoweza kufanya kuongea kirafiki na mapombe kwamba nimepita huku nimekuta hili na lile wakashauriana likaenda-hata mimi na wewe tunaweza kufanya hili. Au anaweza kumuandikia katibu mkuu wake wa chama katika ripoti yake ya safari na katibu akawakilisha kwa rais ambaye atamwagiza au kushauriana na PM na baadaye Pombe ataagizwa. Huu ndio mfumo wa utendaji. Huyu Nape inabidi aingie jandoni tena.
 
Nape ni kilaza tu na ni yaleyale ya magamba kuridhisha uongozi kama wakifalme hakuna lolote na sasa hivi TUMESANUKA HATUIBIWI TENA WALA KUNYONYWA NA MAFSADI ,MWISHO WAO 2015 TUMEDHAMIRIA KUWANG'OA WOTE.
 
Kwanza katika kuonesha umbumbumbu wake anasema anamuagiza waziri 'avunje mkataba' na kumuweka 'mkandarasi' mwingine kana kwamba mkataba uliingiwa kati ya 'waziri' na 'mkandarasi'. Huu nao ni upuuzi mwingine, hata hivyo ni upuuzi mzuri sana kwani unawafanya waendelee kuonekana wapuuzi.
 
Back
Top Bottom