Nape Aikubali CHADEMA,Ntagazwa apokelewa rasmi

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wakuu leo tulikuwa tunafanya Mkutano Mkuu maalumu wa kumpitisha mgombea Urais na mgombea mwenza wa CHADEMA na kupitisha Ilani ya Uchaguzi 2010. Dr Slaa na Saidi Mzee Said wamepitishwa rasmi kupeperusha bendera ya CHADEMA.

Dr Slaa amehudhuria mkutano huu akitokea Hospitali alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa mkono wake. Baadaye alirejea tena hospitali kwa matibabu. It was so sad but it had to be that way..

Katika kikao hki tulialika wageni toka kada mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa.

Kati ya Wageni waliohudhuria ni pamoja na kijana machachari aliyeangushwa kwenye kura za maoni za Ubungo Nape Nnauye. Wakati akitoa salamu toka chama chake amekiri kwamba CHADEMA ni chama kilichojijenga kitaasisi kuliko alivyokuwa akidhani. Nape alikuwa akimwakilisha Katibu wao Mkuu Yusuph Makamba. Amesema anaikubali CHADEMA sana.

Kwa upande mwingine Waziri wa Zamani Arcado Ntagazwa amepokelewa rasmi CHADEMA na kusema kuwa CCM sio mama yake mzazi hivyo amejiunga rasmi na CHADEMA na anatarajia kugombea Ubunge jimboni kwake.

Nape hajajiunga na CHADEMA kama inavyovumishwa

08_10_hxqb4f.jpg
 
CCM kumpeleka Nape katika kuongoza delegation yake instead of Makamba or another senior officionado ni dharau.

CHADEMA wanafurahia "Nape aikubali CHADEMA".

Hilarious.
 
CCM kumpeleka Nape katika kuongoza delegation yake instead of Makamba or another senior officionado ni dharau.

CHADEMA wanafurahia "Nape aikubali CHADEMA".

Hilarious.

Umeona eeh....siasa kweli gozi gozi, sasa hapo dada Regia Mtema sijui anajivunia nini..vipi Mrema alialikwa?..
 
CCM kumpeleka Nape katika kuongoza delegation yake instead of Makamba or another senior officionado ni dharau.

CHADEMA wanafurahia "Nape aikubali CHADEMA".

Hilarious.
Sad. I think this is now condoning trivialities at its best.
Egoistic mentality za namna hii ("wasomi" wengi sana wanazo) ndizo zinatufanya tusifike kokote nchi hii.
Let's address those underlying critical issues za kuiondoa nchi hii kutoka hapa kwenda kule....badala ya kuangalia sura za watu (eti nzuri/mbaya; kubwa/ndogo).
 
CCM kumpeleka Nape katika kuongoza delegation yake instead of Makamba or another senior officionado ni dharau.

CHADEMA wanafurahia "Nape aikubali CHADEMA".

Hilarious.

Heshima ya CCM ina thamani gani? Ukiona unaheshimiwa na CCM ujue una kasoro kubwa...
 
Nimeona kwenye TBC1 akivalishwa t-shirt ya CHADEMA, halafu mwenyewe akaivua haraka kama vile ina upupu!
 
Nimeona kwenye TBC1 akivalishwa t-shirt ya CHADEMA, halafu mwenyewe akaivua haraka kama vile ina upupu!

Mazee umekuwa kama macho yetu tuliokuwa mbali na TV. Thanks.

Moments like these have a way of testing one's quickthinking. It was ill advised to put it on in the first place, he probably did put it on under some pressure to appear civil, and realized just one snap and he would look ridiculous, more ridiculous than Dukakis in army fatigues.

But above all, the entire enterprise of putting the Tee on him was ill advised and predatory. Benevolence does not dictate that, some prank at CHADEMA lacked in benevolence and made Nape look like a lost puppy.
 
Nape hakutakiwa kukiwakilisha chama chake kwenye mkutano mkuu wa chama kingine kama CHADEMA; hiyo ilikuwa ni dharau ya CCM kwa chama chenu. Kama nyinyi mlipeleka ujumbe mzito kwenye mkutano wao, iweje wao wawaletee watu wasiokuwa na nguvu yoyote kwenye chama chao kukiwakilisha katika mkutano wenu huo?
 
Sisi hatuangalii cheo cha mtu tunaangalia dhamira dhati ya mtu.Binafsi nimemfurahia Nape kuliko angefika Makamba.Alionge vizuri kwa kuwa dhamira yake yafanana na yangu..Aliongea vizuri kwa kweli na ninaamini alichokiongea kilitoka moyoni.
 
Kama dhamira yako inafanana na yake mbona mko vyama vyenye tofauti kama usiku na mchana ?

Unaelewa dhamira kuu immediate ya wapinzani ? Kama unaielewa unaweza kusema Nape ana dhamira hiyo hiyo ?
 
Sisi hatuangalii cheo cha mtu tunaangalia dhamira dhati ya mtu.Binafsi nimemfurahia Nape kuliko angefika Makamba.Alionge vizuri kwa kuwa dhamira yake yafanana na yangu..Aliongea vizuri kwa kweli na ninaamini alichokiongea kilitoka moyoni.

Nyie kweli mmekusudia 'kumharibia' huko kwenye CCM. Maana nimemwona pale mlipomvika t-shirt yenu juu ya shati lake, alipomaliza kuivua alisema 'mtafanya jina langu lisirudi Dodoma!' Sasa hapa unapomsifia hivi hilo jina litarudi kweli?

Halafu kwa nini mmemkubalia Ntagazwa kugombea ubunge Kibondo, ina maana kabla hajahamia kwenu hamkuwa na plan ya kuweka mgombea Kibondo? Hao ambao wamekuwa waaminifu kwa CHADEMA miaka yote mnawapa ujumbe gani mnapowaacha na kumpendelea aliyejiunga leo? Hamuoni kuwa mnawakatisha tamaa wengine?

Na pia napenda kuwatahadharisha kuhusu Mabere Marando, bingwa wa kuvuruga vyama. Mkijisahau mkamweka jikoni atamwaga sumu kwenye mboga mtatafutana hamtaonana! Si vyote vyafaa kuzoa ati! Muwe makini na hii 'zoa zoa'.
 
Nape hakutakiwa kukiwakilisha chama chake kwenye mkutano mkuu wa chama kingine kama CHADEMA; hiyo ilikuwa ni dharau ya CCM kwa chama chenu. Kama nyinyi mlipeleka ujumbe mzito kwenye mkutano wao, iweje wao wawaletee watu wasiokuwa na nguvu yoyote kwenye chama chao kukiwakilisha katika mkutano wenu huo?
Inaonyesha arrogance ya CCM. Kuanzia wasinipigie kura...
 
Back
Top Bottom