Naongea naye nini?

Nilikwambia miye...hawa watoto wa siku hizi, kama mzazi unaweza kudhani hawajui lolote kumbe wako loaded na so much info mpaka unaweza kushangaa. Sasa hapo ulipoulizwa, "Wewe hujui?" ulijibu nini? au ulijikausha tu!? lol!

Aisee ninacheck tamthilia Star TV kuna mkaka mmoja ameact kama shoga, nikasema "huyo ni kama shoga eeh", my son kaitikia "ndiyo".

Before kulikuwa na tangazo la Dume, nikamuuliza hiyo ni nini? Akanijibu "condom ya kiume.... kwani wewe hujui?".

It seems he know a lot more than l thought, some how l how l feel my job has become somewhat easier. Ni kujazia Mungu anasema nini juu ya nini, ngoja nitafute verse kwenye biblia about ushoga. Kuna mtu anayo kichwani?
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuu,

EMT umenikumbusha mbali sana na mambo ya government travel warrant!!

Ilikuwa na raha yake...behewa la wanafunzi lilikuwa linaogopwa zaidi ya FFU...!!

Jamaa mmoja ambaye alikuwa Form 5 Iringa miaka ya 87 alikumbwa na kashfa ya kuua mtu aliyevamia behewa lao kwa kumrusha dirishani!!


Halafu jambo la kushangaza...baadhi ya walimu walikuwa wanafagilia sana huo mfumo wa bullying wa form 2 dhidi ya form 1!!

Babu DC!!
shuleni kwetu ilikuwa inaitwa kukatwa mkia!tarehe 9/09.hiyo siku form one walikuwa wanapigwa sana na kumwagiwa amji vitandani!
siku hizi sidhani kama haya mambo yapo kwa kweli!
 
Nakuelewa sana snowhite,

Wazazi wenye mabinti wanapata shida sana ikifika kipindi hiki....

Kuna mmoja (mwamke) nilimtania kuwa anajisikiaje binti yake kwend form 1 (boarding) akaanza kulia....

Mwingine ambaye ni mwanamume (mtoto wake yuko mwaka wa 2 chuo), ukiongelea mambo ya watoto wa kike anakosa amani kabisa!!

Naamini ukienda nao taratibu wanaweza kuvuka hiki kipndi kigumu salama!!

Babu DC!!
tupo wengi tu kwa kweli
 
hata kama anajua, na ni big boy kweli, mie nilianza kusema tangu akiwa 4yrs.

Ila mie, huwa naamini, mtoto anakumbuka sana kitu alichoambiwa na mzazi, ndio maana si lazima amjaze maneno mengi.

Ila vile vitu vya msingi kama kulinda uanamme wake mie naona muhimu, vingine atajifunza mwenyewe.

Na akiwa anarudi ndipo anaongeza dozi.

Sidhani kama kuna haja ya kumwambia hayo. Kwanza anawezadhani kama unamhisi au una wasiwasi nae. Unadhani kwa mazingira ya sasa mtoto wa miaka 12 hajui? 12 years old is a big boy. Empirical evidence hiyo hapo chini.
 
Kongosho dudu kuganda ndio aje? Aisee sijui mengi nahitaji msaada kwa upande huu. Hopefully uncle wake atapata muda wa kukaa naye akienda Dar. Duh, ningekuwa caught unaware aisee.
 
Last edited by a moderator:
sikumbuki kitabu gani, lakini story ya ibrahimu, Ruth na kuchomwa Sodoma na Gomora.

Usimjaze mambo mengi sana kwa leo, kama alivyosema Babu DC. Kumweleza mtoto haya mambo ni mchakato, mie sijawahi mwambia ushoga, japo anajua anatakiwa kulinda hifhadhi zake kwa nguvu zote.

Na si lazima uongee naye leo, hata kesho ukiwa umeshapanga maneno yako usiku kucha.

Mpe na hint kidogo ya balehe, isije mkuta akiwa shule akashangaa. Mambo madogo kama sauti kubadilika na dudu kuganda maana hili huwashangaza watoto.

Kweli kabisa Kongosho,

Hakuna sababu ya kuongea mambo mengi leo....hata EMT kasema pia...Hakuna sababu ya kumu-overdose mtoto..

Aanze na mambo ambayo yanawavuta kusikiliza...

Mfano...tell him kuwa kuna siku bomba lake litamloanisha yeye mwenyewe na akiona hayo asishangae...

Pia mwambie kuwa akienda boarding akumbuke sana kufua chupi kila siku kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wachafu kwa kutofua chupi mara kwa mara....I hope atakuwa nazo za kutosha....Sio kama enzi zetu ambapo ni mastaa wachache wengeweza kuwa na pair 2 au zaidi!!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Nilikwambia miye...hawa watoto wa siku hizi, kama mzazi unaweza kudhani hawajui lolote kumbe wako loaded na so much info mpaka unaweza kushangaa. Sasa hapo ulipoulizwa, "Wewe hujui?" ulijibu nini? au ulijikausha tu!? lol!

Nilisema sijui without looking in his eyes, nahisi amenishtukia fulani hivi. LOL
 
538650_492529450758965_168310883_n.jpg


Inategemea anaenda shule ya aina gani. Only boys? Shule iko town or in a remote area? Kuna shule nyingine za boarding ni tough. Nyingine ni za watoto mayai. Kama alishawahi kusema zomba kwenye thread nyingine, kuna shule za boarding ambazo zinaendeshwa kwa nadharia kuwa mwanafunzi anaepelekwa pale ni kwa ajili ya kupata utulivu na aondokane na vishawishi vya mitaani ili apate kujikita kwenye masomo.

Zipo nyingine ingawaje ni chache sana ambazo zinaendeshwa kwa nadharia ya kuwapatia wanafunzi mazingira ya hali ya juu kwa kila kitu kama vile malazi, makazi, lishe bora na nzuri, michezo ya kuwajenga miili na akili na kuwafanya wawe wanaipenda shule na masomo kuliko nyumbani na vishawishi vya mitaani.

Wa kwako anaenda shule ya aina gani kati hizo hapo juu? Kwa nini umeamua aende boarding school badala ya day school? Did you reach the decision together?
Nilisoma boarding O Level in a very tough school. Nilipelekwa pale ili nijifunze maisha hasa kuishi na watu wa aina mbalimbali, which I did.

Baba yangu aliponidrop hapo shuleni, hakusema lolote zaidi ya kunikatia pocket money na kuniaga. But my mum was very concerned kwa sababu nilikuwa mdogo sana kiumri na umbo. I was 14 by then and the youngest in the school. As a mother, I understand you must be concerned too.

Tulipofungua shule baada ya Pasaka baadhi wanafunzi hasa wale mayai hawakurudi tena shule. Waliobaki wengi walifukuzwa shule kwa sababu mbalimbali. Mtihani wa mwisho kabisa wa form four (I remember it was Biology II) tulifanya huku shule imezingirwa na FFU na baada ya paper tulisimamiwa na polisi kufunga virago vyetu na kuondoka eneo la shule. It was those days though. Siku hizi nafikiri ni shule chache za aina hii zimebakia. Pia shule binafsi ziko money oriented zaidi, so kuliko kumfukuza shule mwanafunzi ni heri kumpa suspension.

Kuhusu bullying, yes ipo. Lakini bullying ipo pia kwenye day schools. Kuna shule zenye mtindo wa form two kuwanyanyasa form one kama kulipiza kisasi vile kwa waliyotendewa wakati wakiwa form one. Kuna makundi pia. Nafikiri the most issue ni kundi atalokuwa ana- mingle nalo. Makundi mengine ni mazuri, mengine ni mabaya.

Kuhusu ushoga, possibly yes, but inategemea pia na system ya uongozi wa shule. Shule niliyosoma, uongozi wa wanafunzi ulikuwa very strict na wafutiliaji. Wale waliokuwa wanajulikana kuwa wanaendekeza ushoga walikuwa wanafunguliwa kwenye ofisi ya vijana na kupewa kibano cha kufa mtu. Again it was those days. Siku hizi ushoga ni jambo la kawaida kwenye jamii yetu.

At the end of the day inategemea pia jinsi ulivyomkuza kwa miaka hiyo 12. O level, kundi langu lilikuwa la wavuta bangi, lakini I never smoked that thing mpaka leo, though nilikuwa mtoro na mbishi kuchapwa bila sababu za msingi. lol. So, it could go either way kulingana na mtoto mwenyewe na jinsi alivyokuzwa. Kama zipo sababu za kumpeleka boarding, na kama uamuzi wa kwenda boarding hasa hiyo shule mlifikia pamoja, then I am sure hutakosa cha kuongea nae.

Hapo mwisho umenikumbusha mbali sana..Home mm kampani yangu ilikuwa wavuta bangi na wacheza kamari lakini sijawahi gusa hiyo mambo kabisa..Inategemea na malezi aisee..
 
Kweli kabisa Kongosho,

Hakuna sababu ya kuongea mambo mengi leo....hata EMT kasema pia...Hakuna sababu ya kumu-overdose mtoto..

Aanze na mambo ambayo yanawavuta kusikiliza...

Mfano...tell him kuwa kuna siku bomba lake litamloanisha yeye mwenyewe na akiona hayo asishangae...

Pia mwambie kuwa akienda boarding akumbuke sana kufua chupi kila siku kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wachafu kwa kutofua chupi mara kwa mara....I hope atakuwa nazo za kutosha....Sio kama enzi zetu ambapo ni mastaa wachache wengeweza kuwa na pair 2 au zaidi!!!

Babu DC!!

Awe anafua soksi zake na anaoga mara kwa mara pia na siyo kupiga passport kila baada ya mwezi. Naamini Feza kuna maji ya kutosha.
 
Aisee ninacheck tamthilia Star TV kuna mkaka mmoja ameact kama shoga, nikasema "huyo ni kama shoga eeh", my son kaitikia "ndiyo".

Before kulikuwa na tangazo la Dume, nikamuuliza hiyo ni nini? Akanijibu "condom ya kiume.... kwani wewe hujui?".

It seems he know a lot more than l thought, some how l how l feel my job has become somewhat easier. Ni kujazia Mungu anasema nini juu ya nini, ngoja nitafute verse kwenye biblia about ushoga. Kuna mtu anayo kichwani?

Mambo ya ushoga kwenye biblia hayajaandikwa wazi sana lakn katika moja ya dhambi zilizoiangamiza sodoma na gomora mojawapo ilikuwa ni ushoga..wale watu walitaka kuwashoga hadi malaika...Soma kitabu cha mwanzo..
 
Awe anafua soksi zake na anaoga mara kwa mara pia na siyo kupiga passport kila baada ya mwezi. Naamini Feza kuna maji ya kutosha.


Kweli kabisa mkuu EMT,

Soksi nazo ni janga kubwa kwa watoto wa kiume...La kushangaza...girls wanakuwa mbele sana kwenye mambo ya usafi wa mwili na nguo za mafichoni!!

Pia amweleze umuhimu wa kupiga mswaki na kuhakikisha hatoi harufu mdomoni....Kwa siku za karibuni, karibu nusu ya wanaume ninakutana nao wananuka mdomo!!

Hapa Bibi ndipo alikuwa anachomekea kuwa...."kumbuka kuwa msafi ili tusikose wakwe warembo...kwamba warembo hawapendi mwanamume mchafu...na anayenuka kila mahali"!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapo mwisho umenikumbusha mbali sana..Home mm kampani yangu ilikuwa wavuta bangi na wacheza kamari lakini sijawahi gusa hiyo mambo kabisa..Inategemea na malezi aisee..

Ni kweli. Wanasema mtoto umleavyo, ndivyo atakavyokuwa. "Don't say one thing and do the opposite. And neither should parents impose anything on their children. They should instead strive to convince them through their own convictions," per Prof Anne Muigai on "Parenting for the future".
 
Ndo maana nimekwambia kuwa kuna vitu ukae tayari kupigwa shule.....

Shukuru Mungu baada ya hilo jibu amekupotezea...angekuwa kama hawa wajukuu zangu, lazima angeanza kukupiga shule mara moja!!

Babu DC!!

Babu Kaunga alikuwa sawa kusema hajui "without looking in his eyes"?
 
Last edited by a moderator:
kuna saa kidude kinaamka bila sababu
mie alinifuata akaniambia 'mbona inaganda ganda? Inanisumbua.

Hiyo term ya kuganda aliitengeneza mwenyewe, hakujua ni nini kimempata.

Vitu kama hivyo lazima uwe umemwandaa kidogo.

Kongosho dudu kuganda ndio aje? Aisee sijui mengi nahitaji msaada kwa upande huu. Hopefully uncle wake atapata muda wa kukaa naye akienda Dar. Duh, ningekuwa caught unaware aisee.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa nini hii thread isiwe sticky.........Mods tafadhali.
Nakumbuka nilipobalehe nilikuwa sipendi kukaa na mama karibu. Kampani yangu vidume wenzangu.

Usimpe vitu vingi sana........Huko anapoenda anatakiwa/atajikuta anatengeneza njia yake mwenyewe.

Wakati mwingine watoto wa kiume hawataki kuonekana na "maadili" saana. Kidogo ununda ni kama njia sahihi
kwa siasa za Boarding school.
 
My son anaenda kuanza form one, (preform one next month) boarding school he is going to be 12 next year.

As a mother namuambia nini? Nafeel kuna kitu napaswa kumwambia sijui nimwambie nini na jinsi gani.

Sijasoma boarding school O'level so sijui kunakuweje, nasikia ushoga unaanziaga huko. Bullying inanitia wasiwasi ukizingatia umri wake ni relatively Mdogo.

Nisaidieni nini cha kuongea naye.
N.B Namlea mwenyewe as a single mom.

Usiogope, mnunulie kitabu cha dini, mfano bible or quran..then mwambie asiige maisha ya mtu yeyote. Aishi naturally.
 
ndio maana huwa naamini sana maneno ya mzazi au nyumbani kwa ujumla.

Kuna viunzi mtu unaviruka ujanani kwa kukumbuka neno moja tu la mzazi.

Hongera kwa kujitambua.

Hapo mwisho umenikumbusha mbali sana..Home mm kampani yangu ilikuwa wavuta bangi na wacheza kamari lakini sijawahi gusa hiyo mambo kabisa..Inategemea na malezi aisee..
 
Thanks EMT kwa uchambuzi yakinifu, anaenda Feza Boys sasa sijui for sure iko kwenye kundi gani. Labda waliosoma hapo wanaweza nitoa wasiwasi juu ya malezi.

Dah kumbe tuna mama zetu humu, I went to Feza too almost 12 years ago,, those days in mikocheni and later in bahari beach for my high school after o level si ndo tulioianzisha bahari beach campus,,, don't wory mom ni nice schools kweli na mkianza form one too mnapewa kama seminars about boarding life, how to survive and so on... Those days o level tulikuwa tunafuliwa uniform sijui nowdays... But to be honest ataenjoy sana form one yake as wale waturuki they know to raise kid.

My self nilikuwa mtukutu sana as hata niliposhushwa form 1 b mkubwa alijua naenda kuanzisha vita but counceling zilinibadilisha sana hadi nilivyorudi likizo akashangaa although akifika form two vi girlfriend vitaanza vya cornelious na marian he he he, maana boys stories after classes mnafundishana datings... But its a nice campus although sijaenda muda. But I promise myself even my son nikifanikiwa kumpata atasoma pale as life is real good those days...

Hopim mr mahmet is still there he will guide him... Have a gudluck madam umenikumbusha mbali sana

Na kama hajui mpira atakuja kuwa bonge la soccer fans as school ilikuwa inaonesha mpira those days so almost all students overthere talks about football
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom