Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,597
Babu, mimi nilisema haya nikakumbushwa tena kwa sauti kubwa kabisa kuwa mtoto anaenda Feza, siyo shule tu ya uchochoroni. kule wanasoma watoto wa mabilionea kwa hiyo na mtoto wa Kaunga naye anatakiwa kwenda kama milionea. Well, tupo tofauti. mimi siwezi kujiita ni wa level ya chini, lakini kila ninapompeleka mwanangu shule (boarding) huwa namwuliza matron minimum amount ya kumwachia mtoto as a pocket money, najua matron angeniambia minimum ni 2M nisingeshindwa kutoa, lakini akiniambia ni elfu 20 huwa naacha elfu 20.
Huyu mtoto yupo shule..... atakula, atalala, ataingia darasani............. akiumwa atatibiwa ikishindikana nitapigiwa simu, kwa nini nimwachie laki? ataifanyia nini? si bora hiyo laki nimwekee kwa account yake ataikuta siku atakapoihitaji?
Pamoja na mzazi kumwelewa mtoto, kitu muhimu pia ni kukaa na mtoto wako na kumwelewesha. kama wazazi hatupaswi kudictate mambo, sawa, lakini tunapaswa kukaa na watoto na kuwaambia hali halisi. na huwa wanaelewa wala hawana shida
Kwa hapo tu (Blue)....naomba utegemee kupokea PM yangu muda si mrefu...Ikizingatia tuvyokaangwa huku site...Unaweza kuwa mkombozi bila kutegemea!!
Nakubaliana na wewe, watoto ni waelewa sana endapo tukiwafundisha kuelewa kwa kuwapa sababu ya kitu tunachokiongea....Nashukuru sana kwa michango yako na pia nimefurahi kwamba bado kuna wazazi wanawaona watoto kama watu wazima wa kesho ambao wanatakiwa kuwa reasonable and responsible!!
Nachukia watu wanaowadekeza watoto na kuwaona kama vile wameumbwa kwa precious metals au fragile materials!
Babu DC!!