Dogo kama huyo anakuzamia PM kuomba mechi. Hahahaha!.Napendekeza ID zetu ziwekwe label..
Mfano under 18
20-30
31-40
Tujuane umri. Hili ni balaa
19 yrs old bado kijana mdogo??Mimi ni kijana mdogo wa miaka 19. Hivi karibuni nimekua nikipatwa na msukumo mkubwa wa kunywa pombe na kuvuta bangi. Kusema kweli najaribu sana kujizuia, lakini naona kama hizi jitihada zangu hazitozaa matunda.....
Kwa muda mrefu sasa, marafiki zangu nawaona wanachukulia hii ishu kawaida sana..... Tukiwa kwenye mitoko, hawawezi acha kulewa ovyo, kuvuta bangi na shisha, na ku-vape. Kwa mtazamo wao, ni kitu cha kawaida sana, na wanaona kama hakuna madhara yoyote yanaweza kutokea. Wanasema 'wanakula ujana', 'wanamwagilia moyo'.....
Miaka mingi sasa tumekua tukiishi haya maisha.... kwenda maclub weekend na 'kula bata'. Mimi nimekua nikijizuia mno...... nazugazuga chupa moja nainya hata masaa 2-3.....
Unaweza sema niko kwenye makundi mabaya, lakini mimi sioni hivyo.... hawa ni marafiki zangu wa muda mrefu, tumekua tukisaidiana sana, sema hapo kwenye mambo ya starehe ndo tunatofautiana.....
Pia ndugu, ukizingatia kwamba mimi ni mchaga(kote upande wa baba na mama), wanatumia sana haya mazaga na wamekua wakinishawishi sana, na hata wengine kuonyesha dharau.... Nakumbuka kuna siku nilitoka na bamkubwa nikakataa kunywa pombe.... alicheka sana na kunishangaa.....
Najua wengine mnaweza sema hakuna shida yeyote kwenye kutumia kidogo, lakini kama nilivosema..... mimi ni kijana mdogo, bado maisha yangu ni marahisi, nategemea wazazi, hivyo bado nina ndoto za kufanya vitu vikubwa na maisha yangu, hivyo naogopa sana pombe na bangi vitanirudisha nyuma. Nimeona watu wengi wakiharibikiwa kwasababu ya pombe na bangi....
Najua humu JF watu wazima mko wengi, naomba mnishauri..... Kuna namna ya kubalance maisha ya kawaida na hizi starehe?? Au niendelee kukaa navyo mbali.... na ikiwa hivyo, nitumie mbinu gani??
Halafu mnanyegeshana na kuambiana upuuzi. Wazee tujitafakari.. Ngoja nihamie majukwaa ya maana labda nitakutana na Wazee wenzanguDogo kama huyo anakuzamia PM kuomba mechi. Hahahaha!.
Wazo zuri sana hilo. Hakika tunaomba kutambuana kwa umri.
Hahahaha!. Nimecheka sana.Halafu mnanyegeshana na kuambiana upuuzi. Wazee tujitafakari.. Ngoja nihamie majukwaa ya maana labda nitakutana na Wazee wenzangu
Muulize kwanza miaka 19 analewa, pesa anatoa wapi?19 years? 🙄🙄🙄
Wewe ni mwanangu kabisa.... Aisee kwaherini JF siitaki tena.
Anakunywa za nyumbani, kwenye sherehe labdaMuulize kwanza miaka 19 analewa, pesa anatoa wapi?
miaka 14..... haikuwa club kipindi hicho.... tulikua tukifunga shule tunajichanga tunakodisha sehemu, tunafanya bash... ila pombe,bangi zilikuwepoMiaka mingi umekuwa ukienda klabu, ndiyo kwanza una miaka 19.
Hiyo miaka mingi ya kwenda klabu ni ipi? Ulianza kwenda klabu na miaka mingapi?
Turudi, unaweza kuwa na urafiki na hao wenzako lakini hulazimiki kwenda kwenye maeneo ya Starehe au wanapovuta bangi. Ambatana nao kwenye mambo mengine, ukishaona sada ni muda wa kwenda Club, wewe nenda nyumbani kalale. Nina hakika hawakulazimishi.
Kila kitu ni maamuzi. Ukishaamua hakuna kinachoshindikana. Ila mwenyewe huna imani tena juu yako. Weka imani yako thabiti.
Jiwekee sababu za kujizuia kunywa pombe au kuvuta bangi. Iwe kiafya na kiuchumi na hata kijamii. Sababu hizo ziwe kichocheo cha wewe kutotaka kujaribu kutumia vilevi.
Kuwa karibu na Mungu. Omba akuongoze. Mshinde shetani. Marafiki zako kuwa wavuta bangi isikufanye nawe uvute. Kama unalazimika basi badili aina ya marafiki.
-Mnajivunia upumbavu sana.Usiache kabisa unaharibu mila kwetu wachaga ....jitahidi uicontrol pombe isikucontrol nashukuru hujataja uraibu wa uterezi hii ndio case study ya dunia
19 years?
Wewe ni mwanangu kabisa.... Aisee kwaherini JF siitaki tena.
ishaenda miaka 6 imepita 😂Mtoto sana,naomba itunze sana bikra yako pleaseee
nikijifanya mkubwa watu wananishusha sasa nifanyeje😂19 yrs old bado kijana mdogo??
Kweli kabisa maana hataaminika sehem yyte ile atayoenda sasa atakua binadam wa aina ganiAchana na hayo makitu kwa sasa. Utafanya baadae sasa hivi utaharibikiwa mchana kweupe