Alicia leon
Member
- Apr 19, 2021
- 52
- 113
Habari Wana JamiiForums,
Nimekuja hapa nikiomba mawazo yenu, ushauri na msaada ikiwezekana. Katika maisha yangu nimejaribu sana kutafuta kazi sehemu mbali mbali bila mafanikio, na hata nikipata haidumu kabisa inatokea changamoto naikosa, nimekuwa mtu wa kutamani sana na Mimi niweze kuwa na sehemu moja ya kujipatia riziki lakini inashindikana, na sitaki kukata tamaa licha ya changamoto zote hizi.
Nimejaribu kuanzisha bihashara mbalimbali lakini huwa hazidumu, hata nilianzisha ya kufua na nilipostigi humu Kuna watu baadhi walijitokeza nikawafanyia kwa ufasaha lakini baadae ikatokea changamoto nikashindwa kuendelea. Nashindwa kuelewa ni kitu gani kinanizunguka kwenye maisha yangu na mtaji wangu, inafika kpindi nakosa hata pesa ya kula kwa siku lakini Muumba wetu anazidi kunipa nguvu ya kuendelea kusimama Tena na kupambana.
Na kipindi hiki cha mfungo kwangu kimekuwa ni kigumu sana kwa kukosa pesa ya kujikimu kwa kipindi kizima. Naombeni mnigaie ushauri nifanye nini niweze kusimama imara kwa uthabiti, mwenr kazi pia naomba anisaidie ili niweze kujikimu.
Naombeni mawazo yenu na ushauri wenu maana akili yangu imefikika mwisho kuwaza Mimi ndugu zangu. Nimechoka.