Naombeni ushauri ndugu zangu!!

sina ushauri sana, ila kama ni yule nanii kweli nakupa pole.

Ila nadhani sekta ya uchimbaji wa madini ina uwendawazimu, asilimia kubwa wako hivyo.
Ningekupa mastori ya town hapa ila basi tu.
 
Kama hautaki kuwatenganisha watoto na baba yao,kuna uwezekano mkubwa kikakusaidia kuwatenganisha tena nawe utatenganishwa nao pia! Stuka
 
aisee, mtu awe na pesa shida, awe kapuku shida... umeshauriwa umnyime jamaa unyumba kama njia ya kujilinda na maambukizi... kwa jinsi jamaa alivyo mkorofi, unadhani unao ubavu wa kusimamia hilo?
 
ki ukweli hili la kunyima unyumba ni kitu ambacho hakiwezekani, labda niondoke nyumbani, kwa sasa hata yeye hana maambukizi tulipima naye, cha msingi mimi naona nijipange kujiondokea kabla hajaniletea huwezi jua ni lini, lakini huwezi kuishi na mwanaume ndani ya nyumba moja huku unamnyima unyumba ni hatari anaweza hata akakudhuru.
 
ki ukweli hili la kunyima unyumba ni kitu ambacho hakiwezekani, labda niondoke nyumbani, kwa sasa hata yeye hana maambukizi tulipima naye, cha msingi mimi naona nijipange kujiondokea kabla hajaniletea huwezi jua ni lini, lakini huwezi kuishi na mwanaume ndani ya nyumba moja huku unamnyima unyumba ni hatari anaweza hata akakudhuru.

Unadhani kama ukiondoka sasa hivi kwa kile ulichonacho unaweza kuendesha maisha yako? Kama ndiyo usisubiri zaidi, kama uliweza kuanza naye akiwa hana kitu na mkajenga wote nadhani unaweza hata kufanya hivyo hata ukiwa mwenyewe japo si rahisi
Najua sasa una mipango mingi lakini ebu jaribu kukusanya uwezacho na ukimbie haraka uwezavyo, utapoteza muda na maisha yako kujaribu kupambana na pepo hilo maana si binadamu huyo
 
Hata kama anasema ukiondoka hatawasomesha watoto...bado kuondoka ni bora kuliko kukaa. Si lazima watoto wasome shule za milioni 39 ili wafanikiwe kimaisha. Ondoka akikataa kweli kuwasomesha (maana anaweza akawa anakutisha tu) wapeleke academy za kawaida. Maana sipendi kukutisha ila inabidi utoe sadaka kwa kujikuta huna HIV...lakini siku zako ziko numbered kama mumeo anaendelea kutembea na wauza baa.


Kuna waliokushauri eti sijuhi ukatae ku do nae au utumie condom...hizo ni theory tu ndugu yangu...as long as mtakuwa mnashare nyumba hutaweza kumyima pale atakapohitaji au eti sijuhi umpe masharti...wewe ni mkewe atafanya apendavyo..It is either utoke ndani au jua ataendelea kuku do atakavyo yeye.

Nina aunt yangu mumewe alikuwa ni player kama huyo wako...watu wakawa wanamshauri aondoke maana atakufa na HIV...Unajua alikuwa anajibu nini..eti hawashirikiani kwenye tendo la ndoa...tulibaki midomo wazi tulipokuja sikia ana mimba. Tukamuuliza ya nani? ...anabaki oooh alinibaka.

Wewe bado mdogo na unasema kipesa si masikini kihivyo...move on...ningeweza kukupa ushuhuda mwingi wa wanawake waliokufa kwa ukimwi kwa excuse ya watoto wanampenda baba yao...watoto watateseka. Ila nitawaboa kwa uzi mrefu.
 
Afu umesema umeshaongea na mwanasheria kuhusu divorce..afu haujamwambia ukweli sababu ya wewe kudai talaka. My dear siku zote ukweli utakuweka huru...Najua hapa JF imekuwa rahisi kwako kuandika ukweli kwa kuwa unaongea na computer lakini ikifikia unataka kuvunja ndoa hakuna siri tena... kuwa wazi kutakusaidia.

Wewe unafikiri ndoa inaweza kuvunjwa bila sababu za msingi? Sema yote...sema anazaa zaa hovyo nje ya ndoa...sema unaogopa kufa na HIV...sema umemvumilia lakini hajirekebishi...Hii inaweza kukusaidia ukapata nusu ya mali zake as long as utapata good lawyer.

Mama yangu alipewa nusu ya mali za baba pamoja na kuwa my dady alikuwa na wanasheria wa nguvu wakati mama alisaidiwa na wale wanasheria wanaosaidia akina mama pale kariakoo...why not you...Na ukipata mgao wako hutashindwa kujilelea wanao. Hata kama ana pesa vipi sheria iko wazi nusu ya mali ni yako.
 
Chapa lapa mapema au subiri wakuzike na kilo 1, hapo kilichokuweka mbaka sasa ni hiyo pesa yake tu hamna cha kwamba unampenda au unamoyo wa chuma jamaa angekua kapuku naamini ungekua umeshasepa zamani bila hata kuja humu jf. Kama unashare kwa kampuni na biashara zako ondoka mapema watoto wataishi tu ilihari baba na mama yao mko hai na watapata mapenzi ya yote sema kwa wakati tofauti..
 
kweli palipo na miti wajenzi hakuna! pole dada yangu, wengine tunatafuta wanawake wavumilivu na wenye mapenzi ya dhati lakini wengine ndo kwanza wanawatesa...!!! muombe Mungu wako kwa dhati atakupa muongozo ambao hutaujutia maishani mwako.
 
Pole sana mpendwa, binafsi nimelelewa na mama pekee, na nljiapiza kwa nliyoyapitia ntahakikisha kuwa wanangu wanapata malezi ya baba na mama, kwa hyo naelewa vizur sana hali uliyokuwa nayo, ila pamoja na yote my dear, mumeo amefika mbali mpenz, hana stara wala aib, cjui nimuweke kwenye kundi gani coz ni kama ana matatzo ya kisaikolojia, ila sasa ww sio mtaalam wa hayo, kwa faida ya wano, ni bora uwalee bila baba yao kuliko kusubr wabak bila ya wazaz wote wawili. kisicho riziki hakiliki, chukua hatua.......................pole sana good woman..
 
SALAAM wanaJMF!! mimi ni mgeni hapa, lakini kutokana na post nyingi nilizosoma humu moyo wangu umeridhia kwamba nitaweza kupata ushauri ambao unaweza kuniondoa kwenye msongo wa mawazo niliyonayo!!,. Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 28 nimeolewa na nimebahatika kupata watoto wa 3, kinachonifanya niombe ushauri ni mume wangu kuwa na na wanawake wengi, kwa kifupi tumeishi kwa miaka 9 hadi sasa, yeye ana miaka 39. kwamuda wa miaka yote 9 mwenzangu amewabebesha wasichana wa kazi 2 mimba, anamtoto wa miaka 2 ambaye amezaa na mwanamke ambaye yeye hata haeleweki anafanya kazi gani, amezaa tena na muhudumu wa baa mtoto ambaye ana mwaka sasa halafu kwa sasa kuna muhudumu mwingine wa baa ana ujauzito wa miezi 6 na wote hao akisha wabebesha ujauzito anawageuzia kibao yaani hawataki wala watoto hawatunzi, hivi karibuni ameanzisha uhusiano na muhudumu mwingine wa baa, ( mwanaume huyu siyo mlevi ni msomi wa chuo kikuu anapesa za kutosha na ana kampuni kubwa tu ya uchimbaji madini ambayo pia mimi ninashare kwenye hiyo kampuni) niliwahi kumlalamikia kuhusu hii tabia yake, aliacha kujihusisha na wasichana wa kazi za ndani lakini kwa hao wa nje haonekani hata kujali malalamishi yangu zaidi aliwahi kuniambia niamue nitakavyo yeye anaweza kuishi bila mwanamke na nikitaka kuondoka niondoke na watoto wangu. mimi nimelelewa bila baba na isitoshe watoto wanampenda sana kwa ukweli huwa anamahusiano mazuri tu na watoto. yaani hii Ndoa mimi ndiyo niamue kuvumilia uchafu wake au niondoke yaani ki ukweli naumia na matendo yake lakini watoto wangu pia sitaki waishi kama mimi nifanyeje??? huwa hashauriwi na mtu niliwahi kumkuta na mwanamke tena nyumabani kwetu nikaenda kumweleza wazazi wake alimwambia baba yake naona umechoshwa na mkeo unataka kumwoa na mke wangu alinibeba juu juu mbele ya wazazi wake, huku baba yake akipelekwa Hospital kwa kupandwa na presha., ushauri pls!!!

Pole kidogo na Hongera sana Dadaangu! Hongera kwa uvumilivu wako na pole kwa matendo ya mwenzako juu yako.
Kwanza kumbuka ule usemi unaosema "Mcha mwana kulia hulia yeye". Nakusudia usipochukuwa hatuwa kwa kuogopa kuwatenganisha watoto na baba yao kuna hatari mkawaacha watoto bila ya baba wala mama. Maradhi dadaaangu yanaweza yakakuumbuweni na kuwaacha watoto yatima.
Inavyoonyesha mumeo hakujali kama mke bali ni mlezi wa watoto, basi kubali cheo hicho uchukuwe watoto ukalee na baba atawafuata hao kwa wakati wake kama anawapenda. Usiogope jambo kabla hujalijuwa pengine machungu yake si kama unavyofikiria,jaribu kwanza uone hutoweza kukaa na watoto bila ya baba yao?
Hata katika harakati za matibabu daktari hutumia dawa kwa stage na akiona kuwa maradhi bado hayajapowa basi hutumia dozi kubwa nawe ilivyokuwa mumeo hatibiki basi amuwa kukaa pembeni ili unusuru malezi ya watoto wako kwani huyo bwana anakokwenda sio mbali sana huenda akalipata analolitafuta, sasa akikushirikisha na wewe mtawaacha watoto yatima.
Jengine kama unaweza gawa vyumba ukimwachia akistarehe na vyake wewe ukiendelea na hiyo kazi ya uyaya aliyokutunukia mumeo.
 
Anza kujiandaa kuondoka, lakini hakikisha unafanya mambo yako bila kumstua huyo baradhuli. Kama huna Bank account basi kafungue sasa na uweke pesa nyingi kadri ya utakavyoweza. Kama hutaweza kulipa ada ya shule ya 39 million basi tafuta shule za bei nafuu. Ni vigumu kwenda kuishi peke yako huku una watoto watatu lakini ni bora mara milioni hasa ukitilia maanani huyo baradhuli asivyokuheshimu na kukuweka katika hali ya hatari kwa kutembea na wanawake wengi bila kujali mateso unayoyapata kwa vitendo vyake...Kila la heri.
 
Ndoa ikivunjika rasmi wanandoa hua wanagawana mali nusu kwa nusu...hakuna haja ya kuishi na mwanaume asiyekupenda wala kukuheshimu hivi ukiendelea kuishi nae mwisho wa siku akakuletea ukimwi nani atawalea watoto??maisha bila mume yanawezekana kabisa ukijipanga..
 
Naona mna nyumba zingine kwa hiyo hili sio tabu kwako, kachukue funguo ya nyumba hio mojawapo uamie na watoto. Si mmmejenga wote from A hivyo usitishike.

Lawyer lazima umwambie ukweli, muombe mwenye comment moja hapo juu umu PM akupe contacts za hao na laywer.

Mie I guess kuna kitu bado deep down kinakufanya usitake ondoka. Kaa chini ufikiria sana kama ni kweli kinakuzuia hivyo na faida yake ni nini huwezi ondoka.

Ukweli ni kwamba, Mungu aepushe, usipoanza kujipanga na mali zenu sasa na wewe kujijua wapi una control juu ya mali, utajuta sana baadae sababu hao watoto wote wa nje watapata share pia, hata mliyoanza kupanda wote. So wai ongoe na lawyer na kuwa mkweli ujue lipi lako lipi umwachie.

Kuwa tayari pia kuwa ukiondoka ataleta mwanamke mwingine ndani, na mwanamke akiwa akili juu utajikuta hauna kitu wee ndo maana umeshauriwa pia itasadia anza kuweka pesa au ongeza kama unauwezo wa ku do hivyo kwenye account yako.

Usafiri si mna sita basi beba mawili. Ila duh inaonekana ana fujo na asije kukuua kabla nenda kwa lawyer asap. Ukijifanya mbabe. Utaondoka na sifuri kwa kupigwa etc.

Sijui kwa nini nimeandika chini ila hakuna zaidia yake naye ni Mungu. Please sali muombe akuongoze katika hii issue, yeye ndie anayeweza na muombe akuongoze kupata ufunuo wa bila matatizo.

Mumweke mumeo kwenye sala pia, kama hamtakuwa wote tena basi aelewe matendo yake na azidi kuwa baba mzuri. Omba Mungu amfungue toka katika hilo giza aliomo. Msalie bila kujali kitu. Ni baba watoto. Usisahau kumsalia aache tabia hii.

Pole tena najua mapenzi ni kazi, usiwe na wasi endelea kumpenda ila wewe jiweke kwanza. Au ma barmedi watalea wanao as utakuwa labda hoi na magonjwa etc.

Unaweza kuta ukiondoka akisikia ma lawyer etc ndo ataanza kuomba radhi, usiwe ki softiiii hakikisha unashughulika kwa yeye kujua hakuna mchezo, hata ukimsamehe ajue wewe ni pilipili.

Umo kwenye kampuni? Achana na u share holder je wewe na yeye mpo kama owners? Hata mie naweza kuwa share holder hapo kwenu.

Mali unawekaga jina lako pia?

Goodluck
 
Afu umesema umeshaongea na mwanasheria kuhusu divorce..afu haujamwambia ukweli sababu ya wewe kudai talaka. My dear siku zote ukweli utakuweka huru...Najua hapa JF imekuwa rahisi kwako kuandika ukweli kwa kuwa unaongea na computer lakini ikifikia unataka kuvunja ndoa hakuna siri tena... kuwa wazi kutakusaidia.



nashukuruni kwa ushauri sana jamani walau Moyo wangu unaanza kupata mwanga, na wogo wa kufanya mahamuzi unaanza kunitoka, nitaufanyia kazi na nitarudi tena kuwashukuru!! Asanteni
 
Nashukuruni kwa ushauri wenu tena sana, walau sasa moyo na akili yangu vinaanza kupata mwanga na woga wa kufanya mahamuzi unaanzakunitoka, kwa kweli naanza kujawa na ujasiri, nitayafanyia kazi na nitarudi kuwashukuru.
 
pole sana dada yangu nikweli kabisa mapenzi yanauwa. labda nianze kwa usemi mvumilivu sanaaaa hula mbovu.
huyo baba kwanza ana umri mkubwa kuliko ww inavyo onekana ujana wake ndio anautumia sasa hivi. chakufanya bora ujifunze kumfisadi ili upate kipato ambacho unaweza ukaanzia maisha then chukua watoto wako ondoka. kwasababu anawapenda sana watoto basi atajitahidi kuja kuwaona na ww hapo hapo utaongeza mtaji
ukiona mtu kafikia hatua ya kuwatharau wazazi wake huyo tena ana lana hivyo nibora uondoke litakapo mpata la kumpata atakukumbuka. usilie sana jipe moyo ondoka zako watu kama hao ninayo mifano mingi hata kwa kaka yangu wa tumbo moja ila kilicho mpata hana hamu tena na maisha.
usijali MUNGU atakusaidia
 
Back
Top Bottom