Naomba ushauri wenu niolewe au?

Binafsi nakushauri usiolewe nae kwasababu tu mama yake akimtenga anaweza akaanza kukulaumu wewe na hata kuanza kukuchukia. Ukikosea kidogo unasikia "ndio maana mama yangu aliona giza juu yako, alijua tu hunifai" hata kama ni chumvi tu umesahau kununua.
 
LAAAA! Pole sana dada inabidi nikueleze tu ukeli ni kwamba suala lako nimejaribu na mimi kuwauliza wakuu wangu wa kazi wemenijibu haya: Ukweli ni kwamba huyo kijana anakupenda sana tatizo unalo wee mwenyewe kuna umekuwa si mwaminifu wa mapenzi tangu ufahamiane na huyo kijana tayari umeshamsaliti mara 9 mara yamwisho ilikuwa tar 20/11/2011 bila yeye kujua na ukiwa naye unamdanganya UNAMPENDA yeye tu huna mwanaume mwingine. Kwahiyo huyo mama mkwe yuko sahihi kabisa ndoa yenu haiwezi kudumu kwa sababu bado hujawa tayari kuingia kwenye ndoa. Nimeamua kukueleza ukweli ili ujue tatizo lako najua utajiuliza nimejuaje usishangae huo ndo uwezo niliopewa na wakuu wangu wa kazi. Kama yeyote yupo mwenye swali lolote la kuniuliza anaweza kunipata kwenye Ombeni.charles@gmail.com
 
Nina mchumba yapata miaka minne sasa,mwaka huu ndio tulipanga tufunge ndoa.lakini alipokwenda kwao kutoa taarifa kwao wamemkatalia.mama yake amemwambia kwamba kila anapomuomba mungu wake anaona giza mbele hivyo haitaji mwanae anioe mie.na akasema anatupatia miaka mitatu hiyo ndoa itakuwa imeshavunjika.kutokana na msimamo alioonesha mchumba wangu kwa wazazi wake nimeamua tufunge ndoa lakini nikifikiria upande wa wazazi wake napata hofu.nifanyaje wapendwa?karibuni kwa maoni.

Dada yangu hapo kwenye nyekundu panahusika sana, hayo yaliwahi kunikuta mimi.Nilikuwa na girlfriend ambaye tulidumu kwenye urafiki miaka kama mitano, kwa kuwa tulikuwa tunaishi karibu wazazi wangu waligundua uhusiano wetu. Mama yangu ndie aliyekuwa wa kwanza kuniuliza juu ya mipango yetuya baadaye, mimi sikumficha nikasema tulikuwa tunafikiri kuja kuishi pamoja...basi mama akafunga siku tatu anaomba. Siku ya nne akanijulisha kuwa katika siku zote tatu alizofunga alikuwa anaona giza mbele, Mungu hachelewi kujibu.... baada ya kama mwezi mmoja girlfriend wangu nae akazama kwenye maombi nae akapata same message. Ni vema nawewe ukamshirikisha Mungu hakika utapata jibu lililosahii (haimanishi kwamba asipokuoa hutapata mwingine mzuri kuzidi yeye).
 
Nina mchumba yapata miaka minne sasa,mwaka huu ndio tulipanga tufunge ndoa.lakini alipokwenda kwao kutoa taarifa kwao wamemkatalia.mama yake amemwambia kwamba kila anapomuomba mungu wake anaona giza mbele hivyo haitaji mwanae anioe mie.na akasema anatupatia miaka mitatu hiyo ndoa itakuwa imeshavunjika.kutokana na msimamo alioonesha mchumba wangu kwa wazazi wake nimeamua tufunge ndoa lakini nikifikiria upande wa wazazi wake napata hofu.nifanyaje wapendwa?karibuni kwa maoni.

kama mimi ni wewe, kwa mara ya kwanza baada ya kupokea hiyo taarifa nitaamini kuwa mchumba wangu ananidanganya na anamlisha mama yake maneno ambayo hakuyasema.

uchumba miaka minne??/ kulikuwa na nini hapa? siyo huyo mpenzi wako ndo anatengeneza maneno ya kukuengua wewe?. inawezekana akajifanya eti yeye ameshikilia msimamo wa kuwa lazima akuoe, lakini unalisoma hilo kwa kina kutoka nafsi yake?. yeye amewaambia wazazi wake wamemkatalia, wewe unakuja jamii forums kutaka ushauri, kwanini nawe usiongee na wazazi/walezi wako ukapata ushauri ambao unatoka kwa watu wenye uzito sawia na alikosema yeye?. siidharau jamii forums, nakushauri upeleke hili swala kwa familia, sikia uzoefu na ushauri wao. baadae urudi hapa, kuongezea ya kukusaidia kuchukua uamuzi
 
kwa nini msiishi tu bila ndoa kwa muda?
muone inakuwaje?
wachaga wana kitu inaitwa 'kubariki ndoa'

hutokea hata baada ya miaka kumi na tano kupita ndo wanaingia church...

subiri mzee wa upako aje akusikie ndo utalijua jiji!
 
Kama utaolewa na huyo mchumba wako basi ni bora uolewe. Lakini kama utaolewa na mama wa mcumba wako basi kataa.
Life is like riding a bicycle. To keep your balance you must keep moving
 
We olewaaa! Kwani anakuoa nani mama mkwe au mchumba wako ulompenda! Olewaaaa!
 
nawashukuru sana wanajamvi kwa ushauri wenu,pia naomba niseme kupitia majibu yenu nimejifunza jambo kubwa sana.so tuombeane kama mambo yatakuwa sawa nitarudi jamvini kwa shukrani zaidi.ila naomba niwaweke wazi kwamba huyo mama mkwe nimeonana nae mara moja tu wala sikubahatika hata kuzungumza nae zaid ya salamu.lakini the way alipokea salamu yangu ilitosha mie kujua anawaza nini.kimsingi huwezi kuanza kucooperate na ndugu wa mwanaume kabla hujakaribishwa rasmi hivyo mie siwezi kusema kwamba kuna tabia mbaya wameiona kutoka kwangu,kwakuwa tunaishi mbalimbali sana zaidi ya km1000 kutoka nilipo na walipo wao.labda tuseme kwamba hawataki au kuna mwanamke walikwisha muandaa wao.kuhusu kushirikisha watumishi hata yeye ni mtumishi sasa tumshirikishe mtumishi gani?watumishi wengine wanasababisha maana ya utumishi kupotea kwasababu ya matendo yao.kimsingi kwa hili lililonitokea siwezi kufikiri kwamba kuna kwenda mbingun kwa baadhi ya watumishi.ni unafiki tu umejaa makanisani.mungu awabariki wote mlionipa ushauri.
 
asante mpendwa lakini kumbuka akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Olewa mama! Kwani hiyo kitu si inatamani muhogo wa jang'ombe? Ipeleke ikakakunwe kwa raha zako! Ondoa wasiwasi, ma'mkwe hanachakufanya kama mwanae ameridhia kuishi na wewe!!!!!!!!!!!!!!!!
 
The funny things wamama sijui wapoje kama sista wako hata akimleta mvuta bangi mama yako ata support tu waoane lakini mwanaume akileta binti inakuwaga kasheshe mara nyingi.

Angalia sana coz mahala pako pa kukimbilia mkikosana ni kwa wazazi wake mambo yakifikia shingoni so fanya maamuzi ya kibusara hapo usije kuishia kuambiwa ," SI unaona tulijua tu"
 
Mungu akulaze mahali pema peponi mtoa mada KANJUNJUkifo chako kina maswali mengi kuliko majibu.
Maadui wako wamefanikiwa kukuondoa hapa duniani ila nao watakufuata huko uliko pale mwenyezi Mungu atakapopenda.
 
Funga ndoa hao wazazi walishakula ujana wao. Ndoa ni wewe na mumeo wazazi ukiwasikilza sana utaishia kuosha rungu.
Mukiwa serious wazazi watakubali tu.
 
Masikini R.i.p Kanjunju ndugu zako wangeona uzi huu si ajabu wangehusisha na kifo chako..mungu ailaze roho yako mahali pema peponi.Amina!
 
Funga ndoa hao wazazi walishakula ujana wao. Ndoa ni wewe na mumeo wazazi ukiwasikilza sana utaishia kuosha rungu.
Mukiwa serious wazazi watakubali tu.

Mkuu hii thread ni ya mwaka 2012 na hivi sasa, mleta thread kashatangulia mbele ya haki. Tumwombee apumzike kwa amani.

RIP Kanjunju. Naamini kifo chako hakina mkono wa mama mkwe.
 
Back
Top Bottom