Naomba ushauri kuhusu ajira hii ya ualimu

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
5,818
11,001
Nilianza kazi 2008 na 2011 niliondoka kusoma bila ruhusa. Nimemaliza Bachellor mwaka jana na niliripoti kituoni tangu mwezi wa8 na mshahara nikiwa masomoni ulifutwa.

TSD walinipa shitaka la utoro wa miaka2 na nikajitetea na nilikaguliwa daftari la mahudhurio na sheme mwezi December. Hadi sasa sijajibiwa na mshahara sijapewa. Nikiwa chuoni niliomba ajira mpya na kuna tetesi kua ajira mwezi ujao zinatoka.

Je nikichaguliwa mkoa mpya niende au nibaki hapa bila Salary?
 
graduate unashindwa jitambua,, kazi ipo. Kalime nyanya tu.
 
tushakuchoka tangu mwaka jana mwezi wa 8 huwa unauliza swali hilihili. kwamba hujafanikiwa tu
 
Maswal mengine ni ya kipuuzi. Utabaki vip mahali bila salary kama kuna mahali unaweza kwenda kupata salary? Labda swali lingekuwa nibaki hapa nisubir salary au nikaanze kaz upya? Lakin all in all kama una hakuka watakurejeshea mshahara bora ubaki maana watakulipa na malimbikizo yote yan tangu walipokata hadi sasa iyo itakuwa faida kwako maana pia umri wa kazi utahesabiwa tangu ajira ya mwanzo na utakuwa na faida nyingi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
watu huwa wakipata mkopo wanajisahau sana mkopo niwa miaka 3 na sio ajira kama uko kwenye system na unaenda somea kazi hiyo hiyo ulikurupuka ya nini.
kawaida baada yakufanya kazi miaka 3 unaruhusiwa kwenda masomoni. hata wakikurudishia mshahara watakurudishia ule wa zamani
labda kama watakurudishia then uombe kubadilishiwa muundo upate mshahara wa elimu yko ya sasa. ungeomba ruhusa sahivi ungeshapa daraja 1, na mwakani lq pili
 
Pole sana kijana, mi ushauri wangu endelea kusubiri kama kuna dalili za kusamehewa vinginevyo fanya mambo yako mengine, kwa ajira ulioomba ukiwa chuo itatoka lakini utakapoenda kuripoti kituoni database itakutema kwasababu details zako tayari zipo, hivyo utaambiwa rudi kituoni kwako. kuna jamaa zangu 3 wapo kitaa kwa hilo mambo yalibuma.
 
Kama ulikuwa na check no huwez pata ajira tena!! Kwa nini ulitoroka kituoni??
 
Nilianza kazi 2008 na 2011 niliondoka kusoma bila ruhusa.Nimemaliza Bachellor mwaka jana na niliripoti kituoni tangu mwezi wa8 na mshahara nikiwa masomoni ulifutwa.Tsd walinipa shitaka la utoro wa miaka2 na nikajitetea na nilikaguliwa daftari la mahudhurio na sheme mwezi December.Hadi sasa sijajibiwa na mshahara sijapewa.Nikiwa chuoni niliomba ajira mpya na kuna tetesi kua ajira mwezi ujao zinatoka.Je nikichaguliwa mkoa mpya niende au nibaki hapa bila Salary ??

Ni PM nikupe maujanja
 
Hilo ni tatizo linawakumba vijana wengi kwa sasa ila hakuna linalo shindikana hapa dunia kwanza njia ya kwanza ni hiyo uliyofanya njia ya pili hii ni illegal ila watu kibao ndo wanafanya ivi kama upo tayari ntafute nikupe mchongo
 
Kituoni niliripoti toka wa8 mwaka jana na Tsd ndio wako hatua za mwisho kuhusu hukumu ya utoro wangu
 
Na sijajua Mshahara utarudishwa ama la!sa nahofia kupoteza muda wangu hapa alafu iwe bila bila
 
Pole sana Chukua za kwako changanya na za kwako. Kazi ya mtu aliyegraduate ni kutengeneza ajira ww unataka ushauri.
 
Pole sana Chukua za mbayuwayu changanya na za kwako. Kazi ya mtu aliyegraduate ni kutengeneza ajira ww unataka ushauri.
 
Pole sana Chukua za mbayuwayu changanya na za kwako. Kazi ya mtu aliyegraduate ni kutengeneza ajira ww unataka ushauri kulinda ajira badala ya kubuni uzalishe ajira pole sana mediocre teacher.
 
Na sijajua Mshahara utarudishwa ama la!sa nahofia kupoteza muda wangu hapa alafu iwe bila bila

Ndugu kwanza nakupongeza kwakujiendeleza,kikubwa hapa nakushauri ajira mpya zikitoka wee nenda kapge kazi kuliko kukaa hapo bila kujua hatma yako!
Pili nakushauri kama ukifanikiwa kupata ajira mpya na kuingizwa kwenye payroll bila matatzo ukimalza miaka miwili kazini fanya mpango ukasome masters tena hiyo masters isiwe ya education...mfano kama umesomea kufundisha masomo ya geograph na G.S nakushauri ukapge masters ya HRM (Human Resource Management) au kama umesomea masomo ya economics,commerce na a/c -piga masters ya finance,accounting,procurement,management,project management,au masters ya economics... .
Kama umesomea masomo ya physics unaweza piga masters ya ICT au MBA -ICT,......
Lengo la ushauri wangu nikutaka kukwambia kwamba ualimu haufai kwa hapa Tz!ila utumie ualimu kama daraja lakufikia malengo yako....
——––––★————★–————–-
UTAFANYAJE ILI MWAJILI WAKO AKURUHUSU KUSOMEA KITU TOFAUTI NA UALIMU?
...Kwanza,mwajili wako kamwe hatakuruhusu ukasomee kitu tofauti na ualimu. ..ila unatumia akiri yako kumzuga mwajili.....
Unaomba masters unayoitaka(lets say MSc. Accounting )kwenye chuo X (tuchukulie Mzumbe)alafu unaomba master degree ya ualimu kwenye chuo Z(tuchukulie UDSM)...
Unapotaka kuomba ruhusa unaitanguliza admission form ya UDSM yenye koz ambayo mwajili atakupa ruhusa na ile yenye adm form ya mzumbe (yenye kozi uipendayo sasa)unaiminya......
Mwajili akikuruhusu tu,wewe unaishia zako mzumbe!
Ukimaliza tu kupga MSc yako ya Accounting unafanya mpango wakubadilishiwa kaz kwenye halmashauri yako(recategorization) yaani mwajili wako akutoe kwenye kushika chaki akuweke kwenye kushika pesa na cheque!(aaahaaaah) najua umefurahi jinsi move ilivyoenda)..
Na ukiona kwamba mwajili wako anazingua basi hama halmashauri ( tafuta halmashauri yenye wakuu flexible wanaoweza kukubadilishia kaz hata kwakuwatoa mkwanja-bongo rushwa imejaa ukijifanya msafi utashangaa umebaki peke yako kwenye mataa).....
———–★★-—★––----------––——
Onyo.
Usimwambie mtu yeyote hata awe rafiki yako vpi hapo kazin maana walimu wengi (si ajabu na wewe ukawa mmoja wao)wana wivu sana!hawapendi mwenzao apige bao....
Ukiwaambia tu utashangaa majungu na hata ruhusa hutapata(kiufupi utawekewa bams kwa kila ukifanyacho)
—————★★———–———
Utapata wapi ada yakusoma masters?

Kopa benki.....sio baypot au blue sijui!kule utajuta!utatembea na chupi kichwan kwa jinsi watakavyokutia matatizoni....
Hiz microfinance organs nyingi zinazojinasibu kwamba zinatoa mkopo ndani ya masaa 24 ni wezi...kaa mbali nao!waogope kama ebola ya sieraleon maana kuna ya uganda haina nguvu!(uliona wapi ebola inazibitiwa ndani ya wiki 2 kama si ebola ya uganda?!)
Kakope CRDB,NMB(japo wanalinga na niwaomba rushwa sana-utadhan hawalipwi),Posta bank au NBC....
hizo ndo benki zakukopa.

Ukikopa Milioni 9 tu,utalipa ada full na utabaki na kama 3M zakukusukuma ukamaliza master degree yako bila shida....
NB;- ukikopa fanya ulicholenga!lipa ada! Sio unaanza kumtafuta Fatuma umuonyeshe ulivyomtamu(kama mcharo vile) oooh utajuta na utashangaa ada tu ya 6M inakushinda.
Pia elewa haya yote yanahitaji moyo wakijitoa,ujasiri...moyo wakupambana!laa sivyo utasanda na utakufa kwa chaki....
(Kama una maswali zaidi ni PM)
——-–––★————★–—–
Specialist88.
 
Back
Top Bottom