Naomba mtizamo wako tafadhali....

Asante Hopecomfort, ulivyowaza ndivyo nilivyofikiria kuwa huwa lift inatokea kwa bahati, sasa hili ka kupiga simu kabisa kuomba lifti hapo ndiyo nilipata utata kwa kuzingatia ubinadamu wetu...
Wacha kuazia mabaya kila siku, kumbuka shetani is already a big player...Hapo ndo anapo penda kucheza na lazima katika ndoa iilio tulia anatafuta njia moja, au nyingine kuanzisha kasoro kwenye ndoa hizo...Wasi wasi na Shaka shaka ndo zake hizo.

Kwa kuwa umesha anza kuwa na wasi wasi na ndoa yako, basi sidhani kama utaenda mbali na ndoa yako.

JARIBU KUTUMIA AKILI HAPA NA UJUWE WAZI....MARA NYINGI SANA WATU WAKISHA KUWa WANAFANYA KAZI PAMOJA WANAKUWA KAMA NDUGU.


Kama mme wako ana mchezo mbaya wapande naye gari pamoja au wasipande naye, wakiwa wanamtaka na yeye anawataka wata fanya tu kitu unacho kuwa na wasi wasi nacho.

Weka uaminifu kwenye ndoa yako, acha kurukia anga za shetani huta ziweza.


Ushauri wa kikubwa, ndoa ni kumuamini huyo uliye naye...ukisha kosa uaminfu utabaki kuimba tu kama kuna ndoa.
 
Namuamini sana tu fazaa lakini hii tabia ya hizi simu ndiyo ilinishangaza kidogo nikadhani kuwa haipaswi kuwa hivyo.
Si unajua shetani anapenda watu kama nyie mnao kuwa na wasi wasi hapo ndo anapo puliza moto mpaa unazidi kuwaka shauri yako....Si unajua ma wivu wivu ya kijinga, yanasababisha kuvunjika kwa ndoa.
 
BPM hapa sijakuelewa,kwa hiyo kinachotakiwa asiwe anapiga simu awe anawahi mahali anapoweza kukutana nae? je unadhani kuendekeza lift pia ni sawa? kwanini mtu asijiendee tu ikitokea iwe ni goodluck?

suala si kuendekeza kwa vile wako ofisi moja na route moja hivyo kikawaida haina tatizo sana haijalishi ni jinsia gani... na hii ni kibinadamu
 
Kibali
Mimi nisichoelewa tatizo ni kuwa anatoa lift always au wapewa lift can ran him according to their schedule? My dear kama mchumba has not given you any reason to doubt there is anything more than hizo lift, and he does put you and your needs before hao wapewa lift then you have nothing to worry about. I'll only be concerned kama, unawekwagwa pending akihangaika na wanalift.............................in summary " dont sweat small things!!":smile:
 
Asante Hopecomfort, ulivyowaza ndivyo nilivyofikiria kuwa huwa lift inatokea kwa bahati, sasa hili ka kupiga simu kabisa kuomba lifti hapo ndiyo nilipata utata kwa kuzingatia ubinadamu wetu...

Ulipata nafasi ya kuzungumza na mlengwa kuusu kuchukizwa kwako na tabia hiyo. Kama sio basi fanya ivyo ili usiendelee kuumia zaidi.
 
hata kama wanaishi mtaa mmoja, kuwa na mipaka muhimu sana, hao wadada hawana staha? Kuna privacy pia inatakiwa, huyo kaka awape lifti kwa kiasi.....
 
Namuamini sana tu fazaa lakini hii tabia ya hizi simu ndiyo ilinishangaza kidogo nikadhani kuwa haipaswi kuwa hivyo.

Kazini kuna utani mwingi, kuna kuzoeana kwingi. But for a responsible husband/wife, anahakikisha huu utani na kuzoeana na wafanyakazi wenzake wa jinsia tofauti kunakuwa out of rich of his/her partner. Ni ustaarabu tu, hata kama hamna kinachoendelea zaidi...
 
hivi,nyie si mnafanya kazi? si mnalipwa mshahara mwisho wa mwezi? ushauri wangu ni kwamba, amka/amkeni asubuhi mkatafute daladala/mjichange mkodi teksi mwende kazini na sio kuanza booking ya gari la watu,ikitokea amepita,mpande accidentaly na sio kuweka plan kabisa kwa usafiri wa watu,if u care
 
Kifupi haija kaa vizuri, cha kufanya ongea na mumeo kama wengine walivyokushauri. Umwambie wazi kuwa haufurahii anavyowapa lift hao wadada. Then, usikilizie kama ataendelea au ataacha. Kwa mwanaume anayependa mke wake awe na amani wakati wote ataacha.
 
Petcash rafiki,asante kwa mtizamo wako..lakini binafsi sikatai mtu kusaidiwa lakini unadhani ni sawa hata kama ni jioni wewe kama mume wa mtu uwe na mtu wako permanent wa kumpa lift hata kama mnakaa njia moja?je ni sawa kuwa unapokea simu za kuomba lift halafu huoni shida tena unafanya kuharakisha ili kumpick aliyekuomba lift?
Kwa kweli kama lifti mi ntatoa sana tu na hata mke wangu akitoa sintojiskia vibaya hata kidogo, I want her to be free.
Ila pia mimi kama mwanaume najua nikioa kuna vitu navipenda ila itabidi nicompomise kama havina umuhimu na mwenzi wangu havitaki. So, talk to him you guys were meant for each other I'm sure he'll understand..
 
Namuamini sana tu fazaa lakini hii tabia ya hizi simu ndiyo ilinishangaza kidogo nikadhani kuwa haipaswi kuwa hivyo.
Mmenikumbusha ule wimbo wa lifti.... Kilichonishangaza sio lifti mama watoto, ni tabasamu na vicheko mlivyokuwa navyo ndani ya gari..... Jamani kasema naniliu hapo juu raha ya lifti usiitegemee. Lifti ikishakuwa mazoea kuzaa mengineyo ni rahisi sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom