Edson Carrington
JF-Expert Member
- Oct 30, 2022
- 216
- 634
Habari wakuu
Mimi ni mwanafunzi wa chuo, mwaka wa pili hapa Dar es salaam na ninasomea shahada ya teknolojia ya habari( information Technology) na pia ni loan beneficiary ( mnufaika wa mkopo).
Ninaishi na mzazi wangu mmoja wa kike yaani mama yangu na mdogo wangu, japokuwa kwa sasa nipo mbali nao kidogo kutokana na masomo yangu hivyo nimeamia sehemu nyingine.
Mazingira ya kiuchumi sio mazuri sana nyumbani, kwani mama hana kazi na pia mdogo wangu mdogo anasoma ( darasa la nne), hivyo basi baadhi ya vitu kama msosi, kodi na pesa za hapa na pale zinakuwa changamoto nyumbani.
Sasa mara nyingi huwa boom langu naligawa kwa familia na pia mimi mwenyewe huwa linatakiwa kunikidhi kitu ambacho inakuwa ni changamoto kwani pesa haitoshi.
Sasa kwa huu mwaka wa pili nahitaji baadhi ya vitu mimi kama mwanafunzi kama laptop kwani ni muhimu kwa masomo yangu ya IT na pia kununua simu maana hii simu ninayoitumia imeingia ubovu wa kujizima.
Lakini Changamoto inakuja nafikiria kuhusu hali ya nyumbani ngumu natamani hata nifungue angalau kaduka cha kujiingizia kipato kisaidie nyumbani lakini bado inakuwa changamoto nikifkiria mahitaji yangu binafsi.
Naumia kichwa sana maana nyumbani wahitaji msaada na inaniuma nikipigiwa simu wakiniambia wana njaa lakini pia na mimi nina mahitaji yangu ya muhimu kwa hiyo nashindwa hata kufanya maamuzi.
Tafadhali kwa mwenye ushauri au aliewahi kupitia changamoto kama yangu na akachomoka naomba msaada ndugu zangu kwani naona kama ni mtihani.
Asante.