Naomba msaada wa ufadhili

ABEL NESTORY

Member
Oct 12, 2012
43
34
Habari ndugu zangu, naitwa Abel ni mvulana wa umri wa miaka 28. Nahitaji msaada wenu Tafadhali maana kwa kupitia humu nitaweza kupata hata nafuu maana akili yangu mawazo yangu nahisi yananifanya nakata tamaa japo naamin ninaweza. Nilimaliza Kidato cha nne 2008 na kupata daraja la kwanza (division one) na baadae form six 2012 ambapo sikufanya vzuri (nilipata division 3) kwakuwa kuna shida ilijitokeza na pia nahisi ilichangiwa na kuchagua mchepuo (combination) ambao haukuwa sahihi kwangu. Hapa ninamaanisha kuchagua masomo ambayo sikuwa nayapenda japo nlikuwa nikiyafaulu vizuri, hii ilitokana na ushawishi wa rafiki na kufuata mkumbo wa marafiki. Kwa kuambiwa nikisoma Sayansi ni miaka mingi chuoni, nitaweza kuwa na akili zisizovizuri, mchafu nk, Nikajikuta nasoma (EGM) ambyo ckuwa nmewahi hata kuiwaza maishani. Tangu nilipokuwa Kidato Cha kwanza/ form one nilipenda sana masomo ya PHYSICS, MATHEMATICS, CHEMISTRY na BIOLOGY na nilikuwa nikifaulu kwa alama za juu sana. Ufaulu wangu ulikuwa
Mathematics- B
Chemistry- B
Physics- B
Biology-B
na C kwa masomo yaliyobaki, Kiukweli mpaka sasa nayapenda toka moyoni na naamini ninaweza kufanya maajabu nikipata nafasi. Natamani sana kurudia kufanya mtihani wa Form six kwa PCM au PCB maana naamini ninaweza. Nilipojarbu kuomba ushauri niliambiwa naweza kusoma Diploma katika vyuo vya udaktari ORDINARY DIPLOMA Katika CLINICAL MEDICINE nk kwa kutumia vyeti vya form four. Pia licha ya mambo ya Sayansi napenda sana ufundi. Natamani sana kutimiza ndoto zangu ninaamini na hilo, pia Mungu anisaidie kwa hili. Ninaandika hii post nikijisikia amani maana nahisi kuna kitu nimekipata humu na nimetua mzigo fulani. Nitashukuruni sana ndugu zangu. Kwasasa ninafanya kazi katika kiwanda fulani na vitu vnavyotokea vinanifanya najuta sana kama unavyoelewa kazi za watu.
OMBI LANGU kwa wadau na ndugu zangu humu. Ninahtaji na ninaomba kufahamu yafuatayo

1/ Je kuna uwezekano wa kupata mtu wa kunisiadia kunisomesha???

2/ Je nawezaje kupata wafadhili kama kuna uwezekano huo??

3/ Nahitaji msaada zaidi wa mawazo maana nawaza sana nmeharibu mwelekeo wa maisha yangu na ndoto zangu. Inafikia kipindi sihitaji kuonana na mtu yeyote niliyesoma naye awali kitu ambacho nahisi ni tatzo la kisaikolojia.

Msaada please hata kwa mawazo mengine ya kunijenga na ushauri ili nitulie na kupata njia sahihi ambayo naamini nitaitendea haki. Mbarikiwe wote na kazi njema na masomo mema kwa wanafunzi.
NDUGU ZANGU, TUWE MAKINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI ILI TUSIJE TUKAJUTA KAMA MIMI.
 
Inawezeka kupata vyuo vya afya na ukasona kozi unayo itaka maana ulikuwa na matokeo mazur ila tatizo ambalo litabakia kikwazo kwako ni kuhusu Hela ya kumudu masomo ya afya maana ngazi za certificate na diploma hawatoi mkopo au ufadhili wowote ila fanya kama unaomba nafasi kupitia NACTE na mungu atakusaidia utatimiza ndoto zako
 
Labda nijaribu mkuu ila shida yngu pia kwenye pesa hapo japo Mungu ni mwema. Ila shida nyingine ni kwamba vyuo vya serikali wanalimit muda uliomaliza Form four. Na inatakiwa uingie katika vyuo binafsi ambavyo kwa upande wangu nahisi ni vgumu sana ktokana na ada yao kuwa juu.
 
Acha kupoteza muda,nani kakuambia kuwa ndoto za watu huwa zinatimia hapa bongo?
 
Tang'ana mkuu ndiyo maana nimeandika hii post ili nishauriwe huko ndoto zinakotimia boss. Siyo vibaya ukanipa mwangaza nielewe
 
ABEL NESTORY sijui uko vipi kiimani, je usha kaa chini ukaongea na Mungu kuhusu hili, mara nyingi sisi binadamu tumekuwa na matakwa yetu katika maisha, lakini katika sala ya Baba yetu, kuna mahali panasema, let your will be done ( mathew 6:10). Je ushawahi kukaa na kutafakari ( spiritual) what is God will to you? katika Luke 6:42 B, Yesu wakati anaendea mateso alisema "however not my will, but yours be done.” . katika mathew 6:10 biblia inasema "let your will be done also in the earth, just as it is in Heaven". Mungu ana plan na maisha ya kila mtu, shida nikuwa tumekuwa tukiangukia kwenye plan zetu za kibinadamu.
 
Giusepe thank you very much my friend. Nmekaa kuhusu hilo namuamini sana Mungu na ndiyo maana sitaki kukata tamaa. Na pia nahitaji hata msaada wa kiroho pia. Naamini Mungu yupo na atanisaidia. I have stress, it hurt my soul and i feel like am loosing something.
 
Na pia kama mwemzetu alivyo kwambia usije kusahau kumuomba muumba wako hata siku moja maana yeye ndiye muweza wa yote but kuna hii taasisi ya MKAPA FOUNDATION ilikuwa inatoa udhamin sijui waliishia wapi
 
Pole sana mkuu, cha msingi usikate tamaa.
Ushauri wangu kwako na wengine wa namna yako: "Unaposhindwa kufanya unachokipenda ni vyema ukapenda unachokifanya". Watu wengi wamefanikiwa kwa kupenda wakifanyacho hata kama kipo nje ya ndoto zao.
 
ABEL NESTORY sijui uko vipi kiimani, je usha kaa chini ukaongea na Mungu kuhusu hili, mara nyingi sisi binadamu tumekuwa na matakwa yetu katika maisha, lakini katika sala ya Baba yetu, kuna mahali panasema, let your will be done ( mathew 6:10). Je ushawahi kukaa na kutafakari ( spiritual) what is God will to you? katika Luke 6:42 B, Yesu wakati anaendea mateso alisema "however not my will, but yours be done.” . katika mathew 6:10 biblia inasema "let your will be done also in the earth, just as it is in Heaven". Mungu ana plan na maisha ya kila mtu, shida nikuwa tumekuwa tukiangukia kwenye plan zetu za kibinadamu.
duuh hii kweli jamii forum ..ukiomba ushauri utapata shauri zote za kiroho kimwili...kifikra au kiakili...namaanisha spiritual.... physical and mental Advice.... penda xana hii mimi
 
Habari ndugu zangu, naitwa Abel ni mvulana wa umri wa miaka 28. Nahitaji msaada wenu Tafadhali maana kwa kupitia humu nitaweza kupata hata nafuu maana akili yangu mawazo yangu nahisi yananifanya nakata tamaa japo naamin ninaweza. Nilimaliza Kidato cha nne 2008 na kupata daraja la kwanza (division one) na baadae form six 2012 ambapo sikufanya vzuri (nilipata division 3) kwakuwa kuna shida ilijitokeza na pia nahisi ilichangiwa na kuchagua mchepuo (combination) ambao haukuwa sahihi kwangu. Hapa ninamaanisha kuchagua masomo ambayo sikuwa nayapenda japo nlikuwa nikiyafaulu vizuri, hii ilitokana na ushawishi wa rafiki na kufuata mkumbo wa marafiki. Kwa kuambiwa nikisoma Sayansi ni miaka mingi chuoni, nitaweza kuwa na akili zisizovizuri, mchafu nk, Nikajikuta nasoma (EGM) ambyo ckuwa nmewahi hata kuiwaza maishani. Tangu nilipokuwa Kidato Cha kwanza/ form one nilipenda sana masomo ya PHYSICS, MATHEMATICS, CHEMISTRY na BIOLOGY na nilikuwa nikifaulu kwa alama za juu sana. Ufaulu wangu ulikuwa
Mathematics- B
Chemistry- B
Physics- B
Biology-B
na C kwa masomo yaliyobaki, Kiukweli mpaka sasa nayapenda toka moyoni na naamini ninaweza kufanya maajabu nikipata nafasi. Natamani sana kurudia kufanya mtihani wa Form six kwa PCM au PCB maana naamini ninaweza. Nilipojarbu kuomba ushauri niliambiwa naweza kusoma Diploma katika vyuo vya udaktari ORDINARY DIPLOMA Katika CLINICAL MEDICINE nk kwa kutumia vyeti vya form four. Pia licha ya mambo ya Sayansi napenda sana ufundi. Natamani sana kutimiza ndoto zangu ninaamini na hilo, pia Mungu anisaidie kwa hili. Ninaandika hii post nikijisikia amani maana nahisi kuna kitu nimekipata humu na nimetua mzigo fulani. Nitashukuruni sana ndugu zangu. Kwasasa ninafanya kazi katika kiwanda fulani na vitu vnavyotokea vinanifanya najuta sana kama unavyoelewa kazi za watu.
OMBI LANGU kwa wadau na ndugu zangu humu. Ninahtaji na ninaomba kufahamu yafuatayo

1/ Je kuna uwezekano wa kupata mtu wa kunisiadia kunisomesha???

2/ Je nawezaje kupata wafadhili kama kuna uwezekano huo??

3/ Nahitaji msaada zaidi wa mawazo maana nawaza sana nmeharibu mwelekeo wa maisha yangu na ndoto zangu. Inafikia kipindi sihitaji kuonana na mtu yeyote niliyesoma naye awali kitu ambacho nahisi ni tatzo la kisaikolojia.

Msaada please hata kwa mawazo mengine ya kunijenga na ushauri ili nitulie na kupata njia sahihi ambayo naamini nitaitendea haki. Mbarikiwe wote na kazi njema na masomo mema kwa wanafunzi.
NDUGU ZANGU, TUWE MAKINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI ILI TUSIJE TUKAJUTA KAMA MIMI.
Ktk maisha lazma upitie changamoto nyingi na jitahidi kuzitatua kwa kujiamini kwanza mwenyewe juu ya mikajati uliyopanga ktk maisha yako May GOD bless you.
 
Back
Top Bottom