King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,718
- 68,714
Mpe big up dogo wako kwa kuezeka math na chemistry,cha msingi na sekondari omba tu uahamisho!
Kaka mimi binafsi siamini kama shule ni kigezo cha mtu kufanya vizuri katika mitihani sanasana hizi shule za serikali zote ni sawa tofauti ni majengo na maeneo zilipo pia idadi rukuki ya walimu watoro na wasio kuwa na dhamira ya kusaidia wanafunzi.
Labda niende kwa mifano utanielewa, mfano wa shule zinazofanya vizuri kwa hapa Dar katika masomo ya sayansi ni kama hakuna ila kuna baadhi ya wanafunzi wa sayansi hizo hizo shule za serikali wanafanza vizuri kuwazidi hata wa huko boarding schools, so it all about self commitment. Mwambie dogo ajitume na kwa kuwa ameshasoma hayo masomo ni rahisi kufanya vizur ila zaidi na zaidi asome sana past papers na ajue syllabus ya sasa iko vipi. Pia apende sana kufanya mitihani katika vituo vyenye ushindani kama kwa MANYILIZU na penginepo. Kingine kuama combination ukiwa shule ni kitu kirahisi kwa hilo asiwaze chochote na namshauri asome PCM just the way he wanted.
Mwisho, ningependa nikushauri na wewe pia kuwa usikariri maisha, kwakuwa umeshazoea kuona shule ina vilaza basi hutaki mabadiliko katika hiyo shule, huyo mdogo wako ndio anaweza kwenda kuweka hiyo heshima katika hiyo shule na akafanya wanafunzi wenzake wenye kujitambua kupata ushindani na wakafanya vizuri wote kwa ujumla. AENDE HAPOHAPO CHANG'OMBE NA USIMPOTEZEE MDA WAKE KUANZA KUFOCUS KWENYE KUHAMA NA KUACHA MAJUKUMU YAKE YA KIMSINGI YA KUSOMA.
Mkuu, thanx for contribution!!
Hata hivyo, naomba nitofautiane na wewe kidogo kuhusu kama shule inachangia matokeo ya mtu! Asikudanganye mtu, shule inachangia sana...almost 70%! Labda hapa niseme jambo moja! Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, shule nyingi za serikali zenye majina makubwa zimebaki majina tu....sina shaka kabisa katika hilo! Hata hivyo, hoja yangu hapa ni kwamba, pamoja na shule hizo kutokuwa na walimu sawa na shule zingine, lakini ile mwanafunzi kukutana na wanafunzi sawa na yeye kunaongeza chachu fulani! Nakumbuka wakati nipo A-Level pale Tambaza, washikaji wa Ilboru na Mzumbe walikuwa hawataki kupiga tution na sisi
kama tukichukua mawazo yako na kuyaweka katika uhalisia wa mambo basi kusingekuwa na div 1 ama div 2 katika shule za kata, huyo mdogo wako yupo mjini na akitumia hii nafasi ya kuwa mjini vizuri basi naamini atapata matokeo mazuri kwani kuna access zote za materials na sehemu nyingi za kufanya practicals hasa kwenye fizikia na kemia. Hao wanafunzi wa mzumbe, ilboru, kibaha na tabora boys wanafanya vizuri kwa kuwa wanajaa sana katika maeneo ya tuition siku za rikizo tofauti na wanafunzi wa mashule mengine na ndio sababu ya kufanya vizuri na hawafuniki madaftari yao kamwe mpaka waelewe kila kitu.
Shule za serikali sio kama shule binafsi, dogo kama akipenda anaweza kuwa anafanya discussion na wanafunzi wa shule zingine ni kujipanga tu na kutumia muda wake katika masomo na yeye atakuwa shuhuda kwako kama shule sana sana hizi za serikali sio ishu ni jitihada binafsi za mwanafunzi. Kuna kijana mmoja alichaguliwa mzumbe alipomaliza kidato cha nne hakwenda kwa sababu kuwa maisha ya pale si mazuri na akaamia benjamin mkapa high school na pale benja kuna mabishoo ila yeye alikuwa anatekeleza wajibu wake wa kula misuli na kufanya majaribio ya mitihani nje ya shule kujiweka fiti. Alichomoka na div 1.4 na alikuwa anawapa wenzake morali ya kusoma na baadhi yao walijitahidi kiaina. Alikuwa anasoma PCB. Hakuna mtu asiyeweza kufaulu ila ni kutotimiza wajibu wa kusoma tu.
Sa kwa points hzo we ulitaka apangwe wapi labda?
hii key point sana ndugu yangu tunajua maana ake wengine
Shule ambazo wenye pass kama zake, tena wengine wenye pass ndogo kuliko yeye wameenda! Shule kama vile Pugu, Minaki, Azania, Moshi Tech and the like....hata kama nazo zimebaki majina; lakini social satsfaction inaweza kumfanya afanye vizuri zaidi. Hata kama zimebaki majina, lakini kukutana na watu wenye uwezo sawa na wake kunaongeza competition!
kuna wengine hawaju kusoma tosa,mzumbe,tabora,pugu kuna umuhimu gani? Hivi hawajiulizi kwa nini vyuoni watu wanaosoma science wengi ni waliotoka shule za boarding za serikali kwa wavulana hata kama hazina walimu?
mimi ni mmoja wa wahanga wa tatizo la uhaba walimu kwenye shule za SCIENCE hasa hizi ambazo wanaenda wavulana naweza zungumzia experience yangu hapa nimesoma MINAKI -PCM niliingia pale hali ilikuwa mbaya sana kwani kulikuwa na uhaba walimu wa masomo yoote na mimi nilikuwa nimetoka DAY SCHOOL NA NI MCHANGANYIKO halafu ilikuwa na walimu wakutosha kwa kweli niona sasa ONE yangu ya o-level inaenda kugeuka ZERO a-level .. lakini baada ya kukaa na kutafakari na kusoma mazingira kwa kina nikagundua hakuna namna nikusoma na ntasomaje jibu likawa simply nikuwa social na washikaji maana wengi walikuwa wamekataa mapindi walipo maliza O-LEVEL na kwa kuwa BOARDING SCHOOL KUNAKUJA watu wa mikoa tofauti uwezo tofauti COMB tofauti hii CLOSED LOOP nzuri sana ukiitumia kwani unapata morali ya kusoma kwa bidii kwani utakutana na changamoto ya wapiga misuli WASONGO NA WAKESHAJI umuhimu ya shule kama MINAKI,PUGU,TOSAMAGANGA,TANGA TECH ,USAGARA,GALANOS , MOSHI TECH , NA SHULE ZA MUDA MREFU ZA BOARDING ZINAKUJENGA SANA KUJITEGEMEA KIMSULI ZAIDI NA UNAKUWA FOCUSED SANA NA SHULE UNAEPUKANA NA ADHA NYINGI SANA ZA DAY ...Seriously, dogo inabidi ahamishwe. Kusoma boarding kutamsaidia kumjenga kwa sababu atapata muda wa kutosha wa kusoma, kudiscuss na wenzake hata kama hakuna walimu, usumbufu wa usafiri na kutochanganyika na mademu. Akirudi likizo anapiga mapindi. Lakini kwa kusema aendelee kusoma chang'ombe sishauri. Isitoshe kwa mchepuo kama PCM lazima ataumia six. Kwa kuanzia inabidi uende ukacheck nafasi na ukakutane na walimu wakuu wa shule unazotaka ahamie. Kuhama ni simple 2.
jamani tuwe honest kwenye hili wale waliosoma day za serikali pcm wenye matokeo mazuri watuambie kabisa maana mzije mkareta ligi isiyo na tija nina mifano mingi na ninajua weight ya pcm ukweli ni kwamba utatumia nguvu nyingi sana kusoma hii comb in day schools tena hizi za kata ukaambulia matokeo ya kawaida hata kama uko vizuri kichwanikwa hiyo unadhan hapo chang'ombe hakuna watu waliofaulu kama yeye? Mawazo kama yako yatampoteza, na wengi huwa wanaangukia pua pamoja na kuama.
Kumuamisha mbona inawezekana, mwache akaripot huku mnashughulikia uhamisho., moja ya sababu ya uhamisho iwe amepangiwa day na dar hana ndugu wa kuishi nae. Kuna mdogo wangu alishawahi kuhama kwa mtindo huo ila ye ilikuwa O'level
jamani tuwe honest kwenye hili wale waliosoma day za serikali pcm wenye matokeo mazuri watuambie kabisa maana mzije mkareta ligi isiyo na tija nina mifano mingi na ninajua weight ya pcm ukweli ni kwamba utatumia nguvu nyingi sana kusoma hii comb in day schools tena hizi za kata ukaambulia matokeo ya kawaida hata kama uko vizuri kichwani
kuna wengine hawaju kusoma tosa,mzumbe,tabora,pugu kuna umuhimu gani? Hivi hawajiulizi kwa nini vyuoni watu wanaosoma science wengi ni waliotoka shule za boarding za serikali kwa wavulana hata kama hazina walimu?
kwa hiyo unadhan hapo chang'ombe hakuna watu waliofaulu kama yeye? Mawazo kama yako yatampoteza, na wengi huwa wanaangukia pua pamoja na kuama.