Naomba Mchango wa Mawazo, Nahisi Hatukutendewa Haki!!

Kaka mimi binafsi siamini kama shule ni kigezo cha mtu kufanya vizuri katika mitihani sanasana hizi shule za serikali zote ni sawa tofauti ni majengo na maeneo zilipo pia idadi rukuki ya walimu watoro na wasio kuwa na dhamira ya kusaidia wanafunzi.

Labda niende kwa mifano utanielewa, mfano wa shule zinazofanya vizuri kwa hapa Dar katika masomo ya sayansi ni kama hakuna ila kuna baadhi ya wanafunzi wa sayansi hizo hizo shule za serikali wanafanza vizuri kuwazidi hata wa huko boarding schools, so it all about self commitment. Mwambie dogo ajitume na kwa kuwa ameshasoma hayo masomo ni rahisi kufanya vizur ila zaidi na zaidi asome sana past papers na ajue syllabus ya sasa iko vipi. Pia apende sana kufanya mitihani katika vituo vyenye ushindani kama kwa MANYILIZU na penginepo. Kingine kuama combination ukiwa shule ni kitu kirahisi kwa hilo asiwaze chochote na namshauri asome PCM just the way he wanted.

Mwisho, ningependa nikushauri na wewe pia kuwa usikariri maisha, kwakuwa umeshazoea kuona shule ina vilaza basi hutaki mabadiliko katika hiyo shule, huyo mdogo wako ndio anaweza kwenda kuweka hiyo heshima katika hiyo shule na akafanya wanafunzi wenzake wenye kujitambua kupata ushindani na wakafanya vizuri wote kwa ujumla. AENDE HAPOHAPO CHANG'OMBE NA USIMPOTEZEE MDA WAKE KUANZA KUFOCUS KWENYE KUHAMA NA KUACHA MAJUKUMU YAKE YA KIMSINGI YA KUSOMA.

Mkuu, thanx for contribution!!
Hata hivyo, naomba nitofautiane na wewe kidogo kuhusu kama shule inachangia matokeo ya mtu! Asikudanganye mtu, shule inachangia sana...almost 70%! Labda hapa niseme jambo moja! Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, shule nyingi za serikali zenye majina makubwa zimebaki majina tu....sina shaka kabisa katika hilo! Hata hivyo, hoja yangu hapa ni kwamba, pamoja na shule hizo kutokuwa na walimu sawa na shule zingine, lakini ile mwanafunzi kukutana na wanafunzi sawa na yeye kunaongeza chachu fulani! Nakumbuka wakati nipo A-Level pale Tambaza, washikaji wa Ilboru na Mzumbe walikuwa hawataki kupiga tution na sisi!!!!!! Walikuwa wanaona kama mabishoo flan hivi!!!! Likewise, nakumbuka discussion zetu za kimtaa tulikuwa tunafanyia pale DSA ( siku hizi wanaita TIA)! Basi nakumbuka, wakati akina sie tulikuwa tunaingia DSA saa 2 usiku na kutoka saa 4 au 5 usiku, kuna washikaji wa Ilboru walikuwa wanaingia wakati sisi tunatoka halafu wanatoboa (yaani hadi asubuhi)!!!!!! Hii maana yake ni kwamba kila shule ina kasi yake na ili uende sambasamba na wenzako ni lazima uendane na hiyo kasi!!! Vilevile nakumbuka wakati tukiwa Form III (St Anthony), kuna mshikaji mmoja alihamia kutoka Kilimanjaro (sifahamu shule gani)! Sasa siku moja nikiwa na gwanda za shule, nikakutana na jamaa mmoja akaniuliza endapo namfahamu huyo mshikaji! Nikamjibu, ndio namfahamu kv tulikuwa moja. Yule jamaa wacha aanze kumwagia sifa huyo mshikaji ambae alihamia shuleni kwe2 kwamba ni mkali ile mbaya...yaani huko alikotoka alikuwa anawaburuza kishenzi! Binafsi, nilishangaa ile mbaya kv sizani hata kama alikuwepo ktk 20 bora mle ndani!!! Hii maana yake nini, mshikaji alikuwa mkali kwenye darasa la vilaza! Hivyo basi, shule inasaidia sana kutokana na morali ya shule husika!
 
Mkuu, thanx for contribution!!
Hata hivyo, naomba nitofautiane na wewe kidogo kuhusu kama shule inachangia matokeo ya mtu! Asikudanganye mtu, shule inachangia sana...almost 70%! Labda hapa niseme jambo moja! Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, shule nyingi za serikali zenye majina makubwa zimebaki majina tu....sina shaka kabisa katika hilo! Hata hivyo, hoja yangu hapa ni kwamba, pamoja na shule hizo kutokuwa na walimu sawa na shule zingine, lakini ile mwanafunzi kukutana na wanafunzi sawa na yeye kunaongeza chachu fulani! Nakumbuka wakati nipo A-Level pale Tambaza, washikaji wa Ilboru na Mzumbe walikuwa hawataki kupiga tution na sisi

kama tukichukua mawazo yako na kuyaweka katika uhalisia wa mambo basi kusingekuwa na div 1 ama div 2 katika shule za kata, huyo mdogo wako yupo mjini na akitumia hii nafasi ya kuwa mjini vizuri basi naamini atapata matokeo mazuri kwani kuna access zote za materials na sehemu nyingi za kufanya practicals hasa kwenye fizikia na kemia. Hao wanafunzi wa mzumbe, ilboru, kibaha na tabora boys wanafanya vizuri kwa kuwa wanajaa sana katika maeneo ya tuition siku za rikizo tofauti na wanafunzi wa mashule mengine na ndio sababu ya kufanya vizuri na hawafuniki madaftari yao kamwe mpaka waelewe kila kitu.

Shule za serikali sio kama shule binafsi, dogo kama akipenda anaweza kuwa anafanya discussion na wanafunzi wa shule zingine ni kujipanga tu na kutumia muda wake katika masomo na yeye atakuwa shuhuda kwako kama shule sana sana hizi za serikali sio ishu ni jitihada binafsi za mwanafunzi. Kuna kijana mmoja alichaguliwa mzumbe alipomaliza kidato cha nne hakwenda kwa sababu kuwa maisha ya pale si mazuri na akaamia benjamin mkapa high school na pale benja kuna mabishoo ila yeye alikuwa anatekeleza wajibu wake wa kula misuli na kufanya majaribio ya mitihani nje ya shule kujiweka fiti. Alichomoka na div 1.4 na alikuwa anawapa wenzake morali ya kusoma na baadhi yao walijitahidi kiaina. Alikuwa anasoma PCB. Hakuna mtu asiyeweza kufaulu ila ni kutotimiza wajibu wa kusoma tu.
 
simply.. haya mambo ya kupangiwa shule nzuri ni bahati ya mtu, kuna watu nilisoma nao walipata div nzuri lkn walipelekwa combi ambazo hawakuzichagua. Kuna a-level classmates tulichagua shule moja combi moja na wao waliperform vizuri zaidi yangu na kati ya 12 tulichaguliwa wawili tu kwenda hiyo shule maarufu tz
 
Sa kwa points hzo we ulitaka apangwe wapi labda?

wewe one 16 a ya math, chemistry unipeleke shule ya kata? Usiombe mziki wa pcb mdogo angu! Bado hajagombana na daladala,home usumbufu na shida nyingine za kusoma mchanganyiko! Bado akili yako haijachanganywa na wadada wanaotembea uchi. Nimejisikia vibaya kwa nafsi yangu, this is not fair! Kwa fikra iliyonijia chap chap kama mtashindwa kumhamisha huyo dogo anaweza akasoma kutimiza muda tu aafu yakaja mambo ya kuanza kutumia cheti cha f4. Mtafutieni shule nzuri asije waangushia lawama zote nyie na wizara!
 
Seriously, dogo inabidi ahamishwe. Kusoma boarding kutamsaidia kumjenga kwa sababu atapata muda wa kutosha wa kusoma, kudiscuss na wenzake hata kama hakuna walimu, usumbufu wa usafiri na kutochanganyika na mademu. Akirudi likizo anapiga mapindi. Lakini kwa kusema aendelee kusoma chang'ombe sishauri. Isitoshe kwa mchepuo kama PCM lazima ataumia six. Kwa kuanzia inabidi uende ukacheck nafasi na ukakutane na walimu wakuu wa shule unazotaka ahamie. Kuhama ni simple 2.
 
Shule ambazo wenye pass kama zake, tena wengine wenye pass ndogo kuliko yeye wameenda! Shule kama vile Pugu, Minaki, Azania, Moshi Tech and the like....hata kama nazo zimebaki majina; lakini social satsfaction inaweza kumfanya afanye vizuri zaidi. Hata kama zimebaki majina, lakini kukutana na watu wenye uwezo sawa na wake kunaongeza competition!

kwa hiyo unadhan hapo chang'ombe hakuna watu waliofaulu kama yeye? Mawazo kama yako yatampoteza, na wengi huwa wanaangukia pua pamoja na kuama.
 
kuna wengine hawaju kusoma tosa,mzumbe,tabora,pugu kuna umuhimu gani? Hivi hawajiulizi kwa nini vyuoni watu wanaosoma science wengi ni waliotoka shule za boarding za serikali kwa wavulana hata kama hazina walimu?


Seriously, dogo inabidi ahamishwe. Kusoma boarding kutamsaidia kumjenga kwa sababu atapata muda wa kutosha wa kusoma, kudiscuss na wenzake hata kama hakuna walimu, usumbufu wa usafiri na kutochanganyika na mademu. Akirudi likizo anapiga mapindi. Lakini kwa kusema aendelee kusoma chang'ombe sishauri. Isitoshe kwa mchepuo kama PCM lazima ataumia six. Kwa kuanzia inabidi uende ukacheck nafasi na ukakutane na walimu wakuu wa shule unazotaka ahamie. Kuhama ni simple 2.
mimi ni mmoja wa wahanga wa tatizo la uhaba walimu kwenye shule za SCIENCE hasa hizi ambazo wanaenda wavulana naweza zungumzia experience yangu hapa nimesoma MINAKI -PCM niliingia pale hali ilikuwa mbaya sana kwani kulikuwa na uhaba walimu wa masomo yoote na mimi nilikuwa nimetoka DAY SCHOOL NA NI MCHANGANYIKO halafu ilikuwa na walimu wakutosha kwa kweli niona sasa ONE yangu ya o-level inaenda kugeuka ZERO a-level .. lakini baada ya kukaa na kutafakari na kusoma mazingira kwa kina nikagundua hakuna namna nikusoma na ntasomaje jibu likawa simply nikuwa social na washikaji maana wengi walikuwa wamekataa mapindi walipo maliza O-LEVEL na kwa kuwa BOARDING SCHOOL KUNAKUJA watu wa mikoa tofauti uwezo tofauti COMB tofauti hii CLOSED LOOP nzuri sana ukiitumia kwani unapata morali ya kusoma kwa bidii kwani utakutana na changamoto ya wapiga misuli WASONGO NA WAKESHAJI umuhimu ya shule kama MINAKI,PUGU,TOSAMAGANGA,TANGA TECH ,USAGARA,GALANOS , MOSHI TECH , NA SHULE ZA MUDA MREFU ZA BOARDING ZINAKUJENGA SANA KUJITEGEMEA KIMSULI ZAIDI NA UNAKUWA FOCUSED SANA NA SHULE UNAEPUKANA NA ADHA NYINGI SANA ZA DAY ...
AMINI NIMESOMA MINAKI ILIKUWA NA UHABA WA WALIMU KITU KILOCHOOVUNJA MOYO MWANZONI LAKINI HICHO KITU NDICHO KILICHO NI MOVITATE KUJISOMEA KWA NGUVU KWA KUONA WENZANGU WANAVYO KAMUA KWA HASIRA NA SASA MIMI NI MHANDISI
 
kwa hiyo unadhan hapo chang'ombe hakuna watu waliofaulu kama yeye? Mawazo kama yako yatampoteza, na wengi huwa wanaangukia pua pamoja na kuama.
jamani tuwe honest kwenye hili wale waliosoma day za serikali pcm wenye matokeo mazuri watuambie kabisa maana mzije mkareta ligi isiyo na tija nina mifano mingi na ninajua weight ya pcm ukweli ni kwamba utatumia nguvu nyingi sana kusoma hii comb in day schools tena hizi za kata ukaambulia matokeo ya kawaida hata kama uko vizuri kichwani
 
Kumuamisha mbona inawezekana, mwache akaripot huku mnashughulikia uhamisho., moja ya sababu ya uhamisho iwe amepangiwa day na dar hana ndugu wa kuishi nae. Kuna mdogo wangu alishawahi kuhama kwa mtindo huo ila ye ilikuwa O'level

Hivyo alikuwa anasoma shule gani vile na alikuwa anakaa wapi vile wakati anasoma O'level!!!?
 
jamani tuwe honest kwenye hili wale waliosoma day za serikali pcm wenye matokeo mazuri watuambie kabisa maana mzije mkareta ligi isiyo na tija nina mifano mingi na ninajua weight ya pcm ukweli ni kwamba utatumia nguvu nyingi sana kusoma hii comb in day schools tena hizi za kata ukaambulia matokeo ya kawaida hata kama uko vizuri kichwani

watu ni wabishi kwa sababu wanatakiwa kubisha. Watu wanaopangiwa tabora boys wengi sana huwa wanawaomba ndugu zao wawahamishe kwa kisingizio haina walimu. Wakishajimingo na wana huwa wanasahau kabisa suala la kuhama na wanafaulu vizuri tu. Hiyo shule ni day, ya kata, mchanganyiko na walimu wenyewe ndo hawa wasiolipwa mishahara,unategemea atatoka. Science sio arts jamani ambayo watu wanasoma mwaka mmoja na kufaulu! Dogo anahitaji close contact na washkaji ili ajue namna washkaji wanavyofight jangwani na kuchomoka.
 
kuna wengine hawaju kusoma tosa,mzumbe,tabora,pugu kuna umuhimu gani? Hivi hawajiulizi kwa nini vyuoni watu wanaosoma science wengi ni waliotoka shule za boarding za serikali kwa wavulana hata kama hazina walimu?

Mkuu, wengi hawajui umuhimu wa hiyo kitu....wengi wanahisi ninaposema shule mzuri, fikira zao wanazani namaanisha shule ambazo zina walimu wazuri...la hasha! Good enough, angalau wewe na Mganga Mkweli ndio mmenielewa namaanisha nini!! Binafsi, mie sijawahi soma boarding...lakini nafahamu umuhimu wa hizo shule....SPIRIT! Shule kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha, Tabora Boys, Tosa, Ifunda, Moshi Tech, and the like, zina-mantain particular spirit ambazo mwanafunzi kama unahitaji kuwa among the best ni lazima u-cope na hiyo spirit!!
 
kwa hiyo unadhan hapo chang'ombe hakuna watu waliofaulu kama yeye? Mawazo kama yako yatampoteza, na wengi huwa wanaangukia pua pamoja na kuama.

Labda tu nikuambie jambo moja; mimi si mtu wa kukurupuka....siwezi ongea kitu bila kukifanyia utafiti!! Ningekuwa mtu wa kukurupuka, ningeipa BIG UP hiyo shule hasa ukizingatia hapo hapo kuna chuo cha ualimu....in short, hamna kitu pale! Hata kama sio rasmi, kimsingi Chang'ombe ni shule ya Kata!!! By the way, pale kulikuwa na HGL(K) tu, na ndipo wakaanzisha na hiyo PCB...bila shaka wana-DUCE wapate sehemu ya kufanyia practical. Na kutoka shule aliyosoma dogo; ni yeye peke yake ndie amepelekwa hiyo hule ya kata....tuache ushindani usio na maana. Fahari ya mwanafunzi aliyefanya vizuri ni kwenda shule inayolingana na ufaulu wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom