Naomba kupata msaada wa kisheria kidogo kwenye hili

thephilanthropist

Senior Member
Aug 28, 2020
171
262
Kuna jamaa mmoja hapa mtaani aliniuzia kitu flani kama miezi miwili hivi iliopita. Tuliuziaba tu kienyeji hapakua na shadihi yoyote wala kuandukiana. Sasa hicho kitu ambacho aliniuzia nikataka kukisafirisha kukipeleka mkoa X nikakiuze nikawa natafuta mtu wa kumpa aende nacho.

Nikaja kumpa yuleyule alieniuzia nikachanganisha na mzigo mwengine ambao nimenunua sehemu nyengine nikamkabizi, Vile Vile wakati namkabizi hapakua na shahidi yoyote yule. Jamaa akafanya tamaa akapotea nao akaenda kuuza, mzigo wote wenye samani kama ya sh Milioni moja na laki 2.

Kwa msaada wa Jeshi la polisi yule jamaa akadakwa na muda si mrefu tutapanda mahakamani, Ila Baadae nikaja kujua kua ule mzigo ambao aliniuzia mimi haukua wake aliazimwa na mtu mwengine. Uyo jamaa nae kamfungulia huyo mwizi kesi nae anampeleka mahakani. Ushahidi ambao mimi niko nao ni Screenshot za sms ambazo alichat na mdogo wangu (mtu ambae alitakiwa amkabizi huo mzigo).

Katika hizo Screenshot kwa Muhtasari, mdogo wangu anamuambia, "Mimi ni mtu fulani kuna mzigo unatakiwa kunipatia" , Jamaa anakiri kweli nimepewa mzigo nisubiri nikifika hapo nitakukabizi, jamaa baadea akaanza janja janja zake, akasema nilipofika hapo nimepata Zarura ya ghafla kuna mtu nakutumia no zake nimemuachia huo mzigo, Mdogo wangu akachat na huyo jamaa ambazo nazo Screenshot zake niko nazo. Jamaa anasema kweli nimepewa mzigo ila niko na kazi kwanza wewe nenda nitakutafuta Baadae. Jamaa akawa ndio kapotea. Kumbe jamaa alioachiwa mzigo hakuachiwa, ila ni kwamba alimpanga tu, ili mimi nione kua mzigo Kakimbia nao huyo jamaa alieachiwa.

Ushahidi mwengine nilionao ni kwamba jamaa juzi nimempigia simu nikamrecord, tukaongea ananiambia Sauti yake inasikika kabisa ananiambia, mimi sio kama sitaki nikulipe ila mambo tu yamekua magumu, Kiufupi ktk hizo audio kwa maongezi anakubali kua nilimpa mzigo. Vile vile kituo cha polisi wakati anachukuliwa maelezo kakubali kuwa mzigo nilimpa akakimbia nao ila atanilipa, kabla ya kesi kufika mahakamani.

Sasa mimi nilitaka kujua, kwanza position yangu mimi, vp Mahakama inaweza ikaniazibu kwa kosa la kununua mali ya wizi, na swali la pili je Mahakama inaweza ikanipa haki yangu kwa kutumia ushahidi wa Screenshots na Audio?
 
kwanza umenunue mali ya wiziii... pili mahakamani hakuna hukumu ya kumfunga mdai yeye kakubali kweli kauza hela kala bhasi hela atakulipa taratibu na ndivyo mahakama itataka iwe sema tu jamaa atakuwa huru kusema atakulipa kiasi gani :D :D :D
 
Kesi ingekuwa nzuri upandewako ungekuwa na risiti, risiti ndio nyaraka inayothibitisha umiliki wako na si screenshot

Mfano, umezungumza kuwa ulinunua kwa huyo jamaa then kunamtu anamshtaki kuwa alimuibia. Ikiwa huyo anamshtaki anauthibitisho wakimaandishi na mashahidi niwazi utaingia matatani.

Angalizo. Ikiwa unanua kitu ambacho unaweza kupewa risiti basi hakikisha unapewa risiti. Pia ukiwa unanua kitu kutoka kwa MTU kisichokuwa na risiti basi hakikisha unapata nyaraka za mauziano yake na pia mnaandikishana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom