Nani mwenye jukumu la kurekodi yanayoendelea Mahakamani?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,943
6,863
Mara kadhaa nimesoma kuwa wakili walimuomba Jaji awasomee alichoandika. Hivi Mahakama haina stenographers ambao kazi yao ni kuweka kumbukumbu ya kinachoendelea?

Kama hiyo inashindikana, kwa nini wasirekodi kwa kutumia voice au video recorder? Mimi naona kumtegemea Jaji sio sahihi. Yeye achukuwe notes za kumsaidia lakini official kumbukumbu zichukuliww na mtu mwenye utaalam wa kufanya hivyo. Nadhani bungeni wapo.

Amandla...
 
Mbaya zaidi jaji anategemewa kuandika hizo notes ili zikamsaidie kwenye kuandaa hukumu, sasa inakuwaje kwenye kesi ya mchongo kama hii na jaji wa mchongo kama huyu, kuaminiwa kwenye notes zake?

Mahakama lazima ije na mbinu mpya za kuandika hizo notes, kwanza jaji kama mwanadamu kuna uwezekano mkubwa akasahau kuandika mambo ya muhimu yanayoweza kuja kuwa na maana kwenye hukumu.

Naunga mkono wazo la voice recorder ndio suluhisho la kudumu na la uhakika, japo nazo wanaweza kuzichezea kwa manufaa yao kama wanavyofanya kwenye ushahidi, ambapo tumeshaona upande wa jamhuri wanapewa nyaraka za kesi na mahakama kinyume cha sheria.
 
Jaji ana makarani wake. Ana timu ya kutosha kutoka ofisi ya msajili wa division husika.
 
Wako wapi? Wana rekodi kwa remote? Kwa nini Kibatala alipomuomba clarification kuhusu jambo fulani hakumuambia karani wake asome alicho andika?
Sijawahi kusikia jaji akimuagiza karani akumbushie jambo ambalo mawakili hawalikumbuki. Yeye anasoma notes zake kila wakati. Kama hao makarani wapo basi hawatumiki au majaji hawana imani na uwezo wao.

Jaji ndio mwenyekiti wa session ya mahakama. Jaji ndio msemaji wa session.
 
..OK

..unasema Jaji ndio mwenyekiti wa session.

..mtoa mada anataka afahamishwe Katibu au mtunza kumbukumbu wa session ni nani?
Asante Mkuu. Hata katika vikao vyetu vya harusi, Mwenyekiti hachukui minutes. Hata bungeni sidhani kama Spika anafanya kazi za Katibu. Kwenye Mahakama za wenzetu wachukua kumbukumbu wanaonekana wazi. Hii inamruhusu Jaji ku concentrate kwenye yanayoendelea mbele yake na kuondoa hisia kuwa ataegemea upande mmoja katika utunzaji wake wa kumbukumbu.

Amandla...
 
Jaji ana makarani wake. Ana timu ya kutosha kutoka ofisi ya msajili wa division husika.
Bado hii ni njia ya kijima, mbona bungeni wana mitambo ya kurekodi ili baadae iingie kwenye hansard? Kuna siku huyu jaji wa michango aliombwa atoe maelezo ya shahidi ya siku iliyopita akamdanganya wakili wa utetezi, Sema akina Kibatala wakakomaa mpaka akabadili..
 
Asante Mkuu. Hata katika vikao vyetu vya harusi, Mwenyekiti hachukui minutes. Hata bungeni sidhani kama Spika anafanya kazi za Katibu. Kwenye Mahakama za wenzetu wachukua kumbukumbu wanaonekana wazi. Hii inamruhusu Jaji ku concentrate kwenye yanayoendelea mbele yake na kuondoa hisia kuwa ataegemea upande mmoja katika utunzaji wake wa kumbukumbu.

Amandla...

Mbaya zaidi jaji anategemewa kuandika hizo notes ili zikamsaidie kwenye kuandaa hukumu, sasa inakuwaje kwenye kesi ya mchongo kama hii na jaji wa mchongo kama huyu, kuaminiwa kwenye notes zake?

Mahakama lazima ije na mbinu mpya za kuandika hizo notes, kwanza jaji kama mwanadamu kuna uwezekano mkubwa akasahau kuandika mambo ya muhimu yanayoweza kuja kuwa na maana kwenye hukumu.

Naunga mkono wazo la voice recorder ndio suluhisho la kudumu na la uhakika, japo nazo wanaweza kuzichezea kwa manufaa yao kama wanavyofanya kwenye ushahidi, ambapo tumeshaona upande wa jamhuri wanapewa nyaraka za kesi na mahakama kinyume cha sheria.

Mitandaoni kila mtu anajua kila kitu. Shida yenu mnaangalia maneno mengi bila kujua kuwa pale kuna issues ambazo zinapingwa au kusupportiwa.

Majudge ni kama mwalimu tu kuelewa swali ndo mwanzo wa kufaulu. Angalia kesi ya uchaguzi kenya. Prof L. Alikuwa na maneno mazuri kwa walay kama Sisi Lakini alishindwa kwa kuwa mwenzake alikuwa specific kwenye issues at hand.
 
Sasa wewe unaejua si ungetuambia nani anachukua kumbukumbu Mahakamani? Mimi sijazungumzia weledi wa Jaji. Ningekua najua kila kitu nisingeuliza.

Amandla...
 
Back
Top Bottom