Nani atapata mali zangu ikiwa nimeachana na mwanamke wa ndoa aliyenikuta na mali?

Kwahiyo za nani? Za kwako? Wanandoa mnagomba na kutengana na hao watoto mlioleta duniani kwa raha zenu waishi wapi? Automatically mali za wazazi ni zao labda muwe wavuta bangi muziuze na kuwatelekeza watoto stand ya Magufuli
Wanawake mnajikuta mna msimamo sana kwenye mgawanyiko wa mali. Unataka mgao ambao ujachangia chochote cha kushangaza nyie ni wabinafsi kupita maelezo. Tafuteni mali zenu mkiachana kila mtu achukue alichokitolea jasho. Mkiachana ondoka kwenye nyumba ya mwenzako kama hauna pa kwenda acha watoto rudi kwenu pambana utengeneze nyumba yako mwenyewe
 
Ukishatanguliza mawazo ya ubinafsi kama hivi ndoa yako inaelekea itakuja kuwa na changamoto kubwa sana.

Halafu kuna jambo silielewi elewi, hizo mali mkifa mnazikontroo vipi kwa mfano!?. Tuseme umehangaika umepambana ukapata mali za kutosha halafu ghafla ukapata ajali ukafa ,unazikontroo vipi mali zako?

Hatutaishi milele
Mkuu wanawake wa sasa wapo kimasilahi zaidi, to date them while your are stable financialy its a dance with a devil, lazima uende nao kwa machale.
 
Mali mnagawana mlizochuma pamoja

1699986774275.png
 
Wakati unaoana na mwanamke unapaswa kuandika document ya mali alizozikuta na yeye asign kukubali, kama ukifanya hivyo then mkitalikiana hazitahusishwa naye!

Ila chagua mke kwa umakini na ondoa hayo mawazo mabaya, ukiwaza hivyo utaishi maisha ya shida na hutamfurahia Mwanamke, achana na story za kataa ndoa.

Hivi ukioa, ukazaa na mwanamke watoto wa 3, anapenda wanawe na ni Mama mwema, kumuachia mali unaona tabu gani? Mimi sioni shida kabisa.
Huo ni ubinafsi Sasa yaan unaweza oa mke alafu ukaanza mambo hayo why usitafute document zako before then uoe
 
Hata hivyo mkizaa watoto, hizo mali ni za watoto na wakiwa bado ni wadogo utaambiwa uondoke hapo abaki mke na watoto!
Sio kweli, mali za ndoa ni za wanandoa. Hili swala kuna hadi case laws zilizosisitiza hili. Nasema hivi sababu sheria ni fani yangu na hili ni eneo ninalofanyia kazi zaidi (kuvunja ndoa za walichokana kistaarabu 😂)

Kuna kesi moja wanandoa walikuwa na mali wakapata talaka kisha mahakama ya chini ikajichanganya kwa kuwapa watoto mali zilizokuwapo. Kesi ikakatiwa rufaa ikaenda Mahakama Kuu, Jaji akapiga chini maamuzi ya Mahakama ya chini na kusema kuwa, mali za ndoa ni za wanandoa na hazipaswi kugawanywa kwa watoto.

Sikumbuki jina kamili la hii kesi, ila unaweza kuitafuta Tanzlii.org kwa key words ambazo ni distribution of matrimonial properties distribution of matrimonial properties to children

Nikimjibu mleta uzi, hilo swala lake linawezekana kabisa akazitenga mali za kabla ya ndoa kati yao na zikabaki kuwa mali binafsi na pale watakapo talakiana zikabaki kuwa mali binafsi.

Pia mali zilizopatikana kabla ya ndoa zinaweza kufikiriwa kugawanywa au kuwawiwa kwa mwenza aliyeikuta kama tu ataweza kuonesha mchango wake kwenye kuendeleza hiyo mali.

Hii haki ya mgawanyo sio haki ya jumla -automatic right_ bali ni haki ya kuionesha ilipotokea.

Hii mada ni pana sana sababu watu wengi wanaenda kwa mazoea bila kuisoma sheria husika.

Pakiwa na swali, karibuni wadau nitajitahidi kujibu kwa wakati.
 
Sio kweli, mali za ndoa ni za wanandoa. Hili swala kuna hadi case laws zilizosisitiza hili. Nasema hivi sababu sheria ni fani yangu na hili ni eneo ninalofanyia kazi zaidi (kuvunja ndoa za walichokana kistaarabu )

Kuna kesi moja wanandoa walikuwa na mali wakapata talaka kisha mahakama ya chini ikajichanganya kwa kuwapa watoto mali zilizokuwapo. Kesi ikakatiwa rufaa ikaenda Mahakama Kuu, Jaji akapiga chini maamuzi ya Mahakama ya chini na kusema kuwa, mali za ndoa ni za wanandoa na hazipaswi kugawanywa kwa watoto.

Sikumbuki jina kamili la hii kesi, ila unaweza kuitafuta Tanzlii.org kwa key words ambazo ni distribution of matrimonial properties distribution of matrimonial properties to children

Nikimjibu mleta uzi, hilo swala lake linawezekana kabisa akazitenga mali za kabla ya ndoa kati yao na zikabaki kuwa mali binafsi na pale watakapo talakiana zikabaki kuwa mali binafsi.

Pia mali zilizopatikana kabla ya ndoa zinaweza kufikiriwa kugawanywa au kuwawiwa kwa mwenza aliyeikuta kama tu ataweza kuonesha mchango wake kwenye kuendeleza hiyo mali.

Hii haki ya mgawanyo sio haki ya jumla -automatic right_ bali ni haki ya kuionesha ilipotokea.

Hii mada ni pana sana sababu watu wengi wanaenda kwa mazoea bila kuisoma sheria husika.

Pakiwa na swali, karibuni wadau nitajitahidi kujibu kwa wakati.
Mkuu wanawake wa kisasa wamekua matapeli sana embu tupe mbinu mkuu, kwa upande wetu wanaume ni nini tunaweza kufanya ili tunapoachana kila mtu abaki na mali yake? Mfano kuandikishiana kwenye cheti cha ndoa hakutakua na mgawanyo mali tukitalakiana iyo inawezekana?
 
Ukifunga ndoa hizo mali zote alizokukuta nazo ni zenu woote! Kama hutaki ahusike nenda mahakamani uandikishe mali zako alizokukuta nazo ili kwamba mkija kutengana mgawane kile mlichochuma wote! Hata hivyo jichanganye na mke wa kichaga uone mziki wake kama hajakutanguliza ahera!
Naona wachagga imekuwa personal sasa hahahhha
 
Mkuu wanawake wa kisasa wamekua matapeli sana embu tupe mbinu mkuu, kwa upande wetu wanaume ni nini tunaweza kufanya ili tunapoachana kila mtu abaki na mali yake? Mfano kuandikishiana kwenye cheti cha ndoa hakutakua na mgawanyo mali tukitalakiana iyo inawezekana?
Usiogope kuoa Mkuu, ni muhimu kabla ya kuoa au kuolewa watu washirikishe Wakili.

Maana ndoa ni mkataba ila ajabu watu wengi wanaingia kwenye huu mkataba kwa kutumia hisia na sio akili.

Mbinu ni hii, tumia akili kwenye kuoa na sio hisia.
 
Back
Top Bottom