Nani atapata mali zangu ikiwa nimeachana na mwanamke wa ndoa aliyenikuta na mali?

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Habari zenu wakuu.

Nimekuwa naona nyuzi nyingi sana watu wakilalamika wanawake wao kuchepuka nje ndoa na kupelekea ndoa kuvunjika.

Mimi ni kijana ambae nina mpango wa kuoa huko mbeleni (Sio leo wala kesho) na moja ya mipango yangu ni kuoa nikiwa nishakuwa na assets za kutosha.

Kutokana na dunia ya sasa kuharibika mpaka vijana wenzangu wengi kukataa ndoa, naomba kuuliza hili swali.

Ikitokea nikamuacha Mwanamke wa ndoa alienikuta nina mali zangu, je na yeye atapata mali zangu?

Nitashukuru mkinijibu wakuu.

Naomba nisaidiwe kwenye hili.
 
Ukifunga ndoa hizo mali zote alizokukuta nazo ni zenu woote! Kama hutaki ahusike nenda mahakamani uandikishe mali zako alizokukuta nazo ili kwamba mkija kutengana mgawane kile mlichochuma wote! Hata hivyo jichanganye na mke wa kichaga uone mziki wake kama hajakutanguliza ahera!
 
Mkuu, mali za wanandoa haziwezi kuwa za watoto kama wanandoa hawajataka hivyo. Mahakama kazi yake ni kufanya mgawanyo wa mali kutokana na mchango mwanandoa aliochangia katika upatikanaji wa mali hizo.
Kwahiyo za nani? Za kwako? Wanandoa mnagomba na kutengana na hao watoto mlioleta duniani kwa raha zenu waishi wapi? Automatically mali za wazazi ni zao labda muwe wavuta bangi muziuze na kuwatelekeza watoto stand ya Magufuli
 
Ukifunga ndoa hizo mali zote alizokukuta nazo ni zenu woote! Kama hutaki ahusike nenda mahakamani uandikishe malizako alizokukuta nazo ili kwamba mkija kutengana mgawane kile mlichochuma wote! Hata hivyo jichanganye na mke wa kichaga uone mziki wake kama ajakutanguliza ahera!
Mkuu haya uliyoandika ni kwa mujibu wa sheria ya ndoa au hearsay?
 
Ukishatanguliza mawazo ya ubinafsi kama hivi ndoa yako inaelekea itakuja kuwa na changamoto kubwa sana.

Halafu kuna jambo silielewi elewi, hizo mali mkifa mnazikontroo vipi kwa mfano!?. Tuseme umehangaika umepambana ukapata mali za kutosha halafu ghafla ukapata ajali ukafa ,unazikontroo vipi mali zako?

Hatutaishi milele
 
Mleta uzi pitia hapa ujielimishe kuna mkuu alishalifafanua

 
Habari zenu wakuu.

Nimekuwa naona nyuzi nyingi sana watu wakilalamika wanawake wao kuchepuka nje ndoa na kupelekea ndoa kuvunjika.

Mm ni kijana ambae nina mpango wa kuoa huko mbeleni (Sio leo wala kesho) na moja ya mipango yangu ni kuoa nikiwa nishakuwa na assets za kutosha eg. Nyumba, biashara n.k

Kutokana na dunia yasasa kuharibika mpka vijana wenzangu wengi kukataa ndoa, naomba kuuliza hili swali.

Ikitokea nikamuacha Mwanamke wa ndoa alienikuta nina mali zangu, je nayeye atapata mali zangu?

Nitashukuru mkinijibu Wakuu

Naomba nisaidiwe kwenye hili.
Tafuta kwanza hizo mali, uwe nazo kisha ndo urudi hapa.
 
Sheria ya ndoa inaruhusu kumiliki mali binafsi
Screenshot_20231114-112416_Firefox.jpg
 
Naona comments nyingi za upotoshaji wa kisheria.
Jitahid kuwatumia wataalam wa fani husika kwa maarifa
Humu jamvini kuna wataalam wa kila aina,amelileta suala lake,eneo sahihi kabisa.
 
Ukifunga ndoa hizo mali zote alizokukuta nazo ni zenu woote! Kama hutaki ahusike nenda mahakamani uandikishe mali zako alizokukuta nazo ili kwamba mkija kutengana mgawane kile mlichochuma wote! Hata hivyo jichanganye na mke wa kichaga uone mziki wake kama hajakutanguliza ahera!
Asante kwa mchango wako Mkuu
 
Andika umiliki kwa jina la mtu mwingine unayemuamini au sajili kampuni na mali hizo ziandike kwa jina la kampuni yako, na wewe uwe ndio mwenye hisa nyingi. Asilimia 99
Asante kwa ushauri wako Mkuu.
 
Mleta uzi pitia hapa ujielimishe kuna mkuu alishalifafanua

Asante Mkuu, naupitia huo uzi.
 
Back
Top Bottom