Namuheshimu mama yangu lakini simpendi

Ndugu mama ni binadamu kama binadamu wengine na anastahili kurekebishika.kuna msemo kwamba kids are the best judges to parents sababu pendo kwa mzazi lipogo siku zote so u can fairly judge a parent.Heshima yake kama mzazi mpe na kamwe usimdharau ila kosa ni kujikalia kimya.
Siku mfungie safari mpelekee zawadi kama kawaida ila this time iwe safari yenye lengo la kumwambia ukweli.mwambie how much u love her and how u feel anakubagua.kuwa nae open na kama una uchungu lia kabisa ajue upo serious na imekuuma.ikiwezekana mkumbushe imcidences kwa kumpa mifano hai ya matukio akiyokubagua.
Afu hela mbaya, hawa ndugu wenye hela tatizo likitokea wanajua kutoa noti zao tu wakidhani wanafanya makubwa sana ila kiukweli si ajabu na wewe wa hali ya chini una mchango mkubwa. Mi ishawahi kutokea ikabidi niuguze ndugu wa saratani ila mtoa hela alikuwa mwingine..matunda, dawa na kila kitu kinanunuliwa ila kumuogesha mgonjwa sasa. Kufamka asubuhi mgonjwa ale na some days kulala nae usiku.mi nalala chini yeye kitandani akianza tu kulia maumivu na mi nimeamka kukaa nae mara tusali.wenye hela wamezitoa ndio ila kazi kama zile hakuna aliyefanya ila mimi nsie na kitu.na kweli yule mgonjwa kabla hajafariki alilia sana kunishukuru nilivokuwa nae kwa karibu kuliko hata hao watoto wake wenye pesa. Money is everything but not always..
Hivyo mamako asisahau kuna kuugua na si ajabu wewe ndo ukawa wa kumuogesha. Hata kama watoto wake wengine anaowahusudu wamemwaga pesa.kuna kitu kinaitwa touch..humpi mtu hata senti tano ila unamgusa kitofauti kabisa.
 
Neno nalo ubarikiwe kwa busara zako. Ikifika muda mtu anaumwa na anahitaji care nzito ndo atajua thamani ya utu na thamani ya pesa. Wenye pesa hapo watamwaga tu mapesa yao but atakayekuogesha, kukulisha, kukubadili nguo, kushika mavi yako etc ni mwingine asiye na kitu. Tuthamini utu
 
Last edited by a moderator:
Pole sana
Endelea kutoa heshma kwa wazazi wako zaidi jitume fanya kazi kwa bidii naamini nawe utapata hizo mali ambazo Mama anadhani ni bora.
 
Aisee hii ipo sana hata kwa waha kwani baba yangu naye alidharaulika wakati mambo hayajanyoka hivi sasa wanataka ushauri kwake kama wewe ni mkiristn bibria inasema mawazo ya masikini hayasikilizwi kata kama mazuri jipe moyo ipo cku watatia heshima

"mkiristn bibria..." ndio nini?
 
Dada Rose Marie naomba nikutie moyo kwamba tabia ya mama yako haipo uchagani tu, nimewaona wengi tu waliopitia changamoto kama yako ila baadae hali inabadilika.
Wewe chukulia tatizo la mama yako kama udhaifu, lakini jambo moja ambalo naweza kukulaumu, ni kwanini hujawahi kumuuliza mama yako kwanini akuthamini kwa sababu ya umaskini wako? pengine huo mtazamo ukawa ni wako binafsi na wala mama yako hakuchulii kama unavyodhani.
 
Last edited by a moderator:
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.

actions and reactions are always equal and opposite,umpendi kwa kuwa yeye hakupendi,uwezi kulazimisha upendo,is better to mind ur business,watu wanajari saana pesa kuliko utu siku hizi,ila pole saana kwa ilo ukiwa na mzazi kama uyo
 
Pole sana it happened ht ktk familia yetu when tulipokuwa wadogo bibi alimdharau sana baba mashangaz nko coz hakuwa na kitu hii imeniathr ht mm siwapend kabisa watu hao hasa mashangaz zng kila mtu na bussnes zake though hali imetengamaa bt kiukwel tabia hii n mbaya sana inaathr hasa kisaikologia
 
haya mapenzi ndg zangu! mimi nina kaka yng mtukutu sana na hamsaidii bimkubwa kwa lolote zaidi ya kuiba tunavyomletea mama. lakini sote tunajua jinsi bimkubwa anavyompenda jamaa. usimwambie endelea kutimiza majukumu yk kama mtoto.
 
we tafuta pesa mama anachukia umaskini wala akuchukii wewe acha kujistukia kaza buti umpe zawadi saka pesa acha utoto iko ivo pote we umeona leo
 
inferiority at its best, nadhani last stage ya kupata ukichaa.

Ni rahisi sana ku judge kama hayajakutokea au kushuhudia nimeshaona kaka mkubwa hashirikishwi vikao vya maamuzi ya family na hata kwenye msiba wanaitana pembeni wadogo na wazazi then jamaa anatumwa tu nenda sokoni kalete hiki na young brother kisa yeye hana kitu
 
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.
Kwetu unakuta kaka ndo anatumwa kukimbiza kuku, kuchinja na kunyonyoa kisa mdogo wake kaja na ana hela na lazima aheshimiwe! Na sisi hatuchukii zaidi ndo tunapata munkari zaidi na sisi kutafuta pesa ili na sisi siku moja atumwe mtu akimbize kuku for us!
Wazazi wetu wa kichaga hawabembelezi mtu asiyejituma kutafuta haswa akiwa wa kiume hata wa kike kama huna muelekeo utakaa home ufagie kwa ng'ombe utusubirie mwezi wa kumi na mbili tuje utupikie chakula na mwisho tukuachie vi elfu kumi siku tunaondoka.
I like it, na ndo maana tuna fight kufa kupona!


A man once said, No Guts....no Glory
 
mkuu mimi ni mwanaume na ni wa kwanza kuzaliwa,wadogo zangu wana uwezo lakini mimi sina uwezo sana ila mungu amenisaidia kuridhika na hali niliyo nayo


Kama wewe ni Muislam nitakwambia yafuatayo na hata kama ww si Muislam najua kuna AYA inayofanana na hii... kwenye Quran kuna yaya inayosema

1.Pepo ya mtoto iko kwenye nyayo ya wazazi wake hasa mama!! (tafsiri si sio ya neno kwa neno)

2. Kuna hadithi ya Mtume wetu inasema (SAW) kuna jamaa alineemeshwa sana rizik na Mola wetu, na hata akasema nani nimfanyie wema zaidi kati ya wazazi wangu wawili kama shukran kwa mola wangu? akakosa jibu , akaamua kwenda kwa Mtume kupata ushauri, Alipofika kwa mtume , akamuuliza Ya Rasulu llah ninani wa kwanza kati ya watu wangu ninaepaswa kumfanyia wema zaidi kama shukran kwa Mola kwa kuniruzuk mali? Mtume akamjibu .. Mama yako, wa pili mtume akasema , Mama yako, na watatu Mtume akasema Baba yako. Jamaa akamuuliza mbona mama umerudia marambili?? mtume akasema wa kwanza ni mama yako na wa pili ni ndugu za mama yako na watatu ni baba yako. Hekima hapa ni kuhakikisha Mama anafurahi no matter what..... komaa nae upate baraka zake

3. Kuna aya Inasema tuwatii wazazi wetu na tuongee nao kwa utaratibu na tusionyeshe hasira au chuki mbele yao ili tupade msamaha toka kwa mola, labda tu kama watataka kumshirikisha MUNGU hapo tumeambiwa tusiwatii ila si kuwachukia ( tafsiri si neno kwa neno) NAKUUSIA NDUGU FANYA SUBRA MAANA MOLA WAKO ANAONA MADHILA UYAPATAYO NA SHINDA MTIHANI HUU
 
Huu Uzi wa 2011 nadhani walishaanza kupendana kabisa ..upendo wa mama na mwana hakunaga kama..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom