Namuheshimu mama yangu lakini simpendi

wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.
Pole mkuu...sijui kwann nashangaa na kuhisi kuwa we si mchaga...kule uchagani hii ni kawaida kabisa.
 
Pole mkuu...sijui kwann nashangaa na kuhisi kuwa we si mchaga...kule uchagani hii ni kawaida kabisa.

mkuu hata mie mchaga
kwanza hata siendagi moshi kwa sababu sina hela
acha wakae na roho zao za kupenda pesa kuliko jambo lolote
nimetulia na muhehe wangu tunakula maisha,niwe na pesa nisiwe nazo bado napata heshima kutoka kwake
kwanza sitaki demu wa kichaga
 
Kina mama siku hizi nao hawaaminiki. Kuna jamaa yangu alimkarabatia mama yake mabanda ili wapate rent nzuri, akawa kajenga nae kijumba akakipangisha ili mama awe assured na life wakati jamaa alisafiri kwenda shule. Jamaa baadae kaoa mtu wa kwao so hakuna cultural crash. Maisha yakaendelea lakini mama anampenda mume Wa binti yake yaani kila anachofanya yy mafuta tu kisa ndugu wakienda jamaa anawapa elfu kumi kumi za nauli. Ikafikia mama ana mkampenia ndugu wamwone jamaa mbaya. Jamaa sababu ya kuchukiwa ni mama anamtaka jamaa asaidie ukoo mzima jamaa anasema mimi hadi mtu afanye kazi ndio tunasaidiana siyo kuja tu naomba hela. Basi jamaa kuona hivyo yy kawapa space waendelee na upendo kwa mkwe lakini hardly anakaa kwa mama yake hata akiwa likizo. Jamaa yy kajikita kutafuta life ila anasaidia mara chachechache kwa mama kama ugonjwa lkn jamaa yuko fine mambo yake juzi kati kafungua mradi kaajiri watu baki maana ndugu wameshakuwa twisted mind zao wanafuata mama. Lakini juzi hapa kasema ndugu wameanza kumuomba ushauri wameona mama ndio kawa lostisha. So siyo siku zote wa mama wako sawa.
 
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.
Maswali ya hovyio uwa na majibu ya hovyio,inaonyesha hata baba yako alipendewa ela.All in all pambana upate ela utapendwa tu
 
Mzee wewe una familia yako na mkeo na watoto unataka heshima ya nini toka kwa mama. Mkeo akisikia na yeye atakudharau na watoto pia. Kuna sababu ya mtu kupewa utajiri na mtu kupewa utoshelezi. Jamii unayoishi nayo lazima uionyeshe upendo wa kweli ili siku moja mama atambue kuwa una thamani mbele ya watu wengine, na kuna na atakuthamini. Kama ni mcha mungu uende ukataubu maana huwezi sema asante hata kwa mafanikio madogo uliyopata. Unless hujui maisha kuna siri kubwa '' utajiri''. Je kwa nini uutese moyo wako kwa mambo ya dunia na kuacha furaha yako.
 
Unaweza usikubaliane na nitakachosema ila ni ukweli mtupu.
Episodes,u will remain POOR FOREVER kama hautafungua moyo,ukamsamehe mama yako na ukaanza maisha mapya mkiwa kwenye good terms.
Kumheshimu na kumchukia mama yako hata Mungu hapendi mana alishatuagiza kuhusu wazazi wetu kwenye amri 10 za Mungu.
Fanya hivi,nakuhakikishia utafanikiwa na atakupenda pengine zaidi ya wote.
Tafuta muda uwe wewe na mama yako tu,mweleze unavyojiskia then msikilize, baada yapo,apologise na umwombe akubariki then rudi mjini, mambo utakayoyapata utamshangaa Mungu sana, tena usisahau mama ni mama tuuuuu
Nani kama mama??????????????
 
Na mimi nakubaliana na maneno ya wahenga kuwa hilo kabila wengi wana roho za kipalestina. I wish angekuziba pua zako kwa manyonyo yake wakati uko kachanga ndo ingekuwa suluhu ya upuuzi wako.[/QUOTE]

Mungu na akusamehe ndugu yangu, nadhani yeye mwenyewe anaichukia hiyo hali ya kutompenda mama yake ndio maana ameirusha hapa ili umshauri, punguza ukali wa maneno kidogo na umsaidie ili awe na upendo na mama yake
 
Kazi kidogo huyo mom anapenda chapaa zaidi na wadogo zako wanamtoa zaidi. Fanya hivi, waulize ndugu zako wanaichukuliaje hiyo hali? Wanafurahishwa? Kama hapana watatatuaje tatizo? Kama watakupuuza hunabudi kufanya mambo yako kimyakimya na kukubaliana na hali ulionayo ikosiku utakuwa na thamani. Pia kumbuka dunia tunapita hakuna kisicho na mwisho, wapo wenye matatizo zaidi ya yako lakini wamekubali na wanafurahia maisha.
 
mkuu baba yangu hakuwa tajiri,tuliishi maisha ya kawaida kabisa,lakini waliweza kutulea
kwa kweli jambo la kusema tulazimishe kupata mali mimi nipo kinyume kabisa
naishi maisha ya kawaida nina nyumba,kazi na kausafiri,na nina watoto wangu wazuri sana
jamani nifanye nini mimi ili niheshimike?


una - NYUMBA, KAZI NA USAFIRI - MKE, WATOTO WAZURI.......bado unajiita maskini???? mh! kwani ndugu zako wana mali zipi ambazo unaona wamekuzidi sana???

Halafu MAMA YAKO HAKUHESHIMU............... yaani hapendi kufika kwako........?? hapendi kusikiliza mawazo yako????........ bado hapo mimi sijakuelewa
jiangalie wewe mwenyewe - unapokuwa na mama yako - unaongea busara??? wewe unamheshimu au unampenda tu moyoni??? je unampa zawadi mama yako na kuonyesha upendo kwake kama MAMA??? unaruhusu watoto wako wazuri wawe karibu na mama yako (bibi yao) - je mke wako anamheshimu Mama yako??? Mambo mengi sana yanaweza changia uhusiano wako na mama yako - HIVYO USIANZE KUMLAUMU - JICHUNGUZE KWANZA wewe mwenyewe
 
Wengi wamesema ni shurti umheshimu mama yako na milango yako itafunguka...wachagga(ndugu) ni watu wa kusaidiana saana wanasomeshana/peana mitaji nk..sasa imikuwaje wewe?...jikague usije ukawa unakikimbia kivuli chako..wapende/wafurahie ndugu zako na ikiwezekana zungumza nao na wewe uwe unapewa vijizawadi wakati wa kwenda mgombani, si ndugu zako hakuna mbaaya..uchagani kuna baraka za wazazi na kuna makusudi yanafanyika ktk kuzipataa..ufalme hunyakuliwa na wenye nguvu..na wazazi hawa husomesha kwa nguvu zoote wakijua siku moja watajasaidiwa miwani kama siyo nyumba za kisasa na watoto.. sasa wewe unalewa huko keko magurumbasi mwaka mzima afu unaenda kumpiga sound/kuchori vigift vyake lazima akuone siyo..
 
Pole sana Mkuu,
Lakini kwa namna yoyote ile ndani ya imani na nje ya imani uwe mwamini Mungu ama siyo mwamini Mungu
Samehe, tumeumbwa sana kuwa wasamehevu, maana tuliopoambiwa tusamehe ni kwa sababu wapo
watakao tukosea nasi tunawakosea, sasa unapaswa kumsamehe mama yako na kuchukulia hilo ni sehemu
ya kosa ambalo mwanadamu anapaswa kusamehe, wala usijione mpweke, ama kutengeneza kinyongo naye
maana huna cha kulipizia ubaya unauona umetendewa/unatendewa na mama huyo ni mama yako na mama kwa wengine
pia, sisi kama jamii tunapaswa kumsamehe na hivyo wewe huna budi
 
Duuuh!! hiyo nilikuwa siijui kumbe ndg zetu wako huko ndo mko hivyo!!!
 
Kufahamu kuwa humpendi ni nzuri sana. Ila kumchukia umefanya kosa.
Jitahidi unapokwenda,jitahid kumpenda,kwasababu ni mamako.
Fahamu anaugonjwa asioufahamu "service disease".
Anafikiri huyo mwenye uwezo pekee ndiye atakayemsaidia.
Sasa hupaswi kusumbua kichwa kufikiria anayokufanyia mama.
Omba uzima, akili, nguvu na maarifa utengeneze maisha yako.
Wangapi wanatoka kimaisha bila msaada wa mama zao bwana.
Inaniuma. Usimtukane wala kuonesha dalili yoyote ya hilo ulilolisema.Pole sana.
 
1. Hakika tatizo limeanzia kwa Baba yako kuwa na mahusiano mabaya na Mama yako ..wala usipepese macho kwingine kutafuta chanzo.
2. Mchakato alioutoa BOSS ..ni wa kina na msingi.. katika kukuwezesha wewe kuona msingi na chazo cha tatizo ... Lazima ujikubali kuona ukweli huu.
3. Picha ya Baba ya msuguano na Mama imebaki ndani ya moyo wa Mama .. na Picha Hiyo ndio tatizo linalimsukuma Mama Kufanya anachokufanyia bila yeye kujua. Mama alimchukia Baba na hivyo kambeba moyoni ... hata kama Baba kafariki lakini ..Yuko Hai kama chuki na ugomvi ndani ya Moyo wa Mama.
4. Kwa kawaida Picha iliyo Moyoni kwa Mama ... Inahitaji ... Kitu halisi kinachofanana nayo kabisa... Kitu halisi Kiliokuwa Ni Baba Yako sasa Hayuko na wewe ndio Umekuwa KITU HALISI. (Boss kwa usahihi alisema umemreplace Baba)
5. KIJINGA TU!! Mama anakufanyia mambo yote yaliyo moyoni kwa niaba ya Baba yako...(Na wewe Kila unapomchukia kukasirikia na kuweka kinyogo unahalalisha hali hii ... Usifanye kosa hilo la kijinga tu!)
6. Nenda sasa hivi kamueleze Mama yako nilichaadika hapa MUELEZR/ONGEA NAYE ..kwa utulivu , Uimara Na upendo wa dhati na ujasiri alafu uje ulete jibu Nini Kimemtokea Mama Yako Na Nini Kimekutokea ... Nategemea utakiunguza hicho Mama alichokibeba... Ikiwa vipi Ni (PM)
7. Ni Lazima kuvunja huu mtandao wa wewe kufanywa kuwa kama BABA YAKO kwani itaendelea kizazi hadi kizazi ....KWANI Kwa hakika ... Baba aliye mzaa Mama yako (Babu yako) alipta matatizo yanayokaribiana kama hayo unayopata sasa hivi kwenye familia yao...Pia ... Mama anaye mzaa Mama yako ..alimfanyia Kaka wa Mama yako (Mjomba) jambo kama hilo ... Fanya utafiti leta majibu hapa tukueleze ... Hiyo Programing inavyotokea.. Just a simple programing ..na wewe ukiedelea bila kuelimika vya kutosha ..Mwanao wa Kiume(Kama unaye) ..atayapta hayohayo toka kwa Mkeo ... Maana kwa vyovyote vile ..Kwa Mbali Mkeo ataanza kufanana na Mama yako mapka itaanza kukutisha..!!
8. Kuharibu hiyo programing Kifupi kabisa ni Kutokuzalisha hisia hasi za chuki, hasira, kinyongo, kukureka nk (negative emotions ) kwa Mama, Mkeo, Upweke wa kumkosa Baba na wote wanao huzika kwenye mchakato huu... wengi wameonyesha ukwlei huu kwa kutumia neno la Mungu.
 
mkuu hata mie mchaga
kwanza hata siendagi moshi kwa sababu sina hela
acha wakae na roho zao za kupenda pesa kuliko jambo lolote
nimetulia na muhehe wangu tunakula maisha,niwe na pesa nisiwe nazo bado napata heshima kutoka kwake
kwanza sitaki demu wa kichaga

hapo kwenye blue na red
 
Pole sana kwa hali inayokutokea wazazi wa namna hii wapo kwenye jamii inayotuzunguka kikubwa ondokana na mawazo ya kujiona wewe maskini kwa ulivyojieleza wewe una maisha mazuri kabisa usimkufuru Mungu kwa hicho ulichonacho............endelea kwenda nyumbani na toa kile ulichonacho kwa mama yako taratibu wazo la kumchukua litaondoka na utakuwa wa kawaida usijali hakupendi yupo anayekupenda sana na siku moja atamwezesha mama yako kukupenda tena
 
wakuu nawashukuru wote mliochangia,sikuwepo nilikuwa vijijini na hamna mtandao,nimewaelewa na ninafanyia kazi
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom