Nampendekeza huyu kuwa katibu mkuu wizara ya afya!!

Katanga namfaham alikuwa kinondoni,alitaka kutufungia makulaji ye2 ya kitimoto sinza ccm palestina coz ya uchafu,anae refaaaaa
 
Huyu Bwana ni mchapakazi mzuri sana.
Alikuwa Dar-es Salaam(sikumbuki Halmashauri gani), Akahamishiwa Singida kuwa Katibu tawala wa Mkoa then akaenda Morogoro.
Mwaka jana aliteuliwa kuwa k/katibu mkuu kabla ya kuwa katibu mkuu kamili wa Wizara ya Maendeleo ya jamii na watoto na sasa ni Katibu mkuu TAMISEMI.
Huko kote alikopita amekuwa mchapakazi mzuri sana kwa mfano mkoa wa singida na Morogoro alihakkikisha kwamba analipa madai yote ya malimbikizo ya wafanyakazi wa AFYA, amesimamia vizuri sana ujenzi na uboreshaji wa Hospitali za mikoa-Singida na Morogoro ndani ya muda mfupi sana....Ndipo Mheshimiwa Raisi akamwona na kumpandisha cheo

Bwn. Hussein Katanga!! nadhani anafaa kuchukua kiti cha Blandina Nyoni

Pale kinondoni hajatokea Mkurugenzi kama yeye alieweka mipango na halmashauri ikakusanya mapato makubwa mpaka leo analiliwa kinondoni hajapata mrithi japo hakupendwa na kina Lon...nakushukuru kwa kumuona ila muache alipo anafaa sana.
 
huyu jamaa namfaham ni bora hata mwana...jakaya kikwete aliyeiaibisha feza girls.mweupeee

Acha unafiki humjui wewe hawa wote wanaokupa recod zake hawatungi hapa ila ni kweli tupu...siungi mkono apewe wizara ya Afya aachwe Tamisemi kwani inakusanya afya,elimu,utwala,halmashauri nk.Viwizara vingine ni kama wakina nyoni vinawafaa.
 
Baba mwanaasha amchague OSCAR KAITABA huyu jamaa yuko safi xana nyoni mwenyewe anajua uwanaharakati wake pale wizarani.
 
Umeamua kujifagilia Mwenyewe?
naunga mkono hoja huyu aliwahi kuwa mkurugenzi wilaya ya mbinga,alifanikiwa kununua magari mengi ,alitengeneza barabara zote za wilaya,upande wa elimu wilaya ilikuwa nafasi ya nne kwa kipindi kirefu,baadaye aliteuliwa kuwa mfanyakazi bora sikumbuki mwaka,pia baada ya kazi nzuri alihamishiwa ILALA manicipal.Niseme kitu hapa mkoa wa Ruvuma toka enzi ya Mwalimu haukuwahi kuwa na kiongozi kama yeye Hussen Katanga,na mkuu wake wa mkoa Said Said Kalembo,Katanga ni Kiongozi hasa sio mtawala,walimu wa mbinga na watumishi wengine kilasiku wanamkumbuka sana,wakuu mtanisamehe kwa kiswahili changu.
 
Bw Kattanga abaki kule TAMISEMI aendelee na kazi nzuri ya kunyoosha Halmashauri. Halmashauri zina matatizo mengi na huyu Bwana anachukua hatua nzuri sana. Akiondoka pale jitihada alizofanya zitakuwa hazijakamilika na wafanya maovu watasherekea.
 
Kwa hali iliyotokea na mambo yalivyoenda hadi madaktari kufanikiwa katika madai yao basi hapana shaka JK atamteua Daktari kuwa PS pale Wizarani. Prof. Kahamba wa MOI anafaa kuchukua nafasi hii. Nadhani ameishafundisha vijana wa kutosha kwenye fani ya neurology.
 
Hapa ndipo tunapokosea kutaja jina la mtu. Tabia ya viongozi wetu hawapendi kushauriwa hususan inapokuwa kwenye masuala kama haya. Si unakumbuka wakati wa Brother Ben W. M alipoambiwa amtoe Marehemu Ngororo alipokuwa KM wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na wanafunzi wa UDSM? Unakumbuka jibu alilokuwa amelitoa wakati huo? Ni kweli Bwana huyo angefaa lakini JK atamwona?
 
Mbona mnaharaka ya kumpendekeza mtu wa kureplace nafasi ambayo aliyekabidhiwa hajaondolewa rasmi? au mmesahau kilichozungumzwa jana na mh.kiranja mkuu mwana wa mkulima? nawakumbusha katibu wa wizara na mganga mkuu wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa mamunyamunya waloyafanya, waziri na naibu wake wasubiri ngonjera za rais. je, mmetafakari vya kutosha ktk (1)KUSIMAMISHWA KAZI KATIBU NA MGANGA. (2)HIZO NGONJERA ZA RAIS ZITAKUWAJE?
Nadhani mnaijua vizuri serikali tulonayo na watendaji wake.
 
Mbona mnaharaka ya kumpendekeza mtu wa kureplace nafasi ambayo aliyekabidhiwa hajaondolewa rasmi? au mmesahau kilichozungumzwa jana na mh.kiranja mkuu mwana wa mkulima? nawakumbusha katibu wa wizara na mganga mkuu wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa mamunyamunya waloyafanya, waziri na naibu wake wasubiri ngonjera za rais. je, mmetafakari vya kutosha ktk (1)KUSIMAMISHWA KAZI KATIBU NA MGANGA. (2)HIZO NGONJERA ZA RAIS ZITAKUWAJE?
Nadhani mnaijua vizuri serikali tulonayo na watendaji wake. YANGU MACHO!
 
Huyu Bwana ni mchapakazi mzuri sana.
Alikuwa Dar-es Salaam(sikumbuki Halmashauri gani), Akahamishiwa Singida kuwa Katibu tawala wa Mkoa then akaenda Morogoro.
Mwaka jana aliteuliwa kuwa k/katibu mkuu kabla ya kuwa katibu mkuu kamili wa Wizara ya Maendeleo ya jamii na watoto na sasa ni Katibu mkuu TAMISEMI.
Huko kote alikopita amekuwa mchapakazi mzuri sana kwa mfano mkoa wa singida na Morogoro alihakkikisha kwamba analipa madai yote ya malimbikizo ya wafanyakazi wa AFYA, amesimamia vizuri sana ujenzi na uboreshaji wa Hospitali za mikoa-Singida na Morogoro ndani ya muda mfupi sana....Ndipo Mheshimiwa Raisi akamwona na kumpandisha cheo

Bwn. Hussein Katanga!! nadhani anafaa kuchukua kiti cha Blandina Nyoni

Kabila lako, ndugu yako, rafiki etc
 
Utendaji serikalini ulivyo wa ovyo hata akiwekwa mchapakazi wa aina gani sidhani Kama ataleta mabadiliko yoyote.
 
Back
Top Bottom